Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Wakipitisha madudu bungeni Poa, Wakipitisha madudu huku kwenu povu hadi puani
Ndugu ntake radhi lini nimeunga mkono mambo wanayopitisha bungeni??? au umeshawai niona kwenye thread yoyote nikiunga mkono hilo jambo????
 
KAULI HII YA KINGUNGE MCHANA INASHTUA KIDOGO

kingunge2-620x308.jpg



KINGUNGE Ngombare Mwiru, ambaye ni kada mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ametabiri anguko na mpasuko mkubwa ndani chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, endapo chama hicho kitaacha kumpitisha mgombea urais anayekubalika kwa wananchi wengi.

Kauli hiyo imekuja mara baada ya jina la Edward Lowasa, aliyekuwa anasaka urais kwa udi na uvumba, kuenguliwa kutoka majina matano yaliyopendekezwa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CC- NEC).


Kutajwa kwa majina ya Bernard Membe, Dk. John Magufuli, Amina Salum Ali, January Makamba na Dk. Asha-Rose Migiro na Kamati kuu kwamba ndio watajadiliwa na Halmashauri Kuu (NEC), kumemfedhehesha Kingunge hata kusema, "…hatua ya kwanza itakuwa kumweka mgombea ambaye hakubaliki ndani ya chama na hakubaliki nje ya chama. Itakuwa ni kura ya hasira."



Kingunge ametoa kauli hiyo kwa kusitasita huku akionekana kuwa na huzuni wakati akifanya mahojiano na kituo kimoja cha luninga leo mchana.


Japo Kingunge hakutaja jina la Lowassa lakini ni muungwa mkono katika mbio zake za kuusaka urais hata wakati wa mkutano wa kutangaza nia mjini Arusha Kingunge alisema, "…Lowassa ndiye pekee anasifa za kuwa rais wa Tanzania."

"Utaratibu wa mwaka huu una matatizo. Kilichotokea ni mazingira yanayotia shaka. Kwa sababu ya muda hakuna atakae kata rufaa. Inaonesha kwamba uongozi umeshakuwa na msimamo juu ya mgombea wanaemtaka," amesema Kingunge.

Amesema kazi ya CC-NEC ni kuyapitia, kuangalia sifa, kuwapima, kuyalinganisha na kisha kutoa mapendekezo. Hawana madaraka ya kuamua.

Kuhusu kukubalika kwa majina hayo na NEC, Kingunge amesema, "…wajumbe wa NEC wanaweza kukubaliana nayo, wanaweza kusema hapana, wanaweza kusema wote waliopendekezwa hawafai na wanaweza kutoa mapendekezo waletewe majina mengine."
Amesema kuwa yanayotokea sasa na yatakayotokea baadae ni mazingira ambayo yamekuwa yakijengwa kwa muda mrefu.

Kuhusu sifa za mgombea anayemtaka, Kingunge amesema ni lazima: Aweze kupambana na nguvu ya upinzani; anayekijua chama; awe na uzoefu wa masuala ya ulinzi na usalama na mtu atakae watoa watanzani kwenye umasikini.


 
tbc1 kama vile wamekurupuka kutoka usingizini! Wamesema kamati inayapigia kura majina ma5 ili kupata ma3, wakati Nape amesema karibu lisaa lililopita kuwa wamekwisha pata majina ma3 ila haruhusiwi kutangaza mpaka kesho! Kizungurumkuti!
 
Napenda kuwapa pole wale wafuasi sugu na wale wote waliokuwa wapambe wa Eddo Lowassa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani .. ..Waswahili walisema "Ukiona ngoma inavuma sana ujue inakaribia kupasuka" na hicho ndicho kilichompata bwana eddo na team yake ...

Hivyo basi Ifike mahali tutambue kuwa unaweza kununua wadhamini wakakufurahisha machoni kwa wengi na hao hao wakakuangusha sirini ... Kilichotokea iwe fundisho kwa wale wote wanaodhani wamezaliwa kuongoza na hawapaswi kukosolewa wala kubugudhiwa!
 
Wakuu kwa mujibu wa mjumbe ndani ya kikao cha NEC amesema January, Magufuli na Migiro ndio waliopenya tatu bora.
 
Ndugu ntake radhi lini nimeunga mkono mambo wanayopitisha bungeni??? au umeshawai niona kwenye thread yoyote nikiunga mkono hilo jambo????

Umenielewa vibaya mkuu, hiyo ni kwa wale wanaolalamika kuhusu yaliyoyokea, kama wewe hulalamiki your safe.
 
Back
Top Bottom