Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Yawezekana nikweli ila kuna mchezo wa e luwasa hapo yawezekana kaamua kucheza karata yake kwa magufuli au yeyote hapo ili kulipa kisasi kwa membe
 
BAsi Magufuli ana nafasi kubwa
lakini uwepo wa hao wamama wawili katika hatua hiyo sio wa kuupuza hata kidogo. Inaelekea kuna agenda fulani nyuma yake. Inaweza kuwa ni bahati pia, kwa maana membe na makamba ilikuwa lazima watoke ili kutuliza hasira za makundi.
 
SIO RASMI....


Kauli ya Kikwete ya hivi punde kwa halmashauri kuu " Hii nchi ni ya Watanzania wote. Kila mtu ana haki ya kuhitumikia! Kila chama kina haki ya kushika dola na kutumikia wananchi kwa sababu ni nchi yao. Hakuna mwenye haki peke yake ya kuongoza nchi hii . Si chama wala mtu mwenye haki ya kipekee kuongoza nchi. CCM haipo peke yake kwenye mchakato huu.! Vyama vya siasa navyo vitaweka wagombea. Pia nao wanasifa ya kutumikia nchi yao. Ni wazalendo pia. Mzalendo akikosekana hapa CCM tunaweza kumpata ndani ya vyama vingine. Siyo dhambi! Nilimchagua Mbatia kutoka NCCR kuwa mbunge. Sikutenda dhambi!...sikulaumiwa! Mkichagua nje ya ccm hamtalahumiwa. Mtakuwa mmekidhi haja yenu ya kikatiba iliyo sahii kabisa. Ni lazima utaribu uheshimiwa la tutakuwa tumeshindwa kabla.......


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
 
Baada ya Jina la aliyekuwa akiaminiwa na watu wengi kuwa atakuja kuwa Kiongozi mzuri ndani ya chama cha mapinduzi CCM, ambayo watu wengi walianza kupoteza uaminifu haswa vijana kukatwa jina, Vijana na wasiovijana zaidi ya 10,000
wajipanga kuhamia UKAWA kutokana na utaratibu mbovu wa wanachama wa chama chicho tawala kuonekana kushindwa kufuata kanuni na taratibu za chama.
CCM go the Hell.......
Kundi hili la vijana walikuwa wameunda TEAM Lowassa, wamedai kuwa walikuwa UKAWA lakini wakahamia CCM baada ya kusikia kwamba Mhe,Lowassa anachukua Fomu.
Pia wamedai kuwa endapo lowasa atafanya maamuzi magumu na kuhamia chama chochote cha siasa,hatuna budi kuongozana naye.
Ili mradi aachane kabisa na SISIEM!!

Acha propaganda hakuna kitu kama hicho...je hao "so called vijana " wamejiandikisha kupiga kura?...kubalini tu matokeo..japo machungu.
 
Back
Top Bottom