Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Wakuu Mungu amesikia maombi yetu, UKAWA hiyooooo namuona Dr Silaa akipanga baraza la mawaziri Waziri Mkuu Mbatia, mwanasheria mkuu Tundu Lisu, Waziri wa ardhi Harima Mdee waziri mambo ya ndani Godbless Lema na....
 
Hilo hata mimi naliona. Huenda team Lowasa wakampigia debe Magufuri kwa hasira ya Membe kupitishwa. Mbali na hapo naona Magufuri anaweza kukukwama maana Membe naye ana watu NEC na mkutano mkuu.

Kama wafuasi wa lowasa wataamua kumsapoti magufuli ni dhahiri membe hana chake next presdaaa ni magufuli
 
Sijui mimi ni mnafiki. Sikuwahi kuwa shabiki wa EL lkn kwa tano bora hii mara laki moja EL. Wamaana hapo ni Magufuli tuu.
 
1.Members:.Huyu ni ndugu na kipenzi wa mwenyekiti na familia kwa ujumla, alishaandaliwa toka siku nyingi,ndo maana hata jana Rais alipoteua wasaidizi wake Ikulu ilikua lazima mtu ufikirie Mara mbili mbili na huyu ndiye mgombea atakayepeperusha bendera ya chama.
2.Magufuli:Huyu nae utendaji wake pekee ndiye uliempatia nafasi hakuna kiingine japo nae ni swahiba wa karibu wawenyekiti.Kwake kupenya kwenye vikao vya mbele ni ngumu sana Labda busara ya kawaida tu itumike.Anaweza kua PM japo kiuhalisia yeye ni bora kuliko wote walioteuliwa.
3.Asha Rose Migiro: Huyu kwanza jinsia ndiyo kigezo pekee japo nae alikwishaandaliwa toka siku nyingi lakini baadae upepo ukahamia kwa mebe. Kwake kupenya mbele inategemeana na kelele za wanawake wenzake mkutano mkuu.
4.Mama Amina: Huyu jinsia na Uzanzibar wake kama mwanamke ndivyo vilivyombeba, Kuna uwezekano mkubwa akawa makamu wa Rais maana naye kupenyeza kwake mbele ni kelele za wanawake wenzie huko mkutano mkuu.
5.January Makamba: Ikumbukwe kwamba huyu bwana baba yake aliwahi kua katibu mkuu wa chama, hiyo pia ni sababu kwahiyo kuna uwezekano kwamba hii ni fadhila na anaandaliwa kwa baadae kumrithi atakaekua Rais,Sidhani kama Janauary Makamba Anaweza kumkaribia Mwigulu nchema kiutendaji wa kazi.Anayo nafasi kubwa sana kupenyeza huko mbele maana wanaomuunga mkono ni wengi lakini atawekwa kando kama JK 1995 nasubiri baadae.

Ukweli na uhalisia ndo huo!
Uchambuzi mzuri ulichosahau kusema ni kuwa wote ni team Membe
 
attachment.php

Haya mabasi yatapelekwa wapi sasa?
 
Sipati picha Wale wapambe wa Mamvi sijui sasa hivi watakuwa na jipya gani?,Eti ooh!,safari ya matumaini,wengine ni waimbaji wa nyimbo zq injili wakampamba kana kwamba hawajui mapesa ya wananchi yaliyo ibwa na huyu mzee,wengine wanafunzi wa vyuo vikuu nao wakajifanya kumpenda kwelikweli!,eti atatengeneza ajira za vijana wapi na wapi!,wengine viongozi wa dini.
 
Hijawahi kutokea, mbwembwe zoote, pesa zoote na nguvu zoote alizotumia mh Edward lowasa na sasa ametolewa nje!

Janja ya lowasa ilionekana toka zamani alijifanya kuwa na upendo kwa makundi mengi ya kijamii ilhali akijulikana dhahiri kuwa hafai ktk urais.

Nimefurahi sana anguko la ufalme huu wa Giza CCM!
 
Ahsante Mungu kwa kusikia kilio cha watanzania, manake angepitishwa huyu mamvi waja wako tungepata shida sana.
Membe iz our new prezidaaaaaaaaa

Kura ziko kanda ya ziwa,hatutaki tena watu legelege !Maana tabia yao huwa kuwatisha raia kwa mabomu ili wawe na hofu na hivyo wasipingane na maamuzi yao yoyote hata kama ni mabaya!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Kumekuwa na ubaguzi wa hali ya juu sana ndani ya cm kuhusu watu wanaotoka kanda ya kaskazini na kihistoria watu wanaotoka kanda ta kaskazini wanapopewa nafasi za juu huwa wana deliver sana.
Mfano, sokoine, msuya nk

napenda niseme mwaka huu ni mwaka wa kaskazi piga ua galagaraza ni kaskazini dr.slaa,makamba,lowassa
 
Nami nasema piga ua URAIS ni Nyanda za juu kusini.
Utake Usitake.
 
Back
Top Bottom