Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Katika Mapokezi ya Tundu Lissu Dodoma na Singida

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Katika Mapokezi ya Tundu Lissu Dodoma na Singida

Akina Crimea na bint Lowassa ni watoto wa waliokua wapinzani fake baada ya kutishwa na jiwe walirudi CCM Sasa hivi simu, Email na chat zao zote zinadukuliwa Ndio maana wanazungumza bila ridhaa ya nafsi zao kumridhisha jiwe lakini bado wanahali ngumu
Hawa watu wanaishi kinyonge Sana
Wanatia huruma wamekua watumwa ndani ya nchi yao wenyewe
 
View attachment 1595493
Hatimaye adhabu aliyopewa Tundu Lissu imemalizika Jana.

Mgombea huyo anayeungwa mkono na mamilioni ya Watanzania leo ataendelea na Kampeni yake katika mikoa ya Dodoma katika maeneo ya Chamwino na Singida katika maeneo ya Ikungi na Manyoni.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekuwa ni kichekesho Cha Dunia kutokana na upendeleo wa waziwazi kuibeba CCM na kuikandamiza Chadema.

Tume hiyo imekataa hata kupokea malalamiko ya Chadema dhidi ya Mgombea wa CCM kwa kukiuka Maadili ya Uchaguzi.

Lissu anatarajiwa kupata mapokezi ya kishindo kutokana na hamu kubwa ya wananchi kutaka kumsikiliza baada ya kudhulumiwa haki yake ya kufanya kampeni kwa siku 7 ili kulinda CCM.

-------- ------- -------

Yanayojiri muda huu saa 5 asubuhi.

Wananchi ktk jimbo la Bahi kata ya Bahi mkoa wa Dodoma baada ya kusikia mhe Rais Tundu Lissu atapita maeneo hayo kuelekea Singinda wameamua kumsubiri barabarani tangia saa moja asubuhi ili angalau waone sura yake tu

Jimbo hili tume ya CCM ilimuengua mgombea UBUNGE wetu kwa SABABU za kijinga kabisa!!

=====

Mkutano mdogo wakampeni wa mheshimiwa Tundu Lissu kwenye viwanja vya Bahi, Jimbo la wilayani Bahi - Dodoma baada ya kusimamishwa na wananchi barabarani wakati akipita kuelekea Manyoni na Ikungi

Mheshimiwa Tundu Lissu ameongea kwa mara ya kwanza na wananchi wa Bahi baada ya Kifungo cha Siku Saba..

Mheshimiwaa Tundu Lissu akiwa Bahi amesema haya.

1. Bahi kukosa mgombea Ubunge kwa sababu za tume, tume imeengua Mgombea wetu ili CCM ipite bila kupitwa. (2015 ni mgombea mmoja tu alioenguliwa lakini 2020 wagombea wa Chadema ni 63 wa ubunge.) Kuengua watu imekuwa njama ya CCM kwenye uchaguzi mkuu huu.

2. Kukosekana kwa uhuru wakuongea, kuhoji mambo yakimaendeleo kwenye nchi hii. Sasa Chadema itakapochukua nchi lazima irudishe uhuru wa wananchi.

3. Jimbo la Bahi watu wengi ni wafugaji ila kuna msululu wa kodi amabazo hazisaidii wafugaji Sasa tarehe 28 mkapige kura kukataa hizi kodi.

4. Uchaguzi mkuu huu mkapige kura kukataa wizi wa vitambulisho vya ujasiriamali. Léo wanasema vitambulisho unaweza pata mkopo sasa Kitambulisho hakina jina wala picha utapata mkopo wanani.

5. Uchaguzi mkuu huu ni muhimu kwenu watu wa Bahi, sasa mkapige kura kuamua hatima yenu, Bahi mkapige kura kuamua kukataa utapeli na udhalimu unaofanywa na MaCCM.

6. Wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye kupiga kura kumchagua madiwani wote waliopitishwa na mpige kura nyingi za Uraisi mpaka washindwe kuiba. Ilituweke mambo yetu sawa.

Ahsanteni Bahi. Tutarudi tena hapa Tarehe 17 tunamkutano mkubwa hapa.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Mhe. Tundu Lissu akizungumza na wananchi wa Bahi waliosimama barabarani kuzuia msafara wake uliokuwa njiani kuelekea Manyoni kuendelea na mikutano ya kampeni, ikiwa ni siku ya kwanza baada ya zuio la kampeni zake kwa muda wa siku 7.

Saa 9 Alasiri.
Lissu amewasili Ikungi na kulakiwa na mafuriko ya watu hasa wazee wanawake na vijana.

Mhe. Tundu Lissu asimamishwa na wananchi kijiji cha Kidabukanje kata ya Issuna, wilaya ya Ikungi.

Kinamama watandika kanga chini Mhe. Lissu apite.

View attachment 1595619
View attachment 1595719
View attachment 1595720
View attachment 1595721
View attachment 1595722
View attachment 1595723
View attachment 1595724
View attachment 1595725
View attachment 1595726
View attachment 1595727
View attachment 1595728
Wafuasi Wa chadema ni watu peace sana kwenye hizi picha hapo nimeona moja bango LA magufuli,nyingine nimeona bendera ya ccm,ingekuwa ni meko anapita hapo,usingekuta bendera ya chadema ccm wangeshusha zote.
 
Msaliti wa Nchi Lissu atajuta huu mwaka

Yale Mabeberu aliyokuwa anayetetea bungeni kutuibia rasmali zetu kama sio Magufuli lissu angeuza Nchi
Anayesaliti nchi ni yule asiyetaka kushauriwa mkuu. Urais ni taasisi lazima ushauriwe.
 
Msaliti wa Nchi Lissu atajuta huu mwaka

Yale Mabeberu aliyokuwa anayetetea bungeni kutuibia rasmali zetu kama sio Magufuli lissu angeuza Nchi
Kiukweli ukoo wangu wote hauwezi kumpa kura huyu aliyeua private sector na kuwauliza uliza vijisenti vidogo tunavyowatumia kutoka ughaibuni ili wanunue chumvi tu. Hayo ni maisha ya kishamba, kijima na kitumwa.
 
Watanzania tuliowengi tutamchagua Rais Magufuli kipenzi cha Watanzania

Yule mropokaji na msaliti wa Nchi Lissu atapigiwa kura na robert tu
Kiukweli ukoo wangu wote hauwezi kumpa kura huyu aliyeua private sector na kuwauliza uliza vijisenti vidogo tunavyowatumia kutoka ughaibuni ili wanunue chumvi tu. Hayo ni maisha ya kishamba, kijima na kitumwa.
 
Pole sana hatukujui wala hatuhitaji kutuma mtu wa aina yako.
Watz tuliochoka na ngonjera za madaraja na midege, tunaohitaji maendeleo ya WATU kwa kutumia kodi zetu , utatusikia na kutuona 28/10 kwenye sanduku la kura.
 
Kwanza hawa washabiki wa Lissu wangejiuliza tangu tuingie mfumo wa vyama vingi 1992, hakuna mgombea yeyote wa upinzani aliyeletwa na wazungu na kusaidiwa waziwazi kama Lissu, kuna nini nyuma ya pazia!?
Kawadanganye wapumbaf wenzako huko Lumumba, watanzania sio wajinga kuwachota kwa propaganda za kijinga hivyo.
 
Watanzania tuliowengi tutamchagua Rais Magufuli kipenzi cha Watanzania

Yule mropokaji na msaliti wa Nchi Lissu atapigiwa kura na robert tu
Amka ndugu acha kulala, kumekucha huku!

 
Amka ndugu acha kulala, kumekucha huku!

View attachment 1596570
20201010_155603.jpg
 
Mimi ningeamini ungeleta taarifa ukiwa huna upande maana umeanza vema ila kumalizia rangi yako ikaonekana.

Hivi pale Mlimani city ulitaka watu wajazane kumfuata kama kariokoo umesahau yale ni maeneo yenye hadhi tofauti?
Kwahiyo unataka kudhibitisha kwa wanaCHADEMA kuwa Tundu Lissu ni Hadhi ya Chini??

Sio, Diamond platnumz tu..Hata Zuchu tu akifika pale utakuta upepo umechange kila mtu anatamani apate nae mambo mawili,matatu.
 
Back
Top Bottom