Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe 26 Jan 2022. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi wake

Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe 26 Jan 2022. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi wake

Anachoongea Urio hakiwezekani. Kwanza ni immoral and unethical. Huwezi kutoa taarifa polisi kuhusu uhalifu na kisha ukawaingiza marafiki zako huku ukijua watapata matatizo makubwa.

Binadamu hufanya hayo pale tu interests zake zinapokuwa hatarini na sio kwenye mazingira mengine.

Kesi kama hii Ingelikuwa kweli. Polisi wangempa Urio watu wa kuwaunganisha na Mbowe. Most likely hao watu wangelikuwa ni wanajeshi bado Lakini wangejifanya waliacha jeshi.

Kilichotokea hapa ni mawili.
1. Hii ni kesi ya kutunga na Urio anaongea uongo.

2. Ni kesi ya ukweli na Urio alikuwemo kwenye ugaidi na hakutoa taarifa polisi mpaka baada ya kuona mpango umegundulika.

Kwa Mimi Nafikiri namba moja ndio sahihi.
 
Denis Denis Denis!!!!!
a) Huruhusiwi hata kuwasiliana na chombo kingine chochote kilicho nje ya mamlaka yako! Taarifa ya uhalifu ulipaswa kuitoa kwa mkuu wako wa kazi na kwa cheo lazima angekuwa kapteni. Sio rahisi kutaka kuonana na DCI na ukapewa access uliyopewa. Wewe ni sehemu ya watesaji. Hukuweza kuripoti kituo cha Polisi huko ulikokuwa mpaka ukaenda Dar kwa DCI?

b) Ulipaswa kuzuia hata recruitment ya hawa makomandoo!! Hasa wakiwa ni watu mliofanya kazi nao pamoja na ukiwadanganya kuajiriwa kazi za ulinzi. Uliwatoa kwenye kazi zao halali ukawaingiza kwenye shida ya uongo!

c) Kingai na task force sasa ndio halisi like kundi la wasiojulikana. Na wewe ni mmoja wao.

Damu ya former colleagues itakulilia!!
 
Halafu kaka yake Mbowe alikuwa na cheo kikubwa sana jeshini. Aache kumtumia kaka yake awatumie watu asio wajua?? Nonsense
Sasa Nonsense ni nani hapa- uombe mbowe asitoke akitoka utapata tabu sana yaani unamwambia NONSENSE
 
Shida NI kwamba he mbowe alimwambia kweli hayo maneno kamanda?
huyo kamanda anampeleka jela mbowe.anaonekana yeye ndio MKUDA
Kingai alichemka... Urio alisema kuwa 500K alipokea ili jamaa wakafanye uhalifu...
Je, kuna sehemu mashahidi waashtaka kuanzia Kingai wameonesha ualifu uliofanywa na watuhumiwa??
Urio keshaimaliza nguvu hii kesi.
Amekuwa mkweli sana!

Kama watamfunga FAM, watafanya hivyo ila si kwa ushahidi unaotolewa kwenye kesi hii...!!
Laki tano, Urio kasema ilikuwa "nauli"...!
 
Kingai alichemka... Urio alisema kuwa 500K alipokea ili jamaa wakafanye uhalifu...
Je, kuna sehemu mashahidi waashtaka kuanzia Kingai wameonesha ualifu uliofanywa na watuhumiwa??
...
Kwani mipango aliyoitiwa kule Mikocheni ilikuwa ya shughuli gani?
 
Anachoongea Urio hakiwezekani. Kwanza ni immoral and unethical. Huwezi kutoa taarifa polisi kuhusu uhalifu na kisha ukawaingiza marafiki zako huku ukijua watapata matatizo makubwa...
Wakili wa Serikali: Baada ya Kusema Wapo tayari?

Shahidi: Laki Moja na tisini na Tisa Iliyobakia, nilimwambia Mtafanya kazi Iliyowapeleka, Lakini mkiona chochote ambacho cha uhalifu mtaniambia, Mohammed Ling'wenya Kwa Maneno yake aliniambia ASKARI HAWEZI KUWA RAIA ILA RAIA ANAWEZA KUWA ASKARI. Nikawaambia Chochote Kitakachotokea Wataniambia, Baada ya Hapo, Nilimpigia Freeman Mbowe akanitumia Laki Moja na Tisini na Tano, Kwa ajili ya nauli yao Kutoka Morogoro Kwenda Dar es Salaam..
 
Shahidi: Kwamba Samahani Tulikuwa Tumepitiwa. Kazi Uliyotuambia temekuja Kufanya Ya Ulinzi Kwa Freeman Mbowe imebadirika siyo hiyo, Kwamba Freeman Aikael Mbowe ametushawishi Kufanya kazi Nyingine.. Ambayo hivi sasa tunavyoongea, Wale Madogo (Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya) Wapo Moshi sasa hivi na Lijenje Wapo Moshi Wamepewa kazi ya kumshambulia Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya.. Na kabla ya Tarehe 07 August 2020 Wanatakiwa Wawe Wameshamaliza kazi hiyo na Kurudi Dar es Salaam.
Kwenye report ya uchunguzi wa simu haya maongezi hayakuonekana.....nini Jamhuri mnafanya jamani mwatutia aibu sie wengine huku khaa, mnajikanganya hadi aibu
 
Shida NI kwamba he mbowe alimwambia kweli hayo maneno kamanda?
huyo kamanda anampeleka jela mbowe.anaonekana yeye ndio MKUDA
Hata hawa watatu alionao hapo na wako wote mahabusu
soma hapa
Wakili wa Serikali: Baada ya Kusema Wapo tayari?

Shahidi: Laki Moja na tisini na Tisa Iliyobakia, nilimwambia Mtafanya kazi Iliyowapeleka, Lakini mkiona chochote ambacho cha uhalifu mtaniambia, Mohammed Ling'wenya Kwa Maneno yake aliniambia ASKARI HAWEZI KUWA RAIA ILA RAIA ANAWEZA KUWA ASKARI. Nikawaambia Chochote Kitakachotokea Wataniambia, Baada ya Hapo, Nilimpigia Freeman Mbowe akanitumia Laki Moja na Tisini na Tano, Kwa ajili ya nauli yao Kutoka Morogoro Kwenda Dar es Salaam..
 
Yaani kwa maoni yangu, akina Adamoo na wenzake waachiwe leo hii hii maana shahidi kishathibitisha kuwa aliwaset up .... !!

Mwanzoni kesi ilipoanza nilikuwa na wasiwasi na hao watu kwa kuwa ni wanajeshi. Nilifikiri walitumika kumchomekea Mbowe. Nilishangaa akina Mbowe kuwaunganisha kwenye utetezi wake...
Naungana na wewe kumtaka DCI ajiuzulu. Haiwezekani suala la kuhatarisha Usalama wa nchi liachwe mikononi mwa Askari mmoja tena Asiyeweza hata kujeshimu wakubwa zake jeshini.

Yaani Mwalimu wa darasa apate Taarifa mwanafunzi wa kike darasani kwake ana mimba, aache kumwambia Kwanza Mwalimu Mkuu aende akamwambie Bwanashamba?

Afisa wa JW unapata Taarifa ya kuteteresha Usalama wa nchi unakimbilia Polisi Dar bila hata kumuaga mkubwa wako wa kazi?
 
Mimi tangu kesi inaanza mwanzo kipindi mbowe anakamatwa.nilisema kosa alilofanya mbowe NI kushirikiana na hao wanajeshi wengi hawakunielewa.

Sasa wanajionea wenyewe.

Kama alikuwa anataka ulinzi alitakiwa atafute kampuni za ulinzi sio hao.

Hao Wana viapo vya UTII.

Ila watu walinibishia humu.

Hata hawa watatu alionao hapo na wako wote mahabusu
soma hapa
Wakili wa Serikali: Baada ya Kusema Wapo tayari?

Shahidi: Laki Moja na tisini na Tisa Iliyobakia, nilimwambia Mtafanya kazi Iliyowapeleka, Lakini mkiona chochote ambacho cha uhalifu mtaniambia...
 
Back
Top Bottom