Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe - Novemba 18, 2021. Kesi imeahirishwa hadi Novemba 22, 2021

Haki itendeke na ionekane ikitendeka.Najaribu kuwaza endapo na Lissu angekuwa hapo na akina Kibatala.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Cremia, Iboya, comte, nyie nyote ni sehemu ya timu bambikizi, pengine miongoni mwa wapiga chabo 24.
Siasi zilivyo za ajabu unawezakuta hawa ni Watu wa karibu sana na Mbowe au ukute ni MDEE na MNYIKA. Ukiangalia jinsi Iboya anavyochangia mijadala muda wote inawezekana akawa ni LEMA anam SNITCH jamaa
 
Yaani haviishi! Matokeo yake, jamaa wanasota ndani bila sababu ya msingi. Wangekuwa WAMEDHAMINIKA, ingekuwa nafuu!

Sijui aliyebuni issue hii anajisikiaje, anapoona wenzie wanateseka kwa UBUNIFU wake!
Bebe nang'we nkoi, iiiiiihh...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
mambo yanazidi kuwa magumu kwenye kesi hii - tutashuhudia mengi.
FUSO, lakini mimi naona Jamhuri kwa ushirikiano na jaji ndio wanayafanya mambo yazidi kuwa magumu. Bahati mbaya yanakuwa magumu kwa upande wao wenyewe. Wanajichanganya sana. Pingamizi likiwekwa leo kesho uamuzi unasema halina mashiko siku ya tatu kitu hicho hicho upande wa utetezi wakikitumia Jaji na Jamhuri wanasema wanakikataa. Kwahiyo wanabaki kujichanganya tu hadi jaji anashindwa kutoa ruling kwa kitu chepesi kama kukutwa na nyaraka ambayo utaratibu haujafuatwa kupanda nacho kizimbani.
 
Dogo, hata Kama una shida na hiyo buku Saba basi jitahidi kuficha upumbavu wako kwenye mvungu wa mwili wako! Unajichoresha mno kwenye haya mambo ya mahakama na ni Bora usome TU na kupita kwani hutachekwa!
Hii kesi ni darasa tosha lenye majibu ya mtihani na watahiniwa wakapepea na A+ hasa wale wa masters ya llb hivyo usiwavuruge wenye kusoma nondo za mawakili wasomi! Hata huyo jaji wa Sasa ameingizwa darasani na anazinyatia nondo za kina Mtobesya na Kibatala! Wewe pita kuleeeee!!!!!!!!!!
 
Wameshasoma mchezo ushahidi wote ukipokelewa dikiteta hachomoki,dawa ni kuweka pingamizi ushahidi ukipokelewa.

Kwa mapingamizi haya kesi inaweza chukua mwaka mzima.
Hujui lolote ungekaa kimya unhesaidia kuficha ujinga wako. Kupinga kupolelewa Kwa vielelezo feki ni wajibu wa Utetezi. Kwa ukosefu wa akili ulionao unajiona umetoa point ya maana?
 
Shemeji yake ni diwani wa CCM, Kwa hiyo anatetea maslahi ya Dada yake wala hajui lolote.
 
Una kisu kama kielelezo kwenye kesi ya mauaji, unaleta Shahidi wa Kwanza ku tender kielelezo hicho upande wa Utetezi unapinga upatikanaji wake Hadi kufikia kuletwa mahakamani. Unaleta Shahidi wa pili unamtaka Ku tender kielelezo kilekile ambacho Mahakama awali ilisema hakikufika mahakamani kihalali, hiyo ndo hoja ya Utetezi. Ni mtego Kwa Mahakama maana wakiruhusu wataonekana lile pingamizi la juzi walilipokea wakijua mbele wataruhusu Shahidi mwingine kuingiza kielelezo hichohicho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…