pappilon
JF-Expert Member
- Jan 27, 2015
- 3,192
- 3,559
Wanabodi leo nguvu ya Lowasa ndani ya CCM imejidhihirisha wazi na hii ni kutokana na wajumbe wanaomsapoti kuamua kupiga kura za bora tukose wote na hili likifanyika watamchagua mgombea mwanamke tena wa kutoka Zanzibar na hilo likifanikiwa tu Lowasa njia nyeupe Magogoni kwani kwa gharama alizotumia na ambazo anaendelea kutumia mpaka sasa na kama kweli ACT ni chama chake na kwa jinsi alivyotumia nafasi ya kutafuta wadhamini kujitangaza nchi nzima na kuona jinsi anavyokubalika je akigombea kupitia ACT au chama chochote huyo Mama ataweza kupambana na Mamvi? Kwa mnaoanglia mkutano wa CCM unaoendelea sasa hivi imedhihirisha wazi EL ni chaguo la wajumbe karibu wote wa mkutano huo kwani kila linapotajwa jina lake ukumbi wote unalipuka kwa kushangilia je hamuoni kama hao wajumbe wanaweza mpigia mgombea mwanamke ambae kwa hali halisi Nchi yetu bado haijawa tayari kuongozwa na Mwanamke? Pia Mamvi ana sapoti kubwa sana ya wabunge wa CCM akiondoka nao si atakua amekimaliza nguvu Chama Cha Mapinduzi na kujisafishia njia kuingia Ikulu?
Mkuu sidhani kama team lowasaa watakubalo yaishe....nasita kukubali hilo...kwanza kabisa wanajiona kama jk aliwatumia na kisha kuwasaliti...mimi ningekuwa jk nisingemkata lowassa mapema...ningefanya kila liwezekanalo nimkatie kwenye cc...kama kweli jina lake halikufika cc...nachelea kusema mambo bado sana...sijui watamnyamazisha kwa kumpa ahadi gani...ugombea wenza labda sijui..kwenye mkutano mkuu lowassa alikuwa na hasira...alikuwa kama anataka kupasuka alivofura...hata aliyekuwa pembeni yake niliona kama alikuwa anaogopa hata kumnong'oneza kitu...sijui kama ile hasira itaisha hivi hivi... Sidhani kama atakubali yaishe...sidhani..