Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe 26 Jan 2022. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi wake

Huu upuuzi kila shahidi anayekuja anauzungumzia halafu hakuna evidence yoyote.

"Watu wa kukata miti pembezoni mwa barabara ya Mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Arusha, Mwanza, Kilimanjaro hasa Mji wa Moshi na Barabara Kuu ya Morogoro - Iringa,kuchoma vituo vya mafuta mijini na masokoni na kwenye mikusanyiko ya watu na kudhuru viongozi wa serikali."

Watu wa kufanya Hii kazi mbona ni zaidi 1,000 huyu afisa ndio aitwe na Mbowe kufanikisha hawa watu?halafu mbona kazi yenyewe haihitaji makomandoo sasa?kukata miti?Hii kazi mbona hata Red Brigade wangeweza kama kweli ndio ilikuwa lengo.

Hapa anasema hakuambiwa hata idadi,mtu aliyepanga kufanya nchi isitawalike hajui anahitaji wanajeshi wangapi?

Wakili wa Serikali: Sasa Shahidi Tuambie, yeye alikwambia anataka Wangapi

Shahidi: Hakuna Kikomo cha Watu, Ni wale Watakaopatikana.

Nasubiri maswali ya Kibatala aisee
 
tulia babu, tukutane kwenye Mbege pale Rau madukani kwa mama P. Leo nasikia kachuja kali balaa.
Naomba na mimi niwepo tafadhali! Na huyu Mzee mwenzangu (Mzee Mgaya) johnthebaptist ! Huwa na yeye anaipenda sana mbege ya Rau Madukani.
 
Mbowe- urio- adamo+wenzake
urio- dci- kingai+ wenzake
airtel, tigo
forensic
Kaaya- sabbaya- mbowe-sabaya
huoni huo muunganiko
 
evidence ni nini?
 
Yaani huu ushahidi wa kitoto haswa. Mtu hamja juana tabia akurupuke tuu kukuambia natka kufnya nchi isitawalike.. This is bulls sheet.
Hivi hizo gharama za hii kesi ya mchongo hizo pesa si wapewe yatima?? Na rais ana angalia tuu huu urojo kweli??
 
Eti Shahidi baada ya kuambiwa hizo taarifa "akashindwa kulimeza" 😬😬😬 hivyo akampigia simu DCI Boaz majira ya saa tatu usiku! 😁😁😁

Wakili wake anamuuliza kuhusu hiyo namba ya DCI kama anaikumbuka, eti anasema sijaikariri kichwani! 😁😁😁 Inawezekana kweli? Hata aina tu ya mtandao wake, kama ni ya voda/airtel/ tigo, nk!!!

Halafu hajasema hiyo namba aliipata wapi!! Ni aibu na fedheha kubwa sana kuwa na aina hii ya wanajeshi!
 
Airtel log ipo na Mh. Kibatala keshaipata inaonyesha Mbowe alimpigia
 
Airtel log ipo na Mh. Kibatala keshaipata inaonyesha Mbowe alimpigia
Mimi namuongelea Shahidi! Baada ya kushindwa kulimeza, na kuamua kumpigia simu DCI majira ya saa tatu usiku, namba yake aliipata wapi?

Na ilikuwaje ameshindwa kuikariri mahakamani kama zile namba alizo pigiwa na watu wa Mbowe?
 
Mbowe- urio- adamo+wenzake
urio- dci- kingai+ wenzake
airtel, tigo
forensic
Kaaya- sabbaya- mbowe-sabaya
huoni huo muunganiko
Muanganiko unaoleta wazo moja la kuonesha nia ya kula njama ya ugaidi haipo.

Mashahidi wa mwanzo wote ukiacha huyu Urio walionesha wazo la namna walivyo wakamata watuhumiwa hakuna mahali wamethibitisha kuwakuta wakiwa ktk harakati zozote ama za mipango, fikra, au vitendo vinavyoashiria ugaidi.

Huyu Urio hadi sasa yeye tu ndiye ameonesha kuelekea kwenye msingi wa kesi, hata hivyo katika maelezo yake hadi sasa hayajapata "support" yenye nguvu ya uthibitisho wa kile anachohadithia kwa maana nyingine hii yaweza kuwa kama "story" za kutungwa labda tusubiri wengine.
 
Upande wa utetezi huyu watamgonga mpaka ijumaa!Yaani Leo ni zamu ya mashtaka tu!Kesho ajiandae vizuri asijepatwa na kiharusi!
 
Hivi hizi hotel kwanini hazinaga CCTV, nafikiri ingetungwa sheria ya kuwalazimisha wafunge cctv.
 
Kwa mjibu wa sheria ya kuzuia na kupambana na ugaidi ya 2002- nia tu inatosha kuweka hatiani kwa ugaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…