Yaliyojiri Ikulu Dar: Rais Magufuli amtaka CAG Kichere kutojifanya Muhimili mwingine, amwambia anaweza kuondolewa hata akiwa na mwaka mmoja

Yaliyojiri Ikulu Dar: Rais Magufuli amtaka CAG Kichere kutojifanya Muhimili mwingine, amwambia anaweza kuondolewa hata akiwa na mwaka mmoja

Katiba yetu inasiginwa.

Magu hakumpenda Assad na Assad atafanyiwa figisu ajute
 
Mwenye serikali yake ''Yupo''.......Hakuna cha muhimili wala mihimili hapa 😀 😀
 
Kwa kauli ya Rais unajua tu kabisa alikuwa hamtaki Proffesa Assad...et we ni mdhibiti wa hesabu za serikali na mwenye serikal yupo ...mwenye serikali ni nani kama sio sisi wapiga kura (wananchi) ,usiende kujifanya mhumili Kwan aliyetoka alifanya mhimili lini?
Au ndo huyo aliyekuwa anasema "Kuna mwingine tumeshauriana sana na katibu Mkuu kumtumbua tunashindwa "

Mtu kupata division one O na I level sio kigezo cha kumpatia kazi...wakati akiwa commissioner wa TRA hukuona hizo divionsin one ,mbona wakati ulisema ameshindwa kazi Leo ndo ataweza kazi ?
Tusubiri wizi mwingine wa matrioni yakienda chato .
 
........ntailinda na kuitetea Katiba ya JMT.........
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, leo Novemba 4, 2019 kuanzia majira ya saa tatu na nusu (3:30) asubuhi atawaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni



Wanaoapishwa ni pamoja na;
1. Charles Edward Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General – CAG)

2. Katarina Tengia Revocati kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe.

3. Mhandisi Aisha Amour kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait.

4. Kanali Francis Ronald Mbindi kuwa Kamishna wa Kazi katika Ofisi ya Waziri Mkuu

Aidha, Mhe. Rais Magufuli anawaapisha Majaji 12 wa Mahakama Kuu
*****

View attachment 1253571
IKULU: Charles Kichere akiapa kuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) akichukua nafasi ya Prof. Mussa Assad aliyekuwa CAG kwa miaka mitano - CAG Kichere alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe na awali alikuwa Kamishna Mkuu wa TRA

UPDATES:
Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma: Leo ni siku ya shukrani na tunamshukuru Rais kwa kutuongezea nguvu kazi. Tumeweza kupata watu bora Namshukuru pia Msajili Mkuu wa Mahakama kwa utumishi uliotukuka Mahakamani na naamini akifika Njombe atafanya kazi zaidi
View attachment 1253651

Prof. Juma: Asante Rais kwa kutuongezea Majaji 12, tukiondoa Majaji 2 wenye majukumu maalumu, nguvu kazi inabaki ni Majaji 76 - Majaji 2 watastaafu mwisho wa mwaka na watabaki 74 na mzigo kwa kila Jaji kwa sasa ni mashauri 518 na uwezo wa kila Jaji ni mashauri 220

Prof. Juma: Majaji tumejiwekea utaratibu wetu katika utendaji. Mfano, kila mwaka tunatakiwa kutoa mashauri angalau 220 kila Jaji, kuangalia hukumu zinatoka kwa wakati - Tuna mfumo wa kujiangalia wenyewe na kwa kujiangalia tunakuwa tunarudisha imani tuliyopewa na Katiba

Spika Job Ndugai: "Mlioteuliwa leo mmepata imani ya Rais Magufuli. Na kwa vile Watanzania walimuamini Rais Magufuli, basi mmepata imani ya Watanzania. "Ndugai akitoa neno kwa wateule walioapishwa na Rais leo. "Nakupongeza sana Mhe.rais kwa teuzi hizi, nawapongeza sana walioapishwa leo, mna imani ya watanzania, mnalo jukumu kubwa, tunawategemeeni sana"

Spika Job Ndugai: "Niwapongeze walioteuliwa, mmepewa imani kubwa kwa walioteuliwa. Kwa kuwa sisi sote tulimpa imani kubwa Mhe. Rais Dkt. Magufuli mjue pia mna imani ya watanzania wote. "CAG Kichere karibu sana, sisi Bunge tunaanza shughuli zetu kesho za kuangalia mipango ya Taifa ambayo inaweka vipaumbele ambavyo vitaisaidia Serikali kuona ni aina gani ya Bajeti ya Serikali ambayo itakuja 2020/21, wewe CAG ndio jicho letu tunakutegemea."
View attachment 1253671
Spika Job Ndugai: "Hivi karibuni Mhe. Rais alitembelea Gereza la Butimba na kutoa maagizo, hata mimi huwa natembelea sana Gereza la Kongwa, nawaomba majaji mkafanye kazi yenu ili kila mtu apate haki yake, anayestahiki kukaa gerezani akae asiyestahiki atolewe na arudi uraini. "Jicho ndiyo kila kitu kwa Binadamu bila jicho hujui unaenda wapi kwahiyo wewe CAG ni jicho letu tunakutegemea kushauri kuona namna ya kurekebisha na taaarifa yako inapojadiliwa Bungeni huwa ni taarifa nzito, tunaahidi kukusaidia kazi yako ni nzito."
View attachment 1253656
Rais Magufuli: Nawapongeza wote mlioapa leo. Zingatieni viapo vyenu mlivyovisoma leo. Pia, mkamtangulize Mungu katika kazi zenu - Nimeambiwa mmoja wa Majaji walioapa leo alifiwa na mke wake wiki iliyopita. Kassim pole sana, roho ya Marehemu ipumzike kwa Amani

Rais Magufuli: Ndugu zangu Majaji kafanyeni kazi ya haki. Judgement huwa inatolewa na Mungu tu ila kwa hapa Duniani mpo ninyi - Katoeni hukumu kwa haki ila haki hizo pia msizicheleweshe kwa sababu changamoto zipo sehemu mbalimbali, Waheshimiwa wamesema hapa

Rais Magufuli: Nakumbuka Jaji, aliyekuwa kwenye Fair Competation (si ni wewe?), huyu wakati akifanya kazi alishaamuliwa kufukuzwa kwasababu alisimamia haki - Walikuwa wanamshangaa kuona Mchaga asiyependa rushwa. Kwasababu pale kwenye Fair Competation kuna kazi

Rais Magufuli: Nendeni mkatimize wajibu wenu, mkawatumikie Watanzania hasa wanyonge ambao haki zao zinapotea - Mkienda kufanya kazi vizuri mtaipunguzia Tume ya Haki za Binadamu mzigo. Kafanyeni kazi

Rais Magufuli: Kamishna wa Kazi nawe kasimamie kazi hivyo hivyo, pale kuna changamoto nyingi. Kawanyooshe Wizara ya Kazi - Malata alifanya kazi nzuri ndio maana nimekaa naangalia muda wote nikaona panafaa Mwanajeshi wenye Qualification. Usiende pale kazi zikawa za hovyo

Rais Magufuli: Kwa CAG mpya nakutakia kazi njema. Usiende huko ukajifanya Muhimili. Mihimili ni mitatu tu na umeiona hapa Mahakama, Bunge na Sisi wa Serikali - Katika Kiapo chako ni Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali, kwa hiyo mwenye Serikali yupo

Rais Magufuli: Kafanye kazi zako za ukaguzi vizuri bila kuonea mtu. Unapopewa kazi na Mihimili mingine kama Bunge, katekeleze. Usibishane nao - Ukipewa maagizo na Mahakama katekeleze, wewe ni Mtumishi. Lakini pia kasimamie hiyo ofisi, kasimamie watendaji wako

Rais Magufuli: Kuna baadhi ya watendaji wako wanapopewa jukumu la kwenda kukagua kwenye Balozi wanalipwa fedha hapa na wakifika kule wanaomba pesa - Sitaki nikutajie majina yao, wewe nenda kule kachambue mwenyewe kwenye ofisi hii. Ofisi ya CAG sio Clean kama mnavyofikiria

Rais Magufuli: Nenda ukapange nafasi za watu wako ili mauchafuuchafu haya ukayasafishe. Najua una Qualification nzuri tu na hatufanyi makosa ktk kuteua - Form 4 umetoka na Div. I, Form 6 Div. I. Hii ni kuonesha wewe ni Kipanga sio Kilaza. Ukachukua Shahada ya Sheria na Account

Rais Magufuli: Tunakuamini. Pia, una heshima, umetolewa kwenye Ukamishna Jenerali wa TRA hukusema neno, 'You're humble, very polite' ukaenda ukafanya kazi huko - Wapo wengine ukiwateua wanafikiri ni nafasi zao. Unampa U-DC ukimtoa ananza kulalamika, wakati hakulalamika ukimteua
Magufuli kawatukana Wachaga kwamba wanapenda rushwa.
 
Inaonesha kuwa Assad alipitia vitisho vingi
 
Political interpreneur mbona anawaapisha haraka haraka kulikoni, jana uteuzi leo kuapishwa?
 
walianza na wahindi (magabacholi) wakatukawa wee
wakanyanyasika wee
wakaandamwa weee
wakafurushwa wee

Wahindi WAKAVUMILIA na Upepo mbaya ukapita..

sasa ni zamu ya wachaga na wanasemwa
ni wezi..
ila wameiba wapi?
mbona hawakamatwi?
magerezani wako wangapi?
mahakamani kuna kesi ngapi?

*wachaga wapo watumishi,wanafunzi,wakulima,mapadri,wachungaji,ma sheikh,wana JF,maaskari,na wanaccm..Je wote nao ni wezi.!?

Xenophobia ni nini.!?

jirani yangu ni mchaga... nafuga dog
 
Hii ni safi sana kwa walioteuliwa, hakika mheshimiwa kawaamini na kuwapa majukumu hayo. Good job Mr. President
 
Ivi Dodoma kashindwa kabisa kwenda uko? Nashindwa kuelewa kabisa ilikuwa ni siasa au mkakati nilitegemea mambo kama aya yafanyike Dodoma maana juzi tu kasema kashaamia uko.
Afya hairuhusu kutoka hapo nje ya nyumba. Akimaliza hayo majukumu hapo anaendelea na bed rest. Madaktari Bingwa wamehamishia ofisi zao hapo.
 
Mtu kupata division one O na I level sio kigezo cha kumpatia kazi...wakati akiwa commissioner wa TRA hukuona hizo divionsin one ,mbona wakati ulisema ameshindwa kazi Leo ndo ataweza kazi ?
Jitahidi kuwaza mbali kidogo basi...mbona majibu ya maswali yako kayajibu pale pale M. Rais! kumtoa pale TRA na kumpeleka Njombe alikuwa anapimwa 'humble' yake, uvumilivu wake katika kuchukulia mambo na maamuzi magumu juu yake na watanzania kwa ujumla. He was being tested for his patience !! Hupo ?
 
Ivi Dodoma kashindwa kabisa kwenda uko? Nashindwa kuelewa kabisa ilikuwa ni siasa au mkakati nilitegemea mambo kama aya yafanyike Dodoma maana juzi tu kasema kashaamia uko.
DSM ni DSM!
 
Mpiga kura ni mshenga tu
Kwa kauli ya Rais unajua tu kabisa alikuwa hamtaki Proffesa Assad...et we ni mdhibiti wa hesabu za serikali na mwenye serikal yupo ...mwenye serikali ni nani kama sio sisi wapiga kura (wananchi) ,usiende kujifanya mhumili Kwan aliyetoka alifanya mhimili lini?
Au ndo huyo aliyekuwa anasema "Kuna mwingine tumeshauriana sana na katibu Mkuu kumtumbua tunashindwa "

Mtu kupata division one O na I level sio kigezo cha kumpatia kazi...wakati akiwa commissioner wa TRA hukuona hizo divionsin one ,mbona wakati ulisema ameshindwa kazi Leo ndo ataweza kazi ?
Tusubiri wizi mwingine wa matrioni yakienda chato .
 
"Kwa CAG mpya nakutakia kazi njema, usije ukaenda huko ukajifanya na wewe ni mhimili, mihimili ni mitatu tu na umeiona hapa, na katika kiapo chako nilikuwa nakisikiliza nafasi yako ni Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kwahiyo mwenye Serikali yupo"- @MagufuliJP #MwananchiUpdates

"Katika maisha ya Duniani hapa huwezi kupewa mamlaka ya kuteua halafu usiwe na mamlaka ya kutengua, ukishindwa hivyo hufai kuwa Rais, CAG kasimamie kazi yako vizuri, mwenzako amemaliza miaka 5 yake, inaisha leo saa sita usiku, kesho nenda pale ofisini kayatoe mauchafu yaliyopo"-JPM
#KiapoIkulu
#MillardAyoIkuluUPDATES


Na katika kiapo chako (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali) nilikuwa nakisikiliza, nafasi yako ni Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kwa hiyo mwenye Serikali yupo, mwenye serikali yupo, kafanye kazi zako vizuri za ukaguzi bila kuonea watu.

Unapopewa maagizo na mihimili mingine kama Bunge katekeleze, usibishane nao. Ukipewa maagizo na mihimili kama Mahakama kaitekeleze, wewe ni mtumishi, wewe ni mtumishi.- Rais John Magufuli.
Kama kayasema haya hadharani je sirini kayasema yapi?

Kama anataka CAG awe upande wa serikali sasa unamkagiaje mtu uliye na maslai nae utamsaidiaje kulinda maslai ya umma?

Ivi CAG akiwa upande wa serikali nani atawasaidia umma kujua madhaifu ya serikali kwenye mapato na matumizi?

Ni kitu gani Magufuli analificha kwenye ukaguzi huru?

Kwanini mihimili yote anaifanya kuwa ya serikali?
 
Back
Top Bottom