Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe 26 Jan 2022. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi wake

Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe 26 Jan 2022. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi wake

Hauwezi kumtafuta mwanajeshi awe mlinzi wako hata Kama amefukuzwa jeshini.
huo ndo ukweli na ndio utakaomfunga mbowe.ameshirikiana na watu SIO.
Kwa hiyo askari akifukuzwa kazi hawezi ajiliwa hata na private sector? ni wapi sheria inakataza? kwamba hao wanajeshi watamgeuka na kusema alitaka kufanya ugaidi? na kama wakitaka kumgeuka una uhakika wanaweza kutetea hoja yao mbele ya sheria? Uongo ni uongo tu haijalishi unasemwa na nani mwisho wa siku ni aibu
 
Hauwezi kumtafuta mwanajeshi awe mlinzi wako hata Kama amefukuzwa jeshini.
huo ndo ukweli na ndio utakaomfunga mbowe.ameshirikiana na watu SIO.
Kwa hiyo hata hayo Makampuni ya Yappi Markez, na mengineyo yaliyo waajiri hao makomandoo hapo kabla, nayo yanatakiwa kushtakiwa kwa ugaidi na uhujumu uchumi baada ya kuwaajiri hao makomandoo!

Au ni Mbowe tu ndiyo haruhusiwi? Halafu kuna sheria yoyote inayo mlazimisha mtu kuajiri walinzi wa Kampuni binafsi? Mimi ninacho fahamu huo utaratibu wa kupangiana maisha kwenye nchi yetu, haupo!

Hivyo jitahidi usijitoe ufahamu. Think critically, ok?
 
Mimi tangu kesi inaanza mwanzo kipindi mbowe anakamatwa.nilisema kosa alilofanya mbowe NI kushirikiana na hao wanajeshi wengi hawakunielewa.

Sasa wanajionea wenyewe...

Hili hitimisho lako ndio matamanio yako toka mwanzo, ni kosa kuwa na walinzi wanajeshi? Mbona hata huko kwenye makampuni binafsi ya ulinzi kuna wanajeshi wengi tu waliostaafu nk? Je angekutana nao huko kwenye makampuni binafsi ya ulinzi kama alikuwa na nia ovu asingewatumia?
 
Yaani nikwambie tu Mimi Sheria nimeisoma siyo kwamba natokea jalalani. Awali nilijua Urio atakuwa na Jambo la maana, lakini tangu Goodluck atoe ushahidi wa majumuisho nilifuta uwezekano huo.

Urio ni miongoni mwa Wasiojulikana ndo maana ofisi ya DCI ni kama kwake. Ndo maana anaweza kutoka kazini bila kuaga akaenda kwa DCI. Ndo maana anapata Taarifa eti ya kupanga kulipua nchi anamjulisha DCI badala ya kuanza na mkubwa wake kazini.

Ninachomwonea huruma ni jinsi atakavyoteseka baada ya ushahidi wa uongo kwamba aliwategea Bomu vijana aliowafundisha ili wakaangamie. Kwenye ukamataji wa uhalifu kuna mengi Ikiwemo kuuawa kama alivyofanyiwa Lijenje.

Unawezaje kuwasakizia kifo watoto wa wenzio? Kwa nini Mbowe asingekamatwa Kwa "Nia yake" ya kulipua nchi bila kuhusisha roho za wasio na hatia kina Lijenje na Kusekwa?

Unaweza kuchekelea Sasa, lakini chukulia ni Mtoto wako Yuko mahabusu halafu linajitokeza jinga moja linasema Mimi ndo nilipewa kazi ya kutafuta wahalifu nikawasakizia hao akiwemo Mtoto wako!!

I truly symphathize with your feelings. Lakini, kwani hukumsikia Luteni Urio akisema kwamba FM alikuwa amezimu kufanya VYOVYOTE VILE ilimradi tu achukue dola?
 
You're so funny, unajua! Unakubali ushahidi wa Luteni Urio kwamba ni kweli Mbowe alimwomba amtafutie bodyguards, at the same time unakataa sehemu iliyosalia ya ushahidi wake kwamba alikuwa anafanya plans za kuzua taharuki na vurugu kwenye nchi?
What is funny you dimwit Mbowe kukubali kwamba bodyguards aliokuwa anawatafuta ni kwa ajili ya ulinzi wake tu na na sio kufanya ugaidi ? Ni kazi ya Kingai na watu wake kuthibitisha kwa vielelezo vinginevyo na mpaka sasa hawajathibitisha hivyo kwa njia yoyote zaidi ya maneno matupu.
 
Kama Ni kweli Mbowe aliwasiliana na Urio basi atakuwa alijitakia mwenyewe. Kwanini uwasiliane na mtu wa jeshini wakati unawindwa Kila wakati upatikane na kosa. Kama Ni kweli lakini.
 
Huyu shahidi huenda ana aiba ya mwendawazimu wa namna fulani.

Kwenye mtego wa rushwa, tangu lini wanawakamata wasiohusika?

Hata kama tukaamua kujivika ujinga kwa muda, tujifanye hatuna akili, tuamini kuwa Mbowe alitaka kufanya uhalifu, makomandoo hawakuwa kwenye mtandao wa kufanya uovu, imekuwaje wakaingizwa moja kwa moja kwenye uovu wakati Urio alitaka kuwatumia tu kuupata mtandao wa uovu wa Mbowe?

Kama hawa makomandoo walitumika katika kuupata mtandao wa uovu wa Mbowe, mbona hawajatajwa hao waliokuwepo kwenye mtandao wa uovu wa Mbowe?
Very good reasoning!
 
Mawakili wa utetezi waende mitandao husika waulize gharama ya kutoa Tsh 500,000/ ilikuwa sh ngapi wakati huo,,maana haiwezekani 500,000 itolewe kwa makato ya buku
 
Yaaani ukisikiliza yanayoendekea mahakamani kuhusu kile kinachoitwa ugaidi unajionea aibu kuwa mtanzania. Hata mzungu aliye asisi sheria ya ugaidi na tafsiri ya ugaidi anajuta kushirikisha baadhi ya watawala wa nchi za kiafrika. Kwa kujaribu kuutumia ugaidi kwa manufaa ya kubaki madarakani wamefanya ugaidi uwe jinai ya kituko isiyo na maslahi wala maana yeyote kwa raia wa nchi zao
 
What is funny you dimwit Mbowe kukubali kwamba bodyguards aliokuwa anawatafuta ni kwa ajili ya ulinzi wake tu na na sio kufanya ugaidi ? Ni kazi ya Kingai na watu wake kuthibitisha kwa vielelezo vinginevyo na mpaka sasa hawajathibitisha hivyo kwa njia yoyote zaidi ya maneno matupu.
Hilo la ulinzi amelisema Luteni Urio. Halafu hakuishia hapo. Amesema pia kwamba harakati ilikuwa UGAIDI. Umemsikia? Sasa kama unakubali hilo la kuwa walinzi binafsi (bodyguards), kubali pia na hili la pili la terrorism.

Otherwise, reject the whole thing. Hapo nitakuona shujaa & muungwana sana!
 
Kwa mjibu wa sheria ya kuzuia na kupambana na ugaidi ya 2002- nia tu inatosha kuweka hatiani kwa ugaidi
Mpaka sasa hiyo ni ya ugaidi ya Mbowe haijathibitishwa kwa kielelezo chochote zaidi ya maneno ya mdomoni tu.
 
Wakili wa Serikali: Tuambie Sasa Umepeleka Watu wawili, Nini Kikafuata.

Shahidi: Freeman Mbowe akaniambia Bado, Ongeza wengine Wawili

Wakili wa Serikali: Baada ya kukueleza hivyo wewe Ulifanyaje

Shahidi: Nikaanza Kuwatafuta Watu wawili

Kwahio hawa watu wanne ndio walitegemewa kuleta taharuki nchi nzima?
 
Mawakili wa utetezi waende mitandao husika waulize gharama ya kutoa Tsh 500,000/ ilikuwa sh ngapi wakati huo,,maana haiwezekani 500,000 itolewe kwa makato ya buku
Hii haiwezekani,kabda kama wakala alikuwa hawara wa Urio
 
Mawakili wa utetezi waende mitandao husika waulize gharama ya kutoa Tsh 500,000/ ilikuwa sh ngapi wakati huo,,maana haiwezekani 500,000 itolewe kwa makato ya buku
Hii haiwezekani,kabda kama wakala alikuwa hawara wa Urio
Basi hii kesi Mbowe ashashinda shahidi muongo hata kama alikuwa na mahusiano na Mbowe
 
Back
Top Bottom