Kwa katiba yetu hii, Mgombea Urais akitoka upande mmoja wa Muungano, lazima Mgombea Mwenza atoke upande mwingine. Kwa maana hii, Kama Membe atakuwa Rais, hawezi kumpendekeza Magufuli kuwa Mgombea Mwenza.
Membe ana kazi kubwa ya kufanya ili kuwashawishi wajumbe hasa ikichukuliwa Timu Lowassa watafanya linalowezekana ili asipate kura za kutosha.
Kama ulivyosema, Asha Migiro ana nafasi iliyo sawa na Magufuli kutokana na mazingira yalivyo.
Timu Lowassa pamoja na mbwembwe zote huku wakiwatisha wajumbe wa Kamati Kuu wamejikuta wako nje.
Nini hatima ya Lowassa katika siasa za CCM?
Hii ndiyo CCM ambayo ina wenyewe!
Kwa kweli, sasa naanza kupata picha kwa nini Membe alikuwa anaplay loser, kwa kuwanyenyekea kanda ya kusini,he was securing votes.he was guaranteed nomination. Sasa kumbuka nyuma ya Membe kuna Pinda na Mwandosya. kama kipita bila Makamba,kura za makamba most likely zitakwenda kwa Membe kama Makamba ataahidiwa FM,kura za kwao Kusini hatapata tabu sana kuzipata.
kabakiza Kaskazini,ambako nina hakika atapata kiduchu sana, na magharibi,ambako nina imani, all he needs to do is offer Wasira a position,he-he, mzee bado ataendelea kuwepo, then atapata some good numbers. Ingawa kikwazo bado kitakuwa magufuli.
Magufuli is shoe in for top 3. yani ukiitazama top 5 ukimtoa magufuli top 3, inabidi uwe na moyo wa chuma.