Mkuu,
Mimi siku ile anatangaza nia ya kuwa mgombea niliangalia/kusoma body language nikagundua kuna mtu/kikundi kiko nyuma ya Makongoro Nyerere.
Makongoro alikuwa ni proxy solder huku akitumia majukwaa ya kuomba udhamini kama uwanja wa kumwaga sumu ambayo viongozi wa juu wa CCM walishindwa kuimwaga.
Niliuliza maswali kwenye Thread hii,
Hata mdahalo maalum wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere lililofanyika juzi lilikuwa na malengo yale yale aliyokuwa akiyatafuta Makongoro.
Butiku, Warioba na Polepole walitumia muda mwingi kwenye mdahalo kumshambulia Lowassa na watu wake.
Hii ni video ya yaliyosemwa katika Mdahalo huo maalum
[video]https://youtu.be/d8SdnhJNOlM[/video]
Tumekuwa tunaambiwa Lowassa ana 'maamuzi magumu', tunayasubiri kwa sasa hayo maamuzi magumu!