Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kinakutana leo chini ya Mwenyekiti wake Rais Magufuli. Miongoni mwa agenda ni kupitisha majina ya wagombea wa nafasi za Ubunge na Uwakilishi.
Mkutano utarushwa mubashara na Channel ten, TBC na ITV
Up dates;
Wajumbe wa halmashauri kuu tayari wameanza kuingia ukumbini na wengine wanajadiliana hili na lile kwa bashasha.
Mwenyekiti wa chama Dr Magufuli ameshaingia ukumbini na sasa mwenezi komredi Polepole anaelezea utaratibu.
Na sasa Katibu mkuu Dr Bashiru anazungumzia makusudi ya kikao na kwamba kikao hiki kitafanya uteuzi wa wabunge tu kwa sababu ratiba za NEC na ZEC ni tofauti.
===
Hotuba ya mwenyekiti wa CCM( - Dkt. John Pombe Magufuli)
Ameanza kwa kutoa salamu kwa wajumbe wote na viongozi mbalimbali wa chama cha Mapinduzi.
Anapenda kuwakaribisha na kuwashukuru kwa kuhudhuria mkuano mkuu na pia anawashukuru wajumbe wa NEC kwa kumpigia kura. "Napenda niwashukuru sana wajumbe wa NEC kwanza kwa jinsi mlivyonipigia kura nyingi, mlikuwa wajumbe hamkuniangusha wajumbe". Mlipokwenda kwenye maeneo yenu mlishiriki kwa upendo mkubwa sana kunitafutia wadhamini na wadhamini walipatika zaidi ya milioni moja point moja.
Nilipotuma wawakilishi kwa ajili ya kwenda kunitafutia wadhamini ili kutimiza masharti ya NEC mlikwenda na nimepata udhamini kwa mikoa mingi sana ya Tanzania bara na Zanzibar nasema hongereni sana na asanteni sana.
Wajumbe wa mkutanao na kikao hiki muhimu natambua kuwa wengine mmesafiri usiku na umbai mrefu ili kuwahi mkutano huu muhimu nasema hongereni sana hii inaonesha mnatambua umuhimu na manakipenda chama chetu.
Mkutano huu una ajenda moja kubwa kufanya uteuzi wa wagombea wa ubunge na uwakilishi kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi. Zoezi la uteuzi ndani ya chama lilianza takribani mwezi mmoja umepita na wajumbe walipiga kura na baada ya kujadiliwa na kamati mbalimbali pia wamefika kwenye mkutano huu ili pia wajadiliwe.
Napenda kuwapongeza wanachama waliojitokeza kugombea nafasi mbalimbali na walijitokeza wengi sana na hiyo ni kwa kuwa wanakipenda sana hivyo nasema hongereni sana.
Wana CCM 10367 walichukua fomu za ubunge wa majimbo na viti maalum na waliojitokeza kuwania ubunge baraza la uwakilishi ni 786 na waliojitokeza kuwania udiwani katika kata wodi na viti maalumu walikuwa 33094 kwa hiyo mytaona waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali walifika 44461 haya ni mafanikio makubwa kwa chama chetu na nafasi hizi ziliomba na watu wa kaliba na tofauti tofauti.
Katika kipindi cha miaka mitano nimekuwa nikiwaona mitembelea miradi mbalimbali na mkikemea kwa waliozembea na kutoa maelekezo mbalimabali na miradi mingi imekamilika na haya ndio matunda ya ufanyaji kazi wenu na ndio maana watu wengi wamejitokeza kuomba nafasi mbalimbali.
Juzi na jana majina ya wagombea yalijadiliwa kwenye vikao katika ngazi ya kamati ya usalama na maadili na kisha kamati kuu kwa ajli ya uchambuzi wa kina na uchambuzi wa kina kweli kweli tulitumia taarifa tulizozipata kupitia vyanzo mbalimbali na kwa yule atakayepata ufafanuzi basi atapatiwa maana nilisoma majina yote kwa kina na hatutakuwa tumempendelea mtu au kumuonea mtu .
Ilitulazimu kutumia taarifa nyingi ili atakaechaguliwa awe na uwezo wa kuipeperusha bendera na awe na uwez wa kungoza nchi yetu na hiyo ni kutokana na unyeti wa nafasi wanayogombea kwa kuwa ndiyo wawakilishi wa wananchi maana ndimo atakapopatikana waziri mkuu na viongozi wengine hivyo ilibidi tuchague mwenye sifa ya kuwa kiongozi.
Ikiwemo kupata viongozi wenye uwezo wa kuongoza, wazalendo, wenye kujitoa kwenye chama wanaofahamu mahitaji ya wananchi wanaokubalika na wananchi na na wenye utayari wa kuwatumikia wananchi na watanzania wote.
Baada ya kufanyika kwa mchakato kwenye ngazi mbalimbali halmashauri kuu ndio imepewa mamlaka ya mwisho kufanya uteuzi wa wagombea kwa mujibu wa kifungu namba 102 ibara ndogo ya 12 g ya katiba ya CCM ya 1977 na toleo la mwaka 2017.