Yaliyojiri Kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu, Coplo Hafidh Abdallah Mohamed atoa ushahidi wake, kesi kuendelea Jumatatu 01 November 2021

WAJINGA TAYARI WAMEFUNGA TWITTER ATA KWA VPN HAIPATIKANI,UKWELI MBOWE NI BALAA !
 
Akimaliza huyu anakuja wa bangi, tutegemee naye ataitesti hapo mahakamani kama inavinasaba vya Afuganistani au Somalia, siku hiyo si ya kukosa na pia siku mahakama itakapohamia barabara ya Morogoro kwenye ushahidi wa jinsi ambavyo miti ingekatwa na kusambaza barabarani.
 
Endelea kujifariji Mama saidi.Huyu shahidi wa leo inaonyesha yupo vizuri.Halafu ndugu yangu usitushikie akili bana kwa kutuaminisha polisi wote hawajasoma,wengi tumehitimu nao vyuo vikuu.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Kuhitimu vyuo viguu siyo kipimo cha kuelimika ukute na we ulikuwa kwenye lile kudi la kuvuliwa chu..pi ili uchomoe supp. upate gpa nzuri. Mbowe siyo gaidi ni suala la muda watesi wake wote wataibika soon
 
Shahdi mtaalam wa kupima milipuko ya vituo vya mafuta / kuosha bunduki na magazine zake kwa spirit, bado tu hajaaza kuhojiwa to na makwakili wa utetezi.
 
kaka ukitaka kujua mtu ni mwerevu ama famba wala usihangaike wewe angalia matokeo yake ya kidato cha nne na sita tu.
 
Endelea kujifariji Mama saidi.Huyu shahidi wa leo inaonyesha yupo vizuri.Halafu ndugu yangu usitushikie akili bana kwa kutuaminisha polisi wote hawajasoma,wengi tumehitimu nao vyuo vikuu.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Hamna lolote hapo angekuwa amesoma miaka yote hiyo aliokaa polisi asingekuwa copro mpaka leo.
 
Acha kutuingiza chaka, graduates hawaendi CCP wanaenda Police College na wakifuzu wanaanza na jiwe moja...
CCP - Chuo Cha Polisi.
Police College - Chuo Cha Polisi.
Inawezekana alidhani China Communist Party (CCP).
Lugha gongana.
 
Hahaa mbona unajichanganya, kwani kati ya kazi na masomo kipi huanza?
Hizo kozi zote ni in job training hakuna kozi ambayo ameisoma nje ya polisi hapo. Labda kwa kukusaidia huenda shahidi amejikita kwenye swali aliloulizwa kuwa uko polisi makao makuu tangu lini?
 
tatizo mnao ripoti kesi hii ya mbowe mnaingiza ushabiki, hivyo mnapotosha ukweli wa kile kinacho jiri mahakamani.
ni bora mkakaa kimya tu.
maana mahakamani huwa sio sehemu ya ushabiki, ni ushahidi tu.
 
Kama ikiwezekana defense wangejaribu to determine ownership of the firearm kutoka kwa manufacturer. Ie where was sold and to whom. You might find it originated from some armoury
 
Ushahidi wa huyu ni kuwa pisto ni nzima inafanya kazi na yanani hajui na kama ilitumika hivi karibuni, na sidhani kama alichukua alama za vidole.
 
tatizo mnao ripoti kesi hii ya mbowe mnaingiza ushabiki, hivyo mnapotosha ukweli wa kile kinacho jiri mahakamani.
ni bora mkakaa kimya tu.
maana mahakamani huwa sio sehemu ya ushabiki, ni ushahidi tu.
Sio kweli,watu wanaripoti neno kwa neno mimi binafsi nilihudhuria mahakamani jana kuhakiki.

Na wewe nenda ushuhudie usiongee tu kwa hisia binafsi.
 
Nieleweshe, hivi unasomea kazi za polisi kabla ya kuajiliwa au unaajiliwa then unapelekwa kusoma?
Sijui sana kuhusu polisi ila nadhani huanza kuajiliwa halafu kutokana na uhitaji wa jeshi la polisi unaweza pelekwa nje ya nchi kusomea kozi mbali mbali kama vile:-

-Cyber security
-Forencic bureau 'Fb'..n.k


Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Mama asema anataka kuona haki kwa wote, hii picha iliandaliwa na jiwe sasa inachezwa tu, tusubiri itaishaje!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…