Kesi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake itaendelea leo katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa, ambapo upande wa mashitaka utaleta shahidi mwingine.
Fuatilia hapa kujua kitakachojiri katika mchakato mzima wa kesi hiyo kwa siku ya leo 29/10/2021
UPDATES
Mpaka sasa mawakili upande wa utetezi tayari wamewasili mahakamani.
Mpaka sasa ni saa nne kasoro, kesi bado haijaanza.
Jaji anaingia 3:50
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe dhidi ya Jamhuri inatajwa.
Wakili wa Serikali Robert Kidando anasimama kutambulisha
1. Robert Kidando
2. Nassoro Katuga
3. Ignas Mwanuka
4. Esther Martin
5. Tulumanywa Majige
6. Jenitreza Kitali
7. Abdallah Chavula
Wote ni Mawakili wa Serikali Waandamizi isipokuwa Jenitreza Kitali ni Wakili wa Serikali.
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Shauri limekuja kwa ajili ya kusikilizwa na Leo tuna shahidi Mmoja, tupo tayari Kuendelea
Jaji: Utetezi
Wakili Peter Kibatala: na sisi tupo tayari Kuendelea
Jaji anaandika
JAJI: Anakuwa Shahidi namba ngapi?
Wakili wa Serikali: Namba 03
Jaji: Majina
Shahidi: namba F 5914 D Coplo Hafidh Abdallah Mohamed
JAJI: umri
Shahidi: 38yrs
Jaji: Kazi S
hahidi: Askari Polisi
Jaji: Dini
Shahidi: Muislam
Shahidi: Mimi namba F5914 Coplo Hafidh naapa kuwa kwa ushahidi huu nitakaotoa utakuwa wa kweli, Eeeh Mwezi Mungu nisaidie
JAJI: KIAPO KIPO SAWA?
Jaji: asaidiwe
Shahidi: Mimi Coplo Hafidh nathibitisha kuwa Ushahidi nitaka toa utakuwa wa kweli, kweli mtupu, Eeh Mwenye Mungu nisaidie
Wakili wa Serikali: nitakuuliza Maswali utajibu kwa Sauti
Wakili wa Serikali: Kazi yako
Shahidi: Askari Polisi, nafanya Makao Makuu DSM
Wakili wa Serikali: Askari polisi tangu lini
Shahidi: 2013
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama tukufu Kituo chako cha kazi ni wapi
Shahidi: Forensic Beaural Dar es Salaam
Wakili wa Serikali: Forensic Beaureau ni kitu gani
Shahidi: ni Maabara ya Uchunguzi wa Kisayansi
Wakili wa Serikali: Upo Kitengo gani
Shahidi: Silaha na Milipuko
Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Kitengo chako kinahusika na Nini (Ballistic and Explosions)
Shahidi: Uchunguzi wa silaha na Milipuko
Wakili wa Serikali: Upo tangu lini?
Shahidi: Tangu 2014
Wakili wa Serikali: umesema Kitengo Chako Kinahusika Kuchunguza silaha, eleza Majukumu yako ya Msingi ni yapi
Shahidi: Kuchunguza Kitako cha Risasi(cartridges)
Wakili wa Serikali: Jingine
Shahidi: Kwenda Eneo la tukio kwa Uchunguzi
Wakili wa Serikali: Jingine
Shahidi: Kuandaa Riport baada ya Kuchunguza Ballistic and Explosion Report
Wakili wa Serikali: Jingine
Shahidi: Kutoa Ushahidi Mahakamani
Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama kama unajukumu lingine
Shahidi: Hakuna
Wakili wa Serikali: Mnafanya Mambo yapi
Shahidi: Kupokea Silaha mbalimbali zinazofanya Uhalifu, Je hii silaha Inafanya kazi..? Hii silaha ni Mzima..? Hii sasa ni Physical Examination.
Wakili wa Serikali: sasa Mnafanya nini
Shahidi: Tunafanya Visual Examination
Shahidi: hii Bunduki ni Mzima, Ina Koki,.? Ina Magazini.? Je Magazini ni Nzima..? Kama inagonga Vizuri kama Nyundo inanguvu..? NitaIkoki katika Upande wa Mitambo Inafanya Vizuri Je Fine pin Inafanya Kazi?
JAJI: fine pin ni nini?
Shahidi: Kiwashio cha Risasi
Shahidi: Nitaangalia Ndani ya Bao (Mtutu) internal Ballistic Ni Safi..? Nitaikoki kama Inafanya Vizuri, Ni hayo tu
Wakili wa Serikali: sasa Uchunguzi wa aina ya pili ni upi
Shahidi: Nimepokea Pistol au SMG
WS: Unaitwaje huu Uchunguzi wa Pili
Shahidi: Comparison Examination
Wakili wa Serikali: Kitu gani kinafanyika
Shahidi: Nachukua Ganda nililoletwa na Mteja Kisha napeka kwenye Mitambo Maalum
WSi: Unafanya hii Comparison Kubaini nini
Shahidi: Je hii Risasi inasifa hii
Wakili wa Serikali: Mnatumia Mitambo Maalum
Shahidi: Unaitwa Computer Microscope and digital Camera Forensic Machine LAECA 2004
Wakili wa Serikali: Umeeleza Vyema, Kuhusu Uchunguzi wa Silaha Kwenye Risasi unafanya kitu gani
Shahidi: Kitaalamu inaitwa Life ammunition...Risasi itaangalia Kiwashio, Je imegongwa..!
Wakili wa Serikali: na hiyo Miss fired ieleze Mahakama, Je live ammunition ikiwa Miss fired Maana yake ni nini
Shahidi: Ni mbovu sababu ulipiga haikulipuka
Wakili wa Serikali: fafanua sasa Mahakamani endapo haijagongwa ni vipi
Shahidi: kama haijagongwa ni Nzima
Wakili wa Serikali: Tofauti na Kugomgwa na kutokugongwa Mnafanya kitu gani
Shahidi: tunaangalia Gun Powder Resolutions
Shahidi: kwemye Risasi Kuna Powder tunaangalia Je powder yako imeganda au Nzima
Yani Bullets Catridge tuna angalia Michuruzi yani Internal Ballistic
Hizo alama za Kipekee tunasema Proved, Shahidi Tuna angalia kitu kinaitwa Twist, Twist silaha/Risasi Kuna Twist Right na Twist Left, Na angalia Counts inasema Twist Right na Left Nyingine unapopiga Kuna Counts Mbili unapopiga Mpaka Kumdhuru Mtu. Inatusaidie Silaha mbalimbali zinazoweza Kufanya uhalifu
Wakili wa Serikali: Tumalizie kwenye Mlipuko, unachunguza nini
Shahidi: Inapotokea Mlipuko wowote sisi tunakwenda Kwenye Eneo la Tukio (SCENE), Wanaenda Askari wa awali. Alafu tunaenda sisi wataalamu Kuangalia kama Kilichotokea ni Local Explosive au Industrial Explosive
Wakili wa Serikali: Wewe unautalamu gani sasa,
Shahidi: Kuchunguza Silaha Mbalimbali ambazo zinatumika kwenye Uhalifu
WS: Kozi ya kwanza
Shahidi: Kuchunguza Maganda ya Risasi Mbalimbali
WS: Ulifanya kwa Muda gani
Shahidi: kwa Miaka 2
Wakili wa Serikali: kingine tofauti ya kuchunguza
Shahidi: Kuandaa Riport za Kitaalamu
Wakili wa Serikali: Kozi gani Nyingine umefanya
Shahidi: Kozi ya Uchunguzi wa awali ya Upelelezi, Basic CID course
Wakili wa Serikali: Ulifanya Mwaka gani na wapi
Shahidi: Mwaka 2004 kwenye Polisi College Zanzibar
Wakili wa Serikali: Ulijifunza nini huko Zanzibar
Shahidi: Nilijifunza Mambo mbalimbali ya Kiupelelezi, Nilijfunza Bunduki Kupiga, Kuchukua alama za Vidole, kutafuta Finger Prints. Kulift Finger Prints, baada ya Kuchunguza Finger prints na Kuhamisha
Wakili wa Serikali: Kingine
Shahidi: Kufungua na Kuirudishia Bunduki
Wakili wa Serikali: Kingine
SHAHIDI: Nilipata Elimu ya awali Juu ya ku Collect Ushahidi Katika Crime scenes
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama kama ulioata Kozi Nyingine
Shahidi: Baada ya Kurudi Ofisni nilihitajika kwenda Kozi Nyingine Moshi Mwaka 2006
Wakili wa Serikali: Ulijifunza kitu gani
Shahidi: Techniques, protocol in Fire arms Evidence
Wakili wa Serikali: fafanua
Shahidi: Kufungua silaha, Vifaa vyake Kuirudishia, na Kutengeneza kama inawezekana NikAfanya Polisi College Dar es Salaam ambayo inaitwa Ballist tools, fire arms, tools and Ballistic Materials testing Mwaka 2007.
Wakili wa Serikali: Kozi Nyingine
Jaji: Jina Kozi rudia
Shahidi: To determine and Examination of fire arms
Wakili wa Serikali: Wapi
Sahidi: Botswana police College Mwaka 2010
WS: NYINGINE
Shahidi: 2015 inaitwa Forensic in General
Ballistic Woundage, Vidonda, Mtu amepigwa Bastola amekufa naangalia Shooter alikuwa Upande gani
Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Utaratibu wa Kupokelewa Vitu Vya kufanyia kazi ukoje
Shahidi: Kwanza Mteja awe na Barua
Wakili wa Serikali: kwenye Barua kuna kuwa na nini
Shahidi: Barua ionyeshe kosa
Wakili wa Serikali: Kingine
Shahidi: aeleze nini anaomba tumfanyie
Wakili wa Serikali: Tofauti na Barua anakuwa na Nini
Shahidi: aje na hivyo Vielelezo husika sasa
Wakili wa Serikali: Barua pamoja na Vielelezo hupokelewa eneo gani na nani anapokea
Shahidi: anakuwa Afisa wa zamu anayetupangia Leo utakuwa zamu na Kupokea Vielelezo Tunakuwa wawili
Wakili wa Serikali: Makishapokea kama Afisa wa zamu anafanya nini
Shahidi: Tunapokea Barua na Kielelezo nafungua Kujiridhisha Alivyovileta yupo sahihi
WS: Ofisini Kwako Unapofanyia kazi, ifahamishe Mahakama Silaha au Mlipuko I natokea wapi
Shahidi: Vituo Vya Polisi na hata TANAPA kuja Kufanya Uchunguzi
WS: ieleze Mahakama Utaratibu wa Kupokelewa Vitu Vya kufanyia kazi ukoje
Shahidi: Kwanza Mteja awe na Barua
Alivyovileta yupo sahihi
WS: Ukishajiridhisha
Shahidi: Lazima niangalie Safety kabla haijaingia Laboratory
WS: Umeshajikizisha Vielelezo na Usalama sasa, Unatakiwa Ufanye kitu gani
Shahidi: Natakiwa Kuingia Laboratory nitai Register
WS: Barua pamoja na Vielelezo hupokelewa eneo gani na nani a napokea
Shahidi: anakuwa Afisa wa zamu anayetupangia Leo utakuwa zamu na Kupokea Vielelezo, Tunakuwa 2
WS: Mkipokea kama Afisa wa zamu anafanya nini
Shahidi: Tunapokea Barua na Kielelezo nafungua Kujiridhisha
WS: inapelekwa kwa Afisa incharge kwa Madhumuni gani
Shahidi: Lazima atambue ni silaha gani, Na nitampa Mtu Kuchunguza hii Kesi
WS: ieleze Mahakama Mnamo tarehe 25 November Unakumbuka ulikuwa wapi
Shahidi: Nilikuwa Ofisini Kwangu Makao Makuu madogo Dar es Salaam
WS: Kwa Kufanya nini
Shahidi: Nita andika Exibit K1 nitaweka FStroke ya Mwaka gani
Wakili wa Serikali: inapelekwa kwa Afisa incharge kwa Madhumuni gani
Shahidi: Lazima atambue ni silaha gani Na atampa Mtu Kuchunguza hii Kesi
WS: baada ya Kusajili Vielelezo Upelekwa wapi
Shahidi: Nitapeleka Sehemu ya Kuhifadhi silaha WS Barua utaipekeleka wapi
Shahidi: Kwa Afisa Incharge
Wakili wa Serikali: inapelekwa kwa Afisa incharge kwa Madhumuni gani
Shahidi: Lazima atambue ni silaha gani Na atampa Mtu Kuchunguza hii Kesi
Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Mnamo tarehe 25 November Unakumbuka ulikuwa wapi
Shahidi: Nilikuwa Ofisini Kwangu Makao Makuu madogo Dar es Salaam
Wakili wa Serikali: Ulikuwa wapi
Shahidi: Kwenye Dawati la Kupokea Vielelezo Mbalimbali
Wakili wa Serikalil Ulipokea Vielelezo Vipi Siku hiyo
Shahidi: nikipokea Vielelezo Kutoka Ofisi ya DCI, Ambavyo ni Pistol yenye namba A5340 callibre 9mm, Ikiwa na Magazine Yenye Rangi Nyeusi Na Nikapokea Risasi 03 WS: za Silaha gani
Shahidi: za Pistol Caliber 9mm
Wakili wa Serikali: Vielelezo hivyo viliambatana na nini
Shahidi: kwanza alivileta PC Goodluck kutoka Ofisi ya DCI
Wakili wa Serikali: Goodluck aliwasilisha nini
Shahidi: Barua
Wakili wa Serikali: baada ya Kupokea Vielelezo hivi na Barua ieleze Mahakama Ulifanya nini
Shahidi: Nilivi-Lebel kama nilivyosema awalI Pistol niliioa alama Exhibit K1, Nikosa ili kwa FB /BALL/LAB 158/2020
Wakili wa Serikali: na hizi Risasi 03
Shahidi: nilizipa alama ya K2 K3 na K4 Wakili wa Serikali: Risasi hizi ulizipa Usajili upi
Shahidi: 158 Kama Pistol
Wakili wa Serikali: Baada ya Kukamilisha Usajili wa Vielelezo Ulichukua hatua gani
Shahidi: Kufanya Uchunguzi wa Kuutambua Hiyo Bunduki na Risasi ni Nzima K2, K3 na K4
Wakili wa Serikali: na Kuhusu Vielelezo Pistol na Risasi ukafanya nini
Shahidi: Kwanza ile Pistol niliipima
Wakili wa Serikali: Kabla ya Kupima, Tupo kwenye hatua ya Upokeaji
Shahidi: Nika-Minutes Kumpelekea Boss
Wakili wa Serikali: Vielelezo Ukapeleka wapi
Shahidi: Nilipeleka Chumba cha Kuhifadhia Silaha
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Nani aliteuliwa kufanya Uchunguzi
Shahidi: Mimi Mmoja wapo
Wakili wa Serikali: Uchunguzi huo ulifanya lini
Shahidi: nilianza Kufanya Tarehe 25 Uchunguzi wa Awali
Wakili wa Serikali: Katika Uchunguzi wako Ulifanya nini Kulingana na Mahitaji
Shahidi: Hatua ya kwanza
Wakili wa Serikali: Mteja alikuwa anataka nini
Shahidi: Mteja alikuwa anataka Kujua ile Pistol na Risasi zilifanya kazi
Wakili wa Serikali: sasa wewe Ulifanya nini
Shahidi: Kwanza Ile Bastola nilipima na Kifaa kinaitwa GUN BARROW GAUGE
Hapo nilikuwa napima Kwenye Barrow yani Mtutu kwamba ile Callibre ni kweli 9mm
Nikaona ni kweli ipo sahihi ni 9mm
Wakili wa Serikali: KingiNe
Shahidi: nikatoa Magazine kumbuka ilikuwa na Magazine inaitwa MAGAZINE RELEASE, Naangalia Magazine yake ile Bastola ni ya kwake, Nikaona Okey Magazine ni ya Kwake
Wakili wa Serikali: Jingine
Shahidi: Ndani ya Magazine Kuna Spring ambayo Ukiweka Risasi inashuka Chini, yenyewe inapandisha Risasi juu, Nikaona Nzima Nikaangalia Nyundo Hummer Kama Nzima sometime inakuwa loose nimabaini, Nzima Nikaangalia Triger kwa kutumia Triger Pull ....kama inafika kwenye 100 nimEbaini ni Nzima
Shahidi: Nikaenda ndani ya Barrow nikatumia Mdeki Kuangalia kama Ilikuwa Safi au Chafu Kupoteza Ubora wake, Nimabaini Barrow lipo Vizuri halina Vumbi hakuna Mchanga Maana yake Barrow lipo safi, Lolote linaweza Kufanya Baada ya hapo nikaikoki kungalia Firing Pin Mechanism kama ..Nilibaini Ipo
Kwa hatua hiyo niliishia hapo
Wakili wa Serikali: Kwa Aina za Uchunguzi ulizotutajia huu ni Uchunguzi wa aina gani
Shahidi: ni Visual Examination
Wakili wa Serikali: kwenye zile Risasi 3 ulichunguza nini
Shahidi: pale niliingia Sana kwenye Pin Impresion kwa Maana Primer au Kiswahili Chake ni Kiwashio au Kitako cha Risasi
Wakili wa Serikali: Hatu gani ikafuata Shahidi: Hatua ya Pili ya Uchunguzi wa Pili
Shahidi: Nilichukua Risasi Mbili ya zile nilizoletewa callibre yake 9mm, Nikaenda kwenye Chumba Maalum Kwenye Chumba Kuna sehemu ya kupigia Silaha Mbalimbali.
Wakili wa Serikali: Ulienda na Kitu gani
Shahidi: Nilikuwa na Pistol na Risasi 03
Wakili wa Serikali: Ulienda Kufanya akitu gani hasa
Shahidi: Kuna Kifaa kinaitwa Tank Water Recovered Bullets
Ws: Kiswahili ni nini
Shahidi: Ni tanki la Maji tunalotumia kupata risasi
Wakili wa Serikali: Kwanini sasa Mnapiga Risasi Kwenye Tanki la Maji
Shahidi: ili Kupata Maganda ya Risasi na Vichwa vyake
Wakili wa Serikali: Kwanini sasa Mnapiga Vile Vielelezo
Shahidi: Najiridhisha sasa, Je Ni kweli zile Risasi ni Nzima.? Na kwenda Kupiga sasa
Wakili wa Serikali: Nini Matokea ya Uchunguzi wa Kina
Shahidi: Nikichukua Risasi Mbili nikaweka Kwenye Magazine Nikaweka kwenye ile Bastola nikapiga sasa, nikapata Maganda na Vichwa Vya risasi. Nikafanya hivyo tena kwa Risasi ya pili, nikapiga
Wakili wa Serikali: Risasi zako zilikuwa na alama, Je Risasi zina alama zipi ambazo ulipiga
Shahidi: K2 na K4
Wakili wa Serikali: Ulifanya nini sasa kuhusiana na Yake maganda
Shahidi: Nilienda kuyalebo yale Maganda yangu mawili
Wakili wa Serikali: Kwa kuyapa alama gani
Shahidi: T1 na T2, T1 ilikuwa K2 na T2 iliyokuwa K4
Wakili wa Serikali: baada ya Labeling Kitu gani sasa Kingine kilifuata
Shahidi: Nikaenda Kuandaa Report yangu (Ballistic Examination Report)
Wakili wa Serikali: baada ya Kuandaa Ulifanya nini
Shahidi: Nilisaini
Wakili wa Serikali: Kingine
Shahidi: Nilipiga Muhuri
Wakili wa Serikali: Muhuri gani
Shahidi: Forensic Beaural Dar es Salaam
Wakili wa Serikali: Kuhusiana sasa na Silaha Yenyewe
Shahidi: Baada ya hatua zote zote hizo nikafunga kwenye Mfuko na Nikafunga seal, nikasaini na Kuandika Tarehe
Wakili wa Serikali: Baada ya Kusaini Ukapeleka wapi
Shahidi: Chumba cha Kutunzia Silaha Wakili wa Serikali: Na Report yako sasa
Shahidi: Niliweka kwenye Bahasha na Nikairudisha kwenye File Book. Baada ya hapo nikiwa nasubiri wenyewe Waje Kuchukua Vielelezo vyao
Wakili wa Serikali: Vielelezo Vyao Vilikuwa Kuchuliwa Siku gani
Shahidi: Tarehe 27 November 2020
Wakili wa Serikali: Nani alikuja Kuchukua Vielelezo hivyo
Shahidi: Afande Swila Kutoka Ofisi ya DCI
Wakili wa Serikali: Nani aliyemkabidhi afande Swila hivyo Vielelezo
Shahidi: Mimi Mwenyewe
Wakili wa Serikali: Ulimkabidhi Swila Vitu gani
Shahidi: Riport yangu ya Kiuchunguzi Ballistic Examination Report, nikamkabidhi Pistol Moja ambayo ni Exibit K1 Callibre A5340 9mm Model yake CZ 41 Rangi Nyeusi Ikiwa na magazine yake. Pia nikamkabidhi Risasi Moja Nzima iliyobaki Ambayo nili nililebel K3. Nikamkabidhi Maganda Mawili na Bullets zake Yale Maganda niliyalebel kama T1 na T2
Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Kwamba tangu ulivyomkabidhi Swila ni Lini tena ulipata Kuviona tena Vielelezo
Shahidi: Jana
Wakili wa Serikali: Kwa Jambo lipi
Shahidi: ili aniletee Vielelezo Kwa ajili ya Ushaidi Mahakamani hii Leo.
Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama hii Report yako ya Kiuchunguzi uliyoiandaa ni kitu gani kitakutambulisha
Shahidi: Kwanza Kwa Nembo ya Ofisi, Nembo ya Polisi Force a namba zangu F5914 Majina yangu ya Copo Hafidh Abdallah
Wakili wa Serikali: Kingine
Shahidi: Na Signature Na Muhuri wa Ofisi
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi anaonyesha anaweza akatambua Nyaraka aliyofanyia Kazi kwa Ruhusa ya Mahakama Tunaomba Kumuonyesha Shahidi anakabidhiwa
Wakili wa Serikali: Shahidi itizame hiyo Kabrasha Ndogo sasa Uimbie Mahakama nilichokupatia ni Kitu gani
Shahidi: Ni report Yangu niliyoindaa kuhusiana na Uchunguzi wa Silaha na Risasi
Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama Vitu gani vinaonyesha wewe Ndiyo uliandaa
Shahidi: Kuna Nembo ya polisi, Force Namba, Signature yangu, Kuna Muhuri wa Ofisi kwa hiyo Riport hii ni ya kwangu
Wakili wa Serikali: Unaiomba nini Mahakama hii
Shahidi: Naomba Mahakama hii Ipokee Riport yangu kama Sehemu ya Ushahidi
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi anaomba Ipokelewa Ballistic Examination Report Wakili wa Serikali Wanaipeleka Upande wa Mawakili wa Utetezi
Nashon Nkungu: kwa niaba ya Mshitakiwa wa kwanza sina Pingamizi
John Mallya: Kwa niaba ya Mshitakiwa wa Pili Pia sina Pingamizi
Dickson Matata: Kwa niaba ya Mshitakiwa wa tatu pia hatuna Pingamizi
Peter Kibatala: Kwa niaba Ya Mashitakiwa wa Nne pia hatuna Pingamizi
Jaji anapelekewa Nyaraka Mahakama bado Ipo Kimya Kidogo, Jaji anaendelea kuandika
JAJI: Mahakama Imepokea Nyaraka Hii yenye Kichwa cha Habari Ballistic Report Ambayo iliandaliwa tarehe 26 November 2020, Napokea na Kama Kielelezo namba 02
Jaji: Nakuomba Shahidi usaidie Kuisoma
Shahidi anapewa
Shahidi: Forensic Beaural Ballistic Laboratory DSM/F Ya Tarehe 26, Nov 2020 Shahidi anaisoma upya yote
Shahidi amemaliza Kusoma Riport yote ambayo Ndiyo yale aliyokuwa anayaeleza, lakini Sheria inataka asome Upya Mahakamani.
Wakili wa Serikali: Kwa mujibu wa a Taarifa hiyo ulikuwa unachunguza silaha ya aina gani
Shahidi: Pistol A5340 ya Callibre 9mm
Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa Uchunguzi wako Ulibaini nini Kuhusu Bastola
Shahidi: Ni Nzima
Wakili wa Serikali: Unamaanisha Nini Nzima
Shahidi: Ukiweka Risasi inalipua
Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa Taarifa yako uliyofanyia Uchunguzi Risasi tatu, Je za Silaha gani
Shahidi: za Pistol caliber 9mm
Wakili wa Serikali: Uhusiano wake Risasi na Bunduki ukoje
Shahidi: Ni za Kwake, kwa Maana zimeingia na Ikapiga (Fire)
Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa Taarifa yako umesema Unaambatanisha K1, K2, K3 na K4, was attached, sasa Elezea kwanini Kwenye Taarifa Yako Umeandika tena K4 Wakati unasema Ulishailipua
Shahidi: Nimekosea Mheshimiwa Jaji, Ni Typing Error Kwa sababu Nilishailipua.
Wakili wa Serikali: Kwa hiyo attachments zitakuwa ni nini
Shahidi: K1 ambayo ni Bastola na K3 Wakili wa Serikali: Ukionyeshwa utavitambuaje
Shahidi: Nimeweka Kwenye bahasha, nimesaini nikaandika na tarehe
Wakili wa Serikali: Mbali na hivyo, silaha ina vitu gani Vingine vitakavyokufanya uitambue
Shahidi: kwanza ni serial Namba, Lebbeling ya Forensic ambayo ni K1 FB /BALL /LAB 158 of 2020 Maganda niliya-Lebel kwa T1 na T2 Na vile vile Nika-Lebel FB /BALL /LAB 158 of 2020
Na Bullets nili-Lebel kwa Maganda yake
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi ameonyesha Uwezo wa Kuvitambua, Kwa Ruhusa ya Mahakama naomba Kumuonyesha anaruhusiwa na mahakama Shahidi Tizama Mfuko Mmoja baada ya Mwingime Shahidi anatizama Mifuko ya Nailon ambayo ni Transparent
Wakili wa Serikali: Huo Mfuko ni nini
Shahidi: Mfuko wa Kuwekea Vielelezo Mbalimbali
Wakili wa Serikali: Una uhusiano gani na wewe Shahidi
Shahidi: Ndiyo nilitumia kuweka Bastola
Wakili wa Serikali: Kitu gani Kinachotambulisha kuwa wewe ndiye Ukiweka silaha
Shahidi: Nilisaini nikaweka na Tarehe 26 November 2020
Wakili wa Serikali: Unasema Kwenye Mfuko huo kuna Kitu gani
Shahidi: Bastola yenye serial Namba A5340 Callibre 9mm CZ 100 nyeusi
Wakili wa Serikali: Mfuko wa Kwanza
Shahidi: Una Risasi, na Nika Lebel na Nikafunga Kwa Seal
Wakili wa Serikali: Kinachokutambulisha kuwa wewe Ndiye Uliweka
Shahidi: Nilisaini na Nikaweka Tarehe, ina alama Exibit K3
Wakili wa Serikali: Tumalizie Mfuko wa Mwisho
Shahidi: Niliweka Maganda T1 na T3 na Bullets zake
Wakili wa Serikali: Unaiomba nini Mahakama
Shahidi: Naomba Mahakama hii Ipokee Vielelezo hivi kwenye kesi husika Wakili wa Serikali: Ipokee nini
Shahidi: Bastola yenye serial Namba A5340 Callibre 9mm ikiwa na Magazine Nyeusi kwa Rangi yake, Model ni CZ 100.
Wakili wa Serikali: Kwenye hiyo Mifuko Mingine
Shahidi: Naomba Mahakama Ipokee Risasi ya Pistol ya Callibre 9mm
Wakili wa Serikali: Uliipa alama gani
Shahidi: K3
Wakili wa Serikali: Mfuko wa Mwisho Mahakama Ipokee
Shahidi: Maganda Mawili ya risasi na Bullets Mbili (Vichwa Vya Risasi)
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi ameomba Vielelezo ambavyo amevitaja Vipokelewe na Mahakama
Wakili wa Serikali Wanaipeleka Mifuko 3 kwa Mawakili Wa Utetezi Mawakili Wa Utetezi Wamezingira Vielelezo wanavikagua Kimoja baada ya Kingine vikiwa bado ndani ya Mifuko.
Nashon Nkungu: Kwa niaba ya Mshitakiwa wa kwanza hatuna Pingamizi dhidi ya Vielelezo hivi vyote kwa Pomoja
John Malya: hatuna Pingamizi kwa niaba ya Mshitakiwa wa Pili
Dickson Matata: Hatuna Pingamizi kwa Vielelezo Vyote
Peter Kibatala: Mhe. Jaji nasi pia hatuna Pingamizi
Jaji anainama anaandika Kidogo Jaji anawakumbusha kuwa Mahakama Ya Rufani imesema Kuwa Vielelezo havipaswi kupokelewa kwa pamoja Kwa hiyo kwa namba nitavipokea Kwa tofauti tofauti.
Jaji: Basi Mahakama Inapokea Silaha Moja ya Moto aina ya Pistol aina ya A5340 kama Kielelezo Mahakama Inapokea Maganda Mawili ya Risasi ambayo yametumika kama T1 na T3
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Sasa Shahidi akate Mifuko ili aweze Kutuelezea anaruhusiwa Shahidi anachana Mifuko MAHAKAMA ipo Kimyaaaaa
Wakili wa Serikali: Shahidi hiyo unasema ni silaha ya aina gani
Shahidi: Ya Pistol
Wakili wa Serikali: anaishika na yeye
JAJI: Wakili wa Serikali nakutaadharisha ulivyoibeba naona Unamuelekezea Jaji MAHAKAMA KICHEKO Kidogo
Wakili wa Serikali: hii ni Pistol ya aina gani
Shahidi: Luger ya 2005
Wakili wa Serikali: elezea mahakama ulivyokuwa unaelezea hii Pistol
Shahidi: Hiki ni Kifunguo cha Magazine Ukiminya Unaruhusu Magazine Itoke Magazine hii inauwezo wa Kuchukua Risasi nane
Wakili wa Serikali: Unasema Ulitest Magazine
Shahidi: Ukibonyeza hii spiring, nilipima Kama Inanguvu ya kusukuma Risasi Na hiii ni Box Magazine, Na Magazine hii ni Nzima
Wakili wa Serikali: na Ulisema Barrow ndiyo ipi
Shahidi: Ndiyo hii kwa Kiswahili ni Mtutu. Nilipima kwa Kuchukua Barrow Gauge nikatoa kwenye Barrow, Je hii ni 9mm, Ikaniambia ni Yenyewe
Wakili wa Serikali: Ulisema Triger, Triger eleze Triger ipo wapi
Shahidi: nilipima Triger kwa Kuminya hivi, Nikaona Ikafika kwenye 100
Wakili wa Serikali: Kwenye 100 Ikafika hapa
Wakili wa Serikali: Hebu onyesha Mahakamani Firing yake na Uwezo wake
Shahidi: Hapa naikoki, hii ni Pini na hapa Nikikoki pana kuwa na Risasi inaenda Chemba nikaikoki nika-fire nikaona Nyundo Inagonga Vizuri.
Wakili wa Serikali: Kitu gani Nyingine Ulifanya
Shahidi: Nilipima Barrow Kupima Kama ni safi, Nikaona Barrow ipo Safi hii ina serial Namba hawa Luger wanaweka Serial Namba hapa na hapa
Wakili wa Serikali: Ni ipi
Shahidi: Imesajiliwa A5340 Kama haijagongwa serial Namba sijajua imeingia Vipi Nchini hii pia ni Risasi niliipa K3
Wakili wa Serikali: Ulichunguza nini kwenye hii Risasi
Shahidi: Nilichunguza Kiwashio, hapa ikiwa na Chuma Ukigonga inalipuka
Wakili wa Serikali: Kiwashio cha hiyo Risasi kikoje
Shahidi: Kizima
Wakili wa Serikali: Twende Kielelezo Cha Mwisho
Shahidi: Haya ni Maganda Kama Ulienda Marekani wanakuandika 9mm Pass 50 Kwamba Kutoka kwenye Base hadi kwenye Kichwa ni Pass 50 Hizi mbili ni Bullets nimezipata baada ya Kupiga kwenye tenki la Maji Kwa Maana hazikudhuru Mtu. Wanaita Terminal Firing Shahidi anarudishia Vielelezo kwenye mifuko yake
Wakili wa Serikali: Mwisho, kwa ufupi nini Ugunduzi wako
Shahidi: Kwamba Vyote Kuanzia Bastola na Hizo Risasi 3 ni Vizima na Vinafanya kazi
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji ni hayo tu
Jaji: upande wa Utetezi
Wakili Peter Kibatala: Naomba kwa Ruhusa yako nimtambulishe Jeremiah Mtobesya ambaye alichelewa kwa sababu alikuwa Mahakama ya Rufaa Na ninamatambulisha kwa sababu Yeye Ndiye ataanza Maswali Kwa niaba ya Mshitakiwa wa kwanza
Jaji anaandika Kidogo
Jaji: naliingiza Jina lako kwenye Orodha ya Mawakili
Jaji: Nitaruhusu watu wapumzike Kidogo kunyoosha Miguu na Kupata maji Mpaka Saa saba Na nusu
Naomba tujitahidi Kutunza Muda
Jaji anatoka