Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wafuasi Wa chadema ni watu peace sana kwenye hizi picha hapo nimeona moja bango LA magufuli,nyingine nimeona bendera ya ccm,ingekuwa ni meko anapita hapo,usingekuta bendera ya chadema ccm wangeshusha zote.View attachment 1595493
Hatimaye adhabu aliyopewa Tundu Lissu imemalizika Jana.
Mgombea huyo anayeungwa mkono na mamilioni ya Watanzania leo ataendelea na Kampeni yake katika mikoa ya Dodoma katika maeneo ya Chamwino na Singida katika maeneo ya Ikungi na Manyoni.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekuwa ni kichekesho Cha Dunia kutokana na upendeleo wa waziwazi kuibeba CCM na kuikandamiza Chadema.
Tume hiyo imekataa hata kupokea malalamiko ya Chadema dhidi ya Mgombea wa CCM kwa kukiuka Maadili ya Uchaguzi.
Lissu anatarajiwa kupata mapokezi ya kishindo kutokana na hamu kubwa ya wananchi kutaka kumsikiliza baada ya kudhulumiwa haki yake ya kufanya kampeni kwa siku 7 ili kulinda CCM.
-------- ------- -------
Yanayojiri muda huu saa 5 asubuhi.
Wananchi ktk jimbo la Bahi kata ya Bahi mkoa wa Dodoma baada ya kusikia mhe Rais Tundu Lissu atapita maeneo hayo kuelekea Singinda wameamua kumsubiri barabarani tangia saa moja asubuhi ili angalau waone sura yake tu
Jimbo hili tume ya CCM ilimuengua mgombea UBUNGE wetu kwa SABABU za kijinga kabisa!!
=====
Mkutano mdogo wakampeni wa mheshimiwa Tundu Lissu kwenye viwanja vya Bahi, Jimbo la wilayani Bahi - Dodoma baada ya kusimamishwa na wananchi barabarani wakati akipita kuelekea Manyoni na Ikungi
Mheshimiwa Tundu Lissu ameongea kwa mara ya kwanza na wananchi wa Bahi baada ya Kifungo cha Siku Saba..
Mheshimiwaa Tundu Lissu akiwa Bahi amesema haya.
1. Bahi kukosa mgombea Ubunge kwa sababu za tume, tume imeengua Mgombea wetu ili CCM ipite bila kupitwa. (2015 ni mgombea mmoja tu alioenguliwa lakini 2020 wagombea wa Chadema ni 63 wa ubunge.) Kuengua watu imekuwa njama ya CCM kwenye uchaguzi mkuu huu.
2. Kukosekana kwa uhuru wakuongea, kuhoji mambo yakimaendeleo kwenye nchi hii. Sasa Chadema itakapochukua nchi lazima irudishe uhuru wa wananchi.
3. Jimbo la Bahi watu wengi ni wafugaji ila kuna msululu wa kodi amabazo hazisaidii wafugaji Sasa tarehe 28 mkapige kura kukataa hizi kodi.
4. Uchaguzi mkuu huu mkapige kura kukataa wizi wa vitambulisho vya ujasiriamali. Léo wanasema vitambulisho unaweza pata mkopo sasa Kitambulisho hakina jina wala picha utapata mkopo wanani.
5. Uchaguzi mkuu huu ni muhimu kwenu watu wa Bahi, sasa mkapige kura kuamua hatima yenu, Bahi mkapige kura kuamua kukataa utapeli na udhalimu unaofanywa na MaCCM.
6. Wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye kupiga kura kumchagua madiwani wote waliopitishwa na mpige kura nyingi za Uraisi mpaka washindwe kuiba. Ilituweke mambo yetu sawa.
Ahsanteni Bahi. Tutarudi tena hapa Tarehe 17 tunamkutano mkubwa hapa.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Mhe. Tundu Lissu akizungumza na wananchi wa Bahi waliosimama barabarani kuzuia msafara wake uliokuwa njiani kuelekea Manyoni kuendelea na mikutano ya kampeni, ikiwa ni siku ya kwanza baada ya zuio la kampeni zake kwa muda wa siku 7.
Saa 9 Alasiri.
Lissu amewasili Ikungi na kulakiwa na mafuriko ya watu hasa wazee wanawake na vijana.
Mhe. Tundu Lissu asimamishwa na wananchi kijiji cha Kidabukanje kata ya Issuna, wilaya ya Ikungi.
Kinamama watandika kanga chini Mhe. Lissu apite.
View attachment 1595619
View attachment 1595719
View attachment 1595720
View attachment 1595721
View attachment 1595722
View attachment 1595723
View attachment 1595724
View attachment 1595725
View attachment 1595726
View attachment 1595727
View attachment 1595728
Kwenye swala la kusomba na nyie bado mnaongea🤔? Zile fuso zenu huwa zinafanya kazi gani?wenzio wanalinganisha na Magufuli ambaye malori yanasomba watu kutoka Dodoma na Singida mjini kujaza uwanja
Anayesaliti nchi ni yule asiyetaka kushauriwa mkuu. Urais ni taasisi lazima ushauriwe.Aliyeisaliti Nchi Ndio anapata aibu
Anayesaliti nchi ni yule asiyetaka kushauriwa mkuu. Urais ni taasisi lazima ushauriwe.
Kiukweli ukoo wangu wote hauwezi kumpa kura huyu aliyeua private sector na kuwauliza uliza vijisenti vidogo tunavyowatumia kutoka ughaibuni ili wanunue chumvi tu. Hayo ni maisha ya kishamba, kijima na kitumwa.Msaliti wa Nchi Lissu atajuta huu mwaka
Yale Mabeberu aliyokuwa anayetetea bungeni kutuibia rasmali zetu kama sio Magufuli lissu angeuza Nchi
Kiukweli ukoo wangu wote hauwezi kumpa kura huyu aliyeua private sector na kuwauliza uliza vijisenti vidogo tunavyowatumia kutoka ughaibuni ili wanunue chumvi tu. Hayo ni maisha ya kishamba, kijima na kitumwa.
Sawa. Hata kuiba ni kazi piaWatanzania tuliowengi tutamchagua Rais Magufuli kipenzi cha Watanzania
Yule mropokaji na msaliti wa Nchi Lissu atapigiwa kura na robert tu
Sawa. Hata kuiba ni kazi pia
Mbona unauchungu namna hii? Kunywa maji kidogo utulize roho yako!Hivi wewe mleta mada unajua maana ya Live?
Wataleta mipicha yao ya kufoji jioni toeni hiyo live.
Vipi tukio LA kuhutubia viti pale Mkapa sijaona ukilizungumzia!Tundu anakamilisha ratiba
Kawadanganye wapumbaf wenzako huko Lumumba, watanzania sio wajinga kuwachota kwa propaganda za kijinga hivyo.Kwanza hawa washabiki wa Lissu wangejiuliza tangu tuingie mfumo wa vyama vingi 1992, hakuna mgombea yeyote wa upinzani aliyeletwa na wazungu na kusaidiwa waziwazi kama Lissu, kuna nini nyuma ya pazia!?
Amka ndugu acha kulala, kumekucha huku!Watanzania tuliowengi tutamchagua Rais Magufuli kipenzi cha Watanzania
Yule mropokaji na msaliti wa Nchi Lissu atapigiwa kura na robert tu
Wakili ameajiriwa kusimamia haki za Lissu, unateseka Mr Bozi Boziana?Jibu hoja msukule povu la nini, Robert Amstadarm anampigia kampeni Lissu ili apate nini??
Kwahiyo unataka kudhibitisha kwa wanaCHADEMA kuwa Tundu Lissu ni Hadhi ya Chini??Mimi ningeamini ungeleta taarifa ukiwa huna upande maana umeanza vema ila kumalizia rangi yako ikaonekana.
Hivi pale Mlimani city ulitaka watu wajazane kumfuata kama kariokoo umesahau yale ni maeneo yenye hadhi tofauti?
Dada maisha yetu mtaani jins yalivyo magumu ni heri ungekaa kimya tuu kuliko kutetea udharimu.Dodoma hana chake pale. Ataambulia aibu tu.