Hatimaye adhabu aliyopewa Tundu Lissu imemalizika Jana.
Mgombea huyo anayeungwa mkono na mamilioni ya Watanzania leo ataendelea na Kampeni yake katika mikoa ya Dodoma katika maeneo ya Chamwino na Singida katika maeneo ya Ikungi na Manyoni.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekuwa ni kichekesho Cha Dunia kutokana na upendeleo wa waziwazi kuibeba CCM na kuikandamiza Chadema.
Tume hiyo imekataa hata kupokea malalamiko ya Chadema dhidi ya Mgombea wa CCM kwa kukiuka Maadili ya Uchaguzi.
Lissu anatarajiwa kupata mapokezi ya kishindo kutokana na hamu kubwa ya wananchi kutaka kumsikiliza baada ya kudhulumiwa haki yake ya kufanya kampeni kwa siku 7 ili kulinda CCM.
-------- ------- -------
Yanayojiri muda huu saa 5 asubuhi.
Wananchi ktk jimbo la Bahi kata ya Bahi mkoa wa Dodoma baada ya kusikia mhe Rais Tundu Lissu atapita maeneo hayo kuelekea Singinda wameamua kumsubiri barabarani tangia saa moja asubuhi ili angalau waone sura yake tu
Jimbo hili tume ya CCM ilimuengua mgombea UBUNGE wetu kwa SABABU za kijinga kabisa!!
=====
Mkutano mdogo wakampeni wa mheshimiwa Tundu Lissu kwenye viwanja vya Bahi, Jimbo la wilayani Bahi - Dodoma baada ya kusimamishwa na wananchi barabarani wakati akipita kuelekea Manyoni na Ikungi
Mheshimiwa Tundu Lissu ameongea kwa mara ya kwanza na wananchi wa Bahi baada ya Kifungo cha Siku Saba..
Mheshimiwaa Tundu Lissu akiwa Bahi amesema haya.
1. Bahi kukosa mgombea Ubunge kwa sababu za tume, tume imeengua Mgombea wetu ili CCM ipite bila kupitwa. (2015 ni mgombea mmoja tu alioenguliwa lakini 2020 wagombea wa Chadema ni 63 wa ubunge.) Kuengua watu imekuwa njama ya CCM kwenye uchaguzi mkuu huu.
2. Kukosekana kwa uhuru wakuongea, kuhoji mambo yakimaendeleo kwenye nchi hii. Sasa Chadema itakapochukua nchi lazima irudishe uhuru wa wananchi.
3. Jimbo la Bahi watu wengi ni wafugaji ila kuna msululu wa kodi amabazo hazisaidii wafugaji Sasa tarehe 28 mkapige kura kukataa hizi kodi.
4. Uchaguzi mkuu huu mkapige kura kukataa wizi wa vitambulisho vya ujasiriamali. Léo wanasema vitambulisho unaweza pata mkopo sasa Kitambulisho hakina jina wala picha utapata mkopo wanani.
5. Uchaguzi mkuu huu ni muhimu kwenu watu wa Bahi, sasa mkapige kura kuamua hatima yenu, Bahi mkapige kura kuamua kukataa utapeli na udhalimu unaofanywa na MaCCM.
6. Wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye kupiga kura kumchagua madiwani wote waliopitishwa na mpige kura nyingi za Uraisi mpaka washindwe kuiba. Ilituweke mambo yetu sawa.
Ahsanteni Bahi. Tutarudi tena hapa Tarehe 17 tunamkutano mkubwa hapa.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Mhe. Tundu Lissu akizungumza na wananchi wa Bahi waliosimama barabarani kuzuia msafara wake uliokuwa njiani kuelekea Manyoni kuendelea na mikutano ya kampeni, ikiwa ni siku ya kwanza baada ya zuio la kampeni zake kwa muda wa siku 7.
Saa 9 Alasiri.
Lissu amewasili Ikungi na kulakiwa na mafuriko ya watu hasa wazee wanawake na vijana.
Mhe. Tundu Lissu asimamishwa na wananchi kijiji cha Kidabukanje kata ya Issuna, wilaya ya Ikungi.
Kinamama watandika kanga chini Mhe. Lissu apite.