Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yaani magaidi wa Uganda wanajilipua na mabomu lkn eti magaidi wetu walikua wamepanga kukata miti mabarabara,😄😄😄 Mizaha sana.Wakifanya hivyo tutafanya Maandamano ya Amani ya kupinga Ufashisti.
Salaam Wakuu,
Leo tarehe 17/11/2021 kesi ya Mwenyekiti wa CHEDEMA Freeman Mbowe inaendelea baada ya kuahirishwa siku ya jana.
Kujua jana kesi ilipoishia, soma: Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe: Jaji aahirisha kutoa uamuzi mpaka tarehe 17/11/2021 saa tatu asubuhi
Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.
UPDATES
- Jaji ameingia Mahakamani
- Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa
Wakili wa Serikali Robert Kidando anatambulisha
1. Pius Hilla
2. Abdallah Chavula
3. Nassoro Katuga
4. Jenitreza Kitali
5. Tulimanywa Majige
6. Esther Martin
7. Ignasi Mwinuka
Wakili Peter Kibatala anatambulisha Jopo la Mawakili wa Utetezi
1.Jeremiah Mtobesya
2. John Mallya
3. Dickson Matata
4. Idd Msawanga
5. Seleman Matauka
6. Khadija Aron
7. Evaresta Kisanga
- Jaji anaita Majina ya washtakiwa 1,2,3 na 4 na wote wanaitika kuashiria wapo...
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Uamuzi Mdogo, Tupo tayari
Wakili Peter Kibatala: Na sisi pia tupo Tayari Kuendelea kusikiliza Uamuzi na Kuendelea na Shauri
Jaji: Ni Kweli Kwamba Mahakama hii ilihairisha Shauri kwa ajili ya Kusoma Uamuzi na Uamuzi upo tayari na haya Ndiyo Maamuzi Yenyewe.
Jaji: Kwenye Shauri Maarufu Sana la Uingereza aliyekuwa Jaji Mkuu wa Uingereza Wakati huo alitoa Kauli ambayo inaisho Mpaka Leo, Kwamba Haki siyo tu Itendwe Bali ionekane Ikitendwa.. Na Kauli hiyo imekuwa Ikitumika Mpaka Leo pamoja na Shauri hili hili kuwa tofauti.
Kwa Mtu atakayesoma Uamuzi huu Hatoweza kuelea Kwanini Nimefika Uamuzi huu.. Historia inaonyesha Askari Polisi Mwenye Namba H4323 DC Msemwa alipokuwa anatoa Ushahidi Wake Mahakamani aliomba Kutoa Kielelezo Chake, Wakati anatoa Upande wa Utetezi walipinga.
Na wakati Pande zote Mbili Wakieendelea Kutoa Hoja, Basi Wakili Peter Kibatala Alisimama na Kusema Kwamba anaomba Kui' move Mahakama Kwamba Shahidi aliyepo Kizimbani ana Diary, pen na Simu...
Na Kwamba aliomba Mahakama Itamke Kwamba Siyo Shahidi Tena na Kwamba Ushahidi Wake ufutwe wote, Mahakama ili chukua Vitu Vile na Kwasababu Muda Ulikuwa Umekwenda sana Mahakama ilishindwa Kulishughulikia Jambo lile..
Na Mpaka Ilipofika 15 Mahakama Ilianza Kujiridhisha Kwamba Kama ingeweza Kujiridhisha kwa Kushughulika Simu. Hata hivyo Mahakama Ikaona hakuwa akitumia Simu Yake Basi Mahakama Ikaona arudishiwe Simu yake, Na Mahakama ikabakia na Diary na Pen
Hata hivyo Mahakama Ikawaelekeza Mawakili Kwamba wakafanye Utafiti, Itakapofika Tarehe 15 Waje na Utafiti, Ilipofika Siku ya Tarehe 15 Mahakama Ilishughulikia Suala Uamuzi Kwanza Kwamba Mahakama Ilielekeza Kielelezo Kipolewe na Kisomwe
Lakini Kabla ya Mahakama Haijasoma Kielelezo hicho basi Mtobesya Alisimama Kabla Shahidi hajasoma akaomba Mahakama Isikilize Jambo hilo kabla Shahidi hajasoma Kwa sababu akisoma Itaonekana aliendelea Kutoa Ushahidi, Upande Wa Mashtaka Wakasema hawana Pingamizi.
Jaji: Wakati Hoja inaletwa walisema waliona Jambo hilo wakati Mahakama Inaendelea, Wakasema Kwamba Shauri Linaundwa Juu Sheria ya Uhujumu Uchumi lakini Wakaona Sheria hiyo haisemi Moja kwa Moja.. Kifungu cha 28 cha Sheria hiyo kinaipa Mamlaka Mahakama Kutumia Sheria Nyingine.
Basi wakatumia Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai Kifungu cha 264, Basi Kwa Kutumia Kifungu hicho cha 28 na 264 ndiyo lilijenga Misingi Kwa wao Kuleta Jambo hilo. Wakasema Kwamba Shahidi anapokuwa Kizimbani hatakiwi Kuwa na Nyaraka Yoyote na Kwamba wakaomba Mahakama Itamke.
Kwamba Shahidi Hafai na Ushahidi Wake Ufutwe. Wakasema Kwamba Kuna Sheria Mbalimbali zinazoelekeza Jambo hilo Ka 168 ya Uhujumu Uchumi na PGO ya 282. Walitoa Hoja Mbalimbali kwa sababu ya Muda sito zitaja zote. Nitaje Kesi walizotumia wakati wa shauri hili Ka NANYARO Vs PENIEL
EDWARD ISACK SHAYO VS JAMHURI, OKUMU Vs UGANDA, GOODLUCK KYANDO Vs JAMHURI, Zote zimetumika katika kutoa Uamuzi huu. Msingi wa Hoja yao Kwamba Shahidi atakiwi Kuwa na Kitu chochote Wakati Mahakama Ikiendelea bila a Kibali Cha Mahakama.
Jaji: Ukweli ni kwamba Walimuona Shahidi Wakati Hoja zingine za Mawakili wa Serikali wakizitoa. Hakuna Ushahidi Kwamba alikuwa akirejea Jambo lolote. Kwa sababu hiyo waliiomba Mahakama i'presume Mambo yafuatayo kwamba wakati anaingia Kwenye Kizimba hicho aliingia nayo.
Kwamba Material ambayo aliingia nayo Wakati Mahakama aikiendele ionekane alitumia, Kwa sababu Aliingia na Nyaraka Bila Kibali cha Mahakama basi Shahidi aonekane ni Incompetent, Ushahidi ambao ameshautoa haufai, Na aondolewe Kutoa Ushahidi Mahakamani.
Na Kama itaonekana Suala la Kumuondoa Shahidi Ni Gumu basi Wakaomba Mahakama iruhusu Notebook Kukaguliwa na wao wapewe ili waweze Kutumia Notebook hiyo katika Maswali yao.. Kanuni inakataza Shahidi Kuingia na Nyaraka Kizimbani, Quran tukufu na Biblia Tukufu ndiyo Vitu Pekee.
Vinavyo Ruhusiwa Kuingia nayo Mahakamani, Kwamba Kwa Shahidi Kuingia na Mambo Mengine yanafanya Shahidi asiaminike. Mahakama ikaombwa Imkoseshe Sifa Shahidi Kwa Kutumia Kifungu cha 127 Sheria Ya Ushahidi. Kuhusu hilo Upande wa Mashtaka Walipinga Kwamba Vifungu hivyo siyo wezeshi
Jaji: Ukisoma Kifungu hiki Kinaweka Vigezo ambavyo ni wazi Vinavyoweza Kufanya Shahidi asitoe Ushahidi Wake Mahakamani.. Kwa Sababu hiyo naona Kwa Kifungu hichi Upande Wa Utetezi wametaja Kifungu Sahihi bil kujali Kama Wapo Sahihi ndani yake kuhusu Shahidi huyu.
Kuhusu Sheria Kesi ya EDWARD ISACK SHAYO VS JAMHURI haina Uhusiano katika kesi hii. Kwa kuwa Mahakama Ime' solve issue ya Jurisdiction imelimaliza.. Imebakia Issue kama Shahidi Vitu alivyokuwa navyo vinaruhusiwana Mahakamani.
Jaji: Mtakumbuka Mshtakiwa anaruhusiwa Kuingia na Vielelezo Kwenye Kizimba, Kwa hiyo Shahidi ambaye anatoa Ushahidi Anaweza Kuingia na Kielelezo Mpaka Muda atakapo Omba kutumia, Hili linaungwa Mkono na Sheria ya Ushahidi katika Kifungu 168(1)(2) ya Sheria ya Ushahidi.
Kwamba Shahidi anapokuwa anaendelea Kutoa Ushahidi Mahakamani hataruhisiwa Kufanya Ukumbusho, Wakati anaandika hiyo Nyaraka alikuwa na Kumbukumbu wakati huo, Na aliposoma andiko hilo lilikuwa Sahihi. Basi ukisoma PGO 282(7) A & A na Sheria ya Ushahidi Kifungu cha 168, 1 na 2.
Shahidi hakatazwi Kuingia na Kitu chochote Kwenye Kizimba, Na Kwamba Kabla hajafanya Marejeo ataomba Ruhusa Ya Mahakama, Jambo linalofuatia katika Shauri hili, Ni Wazi Hakuna Kilicho onekana kama Shahidi akiwa anafanya Rejea.
Jaji: Nakubalina na Kibatala na Mtobesya Kwamba hayo Yalifanyika wakati Shahidi ana Kiapo chake, Sheria inasema Kwamba Wakati amefungua alikuwa anafanya nini, Mahakama Inaona ni Kweli kwa yeye Kufungua na Kuandika ilikuwa ni VIOLATION.
Jambo linalofuatia ni Je baada ya Violation Mahakama Ione nini Kitaifuata.. Upande wa Utetezi wakasema baada ya Violation Wa naomba atamkwe Hafai na Ushahidi Wake ufutwe.
Kuhusu Kumtoa Shahidi asiendelee Kuwa Shahidi Sheria Inasema Ni Shahidi ambaye hana Uwezo Wa Kujibu Maswali na Kwamba iwe imesababishwa na Umri Mkubwa au Mdogo.. Upande wa Utetezi weomba itumike hiyo ya Mwisho ya Any other Similar Cause.
Jaji: Mahakama imeombwa Kurejea Kwenye andiko. Ambalo Mr Kibatala alilirejea Hapa Mahakamani Akiwa ameichukua Kutoka North Carolina, Kwamba Moja ya a Jambo kwao ni Pale Shahidi ana Kosa Sifa ni Kwa Shahidi Kukosa Kuona Umuhumimu wa a kutoa Ushahidi wale.
Kwa sababu hiyo Sheria hiyo kwetu Tanzania hakuna, Mtobesya ameomba Mahakama ifanye kazi ya Bunge. Mahakama haiwezi Kuongezea Jambo hilo pamoja na Kuomba Mahakama inaweza Kuongezea Sheria hiyo.
Pale ambapo Inaona kwamba Kuna Ulazima wa Kufanya Jambo hilo, Hasa Ikiwa imethibishwa Kwamba Kweli limetokea.. Suala la Kwamba Shahidi hajaona Umuhimu Wa Kuzungumza Ukweli Kwa kuwa hakuna Sehemu imeelezwa Kwamba Shahidi hajui Umuhimu Wa Kuzungumza Ukweli.
Jaji: Kinachoonekana Ni kwamba Shahidi Kwa Kuonekana na Jambo hilo Mahakamani ni suala La Kutoaminika Ushahidi Wake.. Mahakama hii sasa Inashindwa Kumuodoa Shahidi Huyu.. Nafahamu katika PGO ya 292 (5&6) eeleza Sifa ya Notebook na Kwamba Details za namna gani.
Kwamba inatakiwa Kuwa na Taarifa za Utendaji kazi, Hapo Ndipo nakubalina na Suala la Utetezi kwamba Upo Umuhimu wa kukagua Notebook hiyo, Lakini Mr Chavula alisema Kw a siyo wote ambao wameruhusiwa kukagua Notebook hiyo.. Kwa PGO 282 (7)C kwamba Ndiyo Kuna watu waliotajwa Kuhusu.
Kukagua Notebook hiyo, Lakini kwa Jambo hilo Mahakama ina maamuzi Kwamba Nyaraka Yoyote inayojitokeza Kwenye Mwenendo Wa kesi Mahakamani basi Itakuwa ni Nyaraka ama Kielelezo Cha Mahakama. Na Kwa Sababu Notebook hiyo ilikutwa Kwenye Kizimba cha Mahakama hii basi Upande Wa Utetezi.
Jaji: Lakini Mahakama Ina maoni Kwamba Kuhusu Taarifa za Siri zilizokuwa katika Notebook hiyo zinaweza kuangukia katika Mikono ya watu Wasio husika, Kwa Namna hiyo basi Kwa sababu Jambo hilo linahusu Haki za Watu Mahakama inaweka Utaratibu Wa Wakili Mmoja Mmoja ataruhisiwa.
Kukagua na Kwa sehemu husika tu.. Na Wakili hatoruhusiwa Kupiga Picha Sehemu ya Notebook hiyo. Hiyo ndiyo Maana ya Kauli yangu kwamba HAKI ISITENDWE TUH BALI IONEKANE IKITENDWA.. Na huo ndiyo uamuzi wangu..
- Mawakili wa pande zote mbili Wanasimama Kukubaliana na Uamuzi wa Jaji
Jaji: Sasa Kuhusu Utaratibu wa Nani ataruhisiwa Kukagua, Mtachaguana Mmoja Mmoja.. Na Kwamba Notebook hii ilikuwa Chini ya Mikono ya Mahakama, basi nawakabidhi hapa. Je, Mniambie Maoni yenu Mkafanyie zoezi hili katika Usiri (Privacy) au hata hapahapa.. Nahitaji Maoni yenu..
- Mawakili wa pande zote mbili Wanashauriana
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Kama Ukiridhia naomba Uhairishe Shauri kwa Muda kwa Sababu hatuwezi Kujua Ukaguzi Utachukua Muda gani.
Atalazimika kuchukua hatua hata kama hapendi.Kama ni kweli, Mama afanye namna mapema kuepusha hii kadhia.
Shukurani kwa Proffesa J kwa kumuona huyo shahidi maandazi na kuwatonya mawakili wa utetezi
Yes, Kibatala ndio alisema hivyo.Kumbe profesa J ndo aliyeona hicho kitu at first place?
Daaaah ! kesi za kutengenezwa madhara yake mnaumbuka kirahisi sana aiseeeYes, Kibatala ndio alisema hivyo.
Ingekuwa ni hivyo, yote haya yangetoka wapi?Kwani kikawaida shahidi haandaliwi maswali na majibu na wakili wake?
Mawakili wa utetezi wamekubali kuikagua hiyo diary ama wamegoma
Ana deserve hilo jina la prof J kuliko yule profesa wetu aliyeokotwa Jalalani.
Unadhani simbachawene alikosea kusema wao hua wanataka police wenye ufaulu wa div 4?Hayo ndio matunda yake.Daaaah ! kesi za kutengenezwa madhara yake mnaumbuka kirahisi sana aiseee
Huyo shahidi kafanya makusudi kuingia na diary bila kuiarifu mahakama.Ingekuwa ni hivyo, yote haya yangetoka wapi?
Mtaongea lugha zote safari hii.Huyo shahidi kafanya makusudi kuingia na diary bila kuiarifu mahakama.
Atakuwa mkibosho huyo!
Proffessor J hoyeeeehhhhhShukurani kwa Proffesa J kwa kumuona huyo shahidi maandazi na kuwatonya mawakili wa utetezi