Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM: Majina ya walioteuliwa kuwania nafasi za Ubunge kwenye Majimbo mbalimbali nchini

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM: Majina ya walioteuliwa kuwania nafasi za Ubunge kwenye Majimbo mbalimbali nchini

Mimi nawajuwa vizuri lakini mikakati iliyopo inaniogopesha, halafu hawa jamaa wapo kimya kabisa.

Cha kushangaza mpaka wazee wa kichaga wameingia MoU na ccm kuwapa majimbo ccm ili watoto wao waingizwe serikalini serikali ijayo, ndio sababu hata yule katibu mkuu wa maliasili na utalii kaenda kugombea kwao Rombo na anakwenda kuwa mbunge wa Rombo.

Arusha kama watu wa kawaida wana imani na Lema basi atadhinda, lakini upande wa matajili wameshamwagiwa sumu.
Dah,Mkuu unadonoa!
 
Uimara was ccm hilo halina shida.Shida no pale wanaoo tumia dola na raslimali za Taifa kuminya Uhuru wa vyama vingine.Miaka mitano vyama vimezuiliwa kufanya kazi .TV zote hazi onyeshi matukio ya wapinzani.Niccm tu
Kama yote hayo yangekuwa yanafanyika bila Shaka usingekuwa na Uhuru wa kuyazungumza haya Kama unavyofanya hapa.
 
Baada ya kufanyika kwa mchakato kwenye ngazi mbalimbali halmashauri kuu ndio imepewa mamlaka ya mwisho kufanya uteuzi wa wagombea kwa mujibu wa kifungu namba 102 ibara ndogo ya 12 g ya katiba ya CCM ya 1977 na toleo la mwaka 2017.
Changa la macho JPM kashachagua majina ya wagombea hiyo halmashauri kuu ni rubber stamp tu hawana say yeyote.
 
Makonda is dying horse, hana chake, akajiajiri kama wanavyowashaurigi vijana kwamba ni wavivu na hawapendi kujishughurisha, na uzuri Makonda hana tatizo la mtaji kama walivyo vijana wengi.
Hata akikosa ubunge inakuhusu nni?

hujui yupo katika payroll za kitengo?
 
Mbona chadema wao haikusisimua kabisa
Kwa sababu hii ni hukumu ya majambazi sugu waliotutesa kwa miaka karibu 60. Tuna hamu ya kujuwa hatima zao kama ni kitanzi au life without a possibility of parole.
 
[emoji23][emoji23] Kumbe hadi wewe hutaki RC mstaafu apite?
Hata wakina Juakali wawatu jamani na machozi yale walolia bungeni?
Kila mmoja atapitishwa kwa sifa zake zinazostahili haonewi mtu!
 
Mbona nasikia ana utajiri wa kutisha, ameupataje kama sio kwenye biashara nje ya ajira yake?
Ana utajiri gani alikuwa anapora wafanyabiashara wakihindi na waarabu.

Wewe unafikiri ile vita ya madawa ya kulevya ililenga nini ?

Kuna mhindi mmoja niliwahi kuongea nae nilisikitika sana jinsi walivyokuwa wanafanyiwa hapo Dar es salaam.

Miaka mitano iliyopita ilikuwa michungu sana kwa matajiri hapa mjini
 
Miongoni mwa Wabunge na Wawakilishi atapatikana Waziri Mkuu, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar,Mawaziri, Spika nk, hivyo ilitulazimu kuwajadili Wagombea kwa kina ili tujiridhishe tutakaowapitisha wana sifa zinazostahili kuwa Viongozi na wanafahamu Dira za Nchi na Sera za CCM



Kamati Kuu itawasilisha majina ya Wagombea iliyowapendekeza ili Wajumbe wa NEC mfanye maamuzi ya mwisho, naomba mjadili mapendekezo kwa umakini mkubwa, kwa kumtanguliza Mungu na maslahi mapana ya Taifa na CCM, tusiweke mbele Undugu, Ukanda au Udini bali uwezo wa kuongoza

Aidha Raisi Magufuli amesema kuwa hajapendelewa yeyote kwenye ugombea

Juzi na jana majina ya Wagombea yalijadiliwa kwenye vikao katika ngazi ya Kamati ya Usalama na Maadili na Kamati Kuu kwa ajili ya uchambuzi wa kina, uchambuzi ulikuwa wa kina kweli, tulitumia taarifa kutoka vyanzo vingi, niwathibitishie Wajumbe nimesoma majina yote 10,367


Uchambuzi wa kila mmoja wa kina tunao, Kamati Kuu tumejadili vizuri, hatujampendelea Mtu au kumnyima haki yake, ila ilitulazimu kutumia taarifa nyingi na kuwajadili Wagombea kwa muda mrefu ili watakaopotishwa wawe wenye uwezo wa kuipeperusha bendera ya CCM na kutupa ushindi
 
Ana utajiri gani alikuwa anapora wafanyabiashara wakihindi na waarabu.

Wewe unafikiri ile vita ya madawa ya kulevya ililenga nini ?

Kuna mhindi mmoja niliwahi kuongea nae nilisikitika sana jinsi walivyokuwa wanafanyiwa hapo Dar es salaam.

Miaka mitano iliyopita ilikuwa michungu sana kwa matajiri hapa mjini
Na bado mitano mingine
 


Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kinakutana leo chini ya Mwenyekiti wake Rais Magufuli. Miongoni mwa agenda ni kupitisha majina ya wagombea wa nafasi za Ubunge na Uwakilishi.

Mkutano utarushwa mubashara na Channel ten, TBC na ITV

Up dates;

Wajumbe wa halmashauri kuu tayari wameanza kuingia ukumbini na wengine wanajadiliana hili na lile kwa bashasha.

Mwenyekiti wa chama Dr Magufuli ameshaingia ukumbini na sasa mwenezi komredi Polepole anaelezea utaratibu.

Na sasa Katibu mkuu Dr Bashiru anazungumzia makusudi ya kikao na kwamba kikao hiki kitafanya uteuzi wa wabunge tu kwa sababu ratiba za NEC na ZEC ni tofauti.

===

Hotuba ya mwenyekiti wa CCM( - Dkt. John Pombe Magufuli)

Ameanza kwa kutoa salamu kwa wajumbe wote na viongozi mbalimbali wa chama cha Mapinduzi.

Anapenda kuwakaribisha na kuwashukuru kwa kuhudhuria mkuano mkuu na pia anawashukuru wajumbe wa NEC kwa kumpigia kura. "Napenda niwashukuru sana wajumbe wa NEC kwanza kwa jinsi mlivyonipigia kura nyingi, mlikuwa wajumbe hamkuniangusha wajumbe". Mlipokwenda kwenye maeneo yenu mlishiriki kwa upendo mkubwa sana kunitafutia wadhamini na wadhamini walipatika zaidi ya milioni moja point moja.

Nilipotuma wawakilishi kwa ajili ya kwenda kunitafutia wadhamini ili kutimiza masharti ya NEC mlikwenda na nimepata udhamini kwa mikoa mingi sana ya Tanzania bara na Zanzibar nasema hongereni sana na asanteni sana.

Wajumbe wa mkutanao na kikao hiki muhimu natambua kuwa wengine mmesafiri usiku na umbai mrefu ili kuwahi mkutano huu muhimu nasema hongereni sana hii inaonesha mnatambua umuhimu na manakipenda chama chetu.

Mkutano huu una ajenda moja kubwa kufanya uteuzi wa wagombea wa ubunge na uwakilishi kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi. Zoezi la uteuzi ndani ya chama lilianza takribani mwezi mmoja umepita na wajumbe walipiga kura na baada ya kujadiliwa na kamati mbalimbali pia wamefika kwenye mkutano huu ili pia wajadiliwe.

Napenda kuwapongeza wanachama waliojitokeza kugombea nafasi mbalimbali na walijitokeza wengi sana na hiyo ni kwa kuwa wanakipenda sana hivyo nasema hongereni sana.

Wana CCM 10367 walichukua fomu za ubunge wa majimbo na viti maalum na waliojitokeza kuwania ubunge baraza la uwakilishi ni 786 na waliojitokeza kuwania udiwani katika kata wodi na viti maalumu walikuwa 33094 kwa hiyo mytaona waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali walifika 44461 haya ni mafanikio makubwa kwa chama chetu na nafasi hizi ziliomba na watu wa kaliba na tofauti tofauti.

Katika kipindi cha miaka mitano nimekuwa nikiwaona mitembelea miradi mbalimbali na mkikemea kwa waliozembea na kutoa maelekezo mbalimabali na miradi mingi imekamilika na haya ndio matunda ya ufanyaji kazi wenu na ndio maana watu wengi wamejitokeza kuomba nafasi mbalimbali.

Juzi na jana majina ya wagombea yalijadiliwa kwenye vikao katika ngazi ya kamati ya usalama na maadili na kisha kamati kuu kwa ajli ya uchambuzi wa kina na uchambuzi wa kina kweli kweli tulitumia taarifa tulizozipata kupitia vyanzo mbalimbali na kwa yule atakayepata ufafanuzi basi atapatiwa maana nilisoma majina yote kwa kina na hatutakuwa tumempendelea mtu au kumuonea mtu .

Ilitulazimu kutumia taarifa nyingi ili atakaechaguliwa awe na uwezo wa kuipeperusha bendera na awe na uwez wa kungoza nchi yetu na hiyo ni kutokana na unyeti wa nafasi wanayogombea kwa kuwa ndiyo wawakilishi wa wananchi maana ndimo atakapopatikana waziri mkuu na viongozi wengine hivyo ilibidi tuchague mwenye sifa ya kuwa kiongozi.

Ikiwemo kupata viongozi wenye uwezo wa kuongoza, wazalendo, wenye kujitoa kwenye chama wanaofahamu mahitaji ya wananchi wanaokubalika na wananchi na na wenye utayari wa kuwatumikia wananchi na watanzania wote.

Baada ya kufanyika kwa mchakato kwenye ngazi mbalimbali halmashauri kuu ndio imepewa mamlaka ya mwisho kufanya uteuzi wa wagombea kwa mujibu wa kifungu namba 102 ibara ndogo ya 12 g ya katiba ya CCM ya 1977 na toleo la mwaka 2017.

Hapa ndiyo CCM wenyewe huwa wanavurugana na kuacha upinzani kupeta........maana kunatokea na mipasuko kwa kutojali maamuzi ya wajumbe nawote kuamua kuhamishia kura kwa mtu toka chama kingine,mwaga ugali tumwage mboga.
 
Back
Top Bottom