Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM: Majina ya walioteuliwa kuwania nafasi za Ubunge kwenye Majimbo mbalimbali nchini

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM: Majina ya walioteuliwa kuwania nafasi za Ubunge kwenye Majimbo mbalimbali nchini

Baada ya kikao cha halmashauri kuu kuketi asubuhi, Katibu mkuu mwenezi wa CCM anaongelea yaliyojiri.
=======

Polepole: Vikao vyote cha jana na leo vilikuwa chini ya mwenyekiti wa CCM. Kikao cha halmashauri kuu kilikuwa na lengo moja na limekamilika. Lengo lilikuwa kufanya uteuzi wa mwisho kwa wagomea wa majombi na viti maalum. Napenda kuleta taarifa hiyo kwenu kwa maana hawa walioteuliwa leo kwa majimbo na viti maalum.

Walijitokeza 10,367 nafasi za majimbo 264, chama chetu kimeandika rekodi na historia ya kukubalika. Upande wa uwakilishi leo haukufanyika uteuzi kwa sababu ya muingiliano wa ratiba ya NEC. Wagombea 33,094 waliomba kukiwakilisha chama cha mapinduzi kwenye udiwani ilhali nafasi zipo kama elfu nne na kitu na kufanya jumla ya watu 43,461 waliiomba kukiwakilisha chama cha mapinduzi kwenye nafasi mbalimbali.

Wajumbe wa halmashauri kuu wametimiza wajibu wao na kikao kimeeleza wajibu wao wa kusimamia serikali mpaka tumefika hapa, uamuzi walioufanya leo umezingatia watu wabobevu kusimamia maslahi ya watu wetu watakaofanya kazi sambamba na serikali ya chama cha Mapinduzi ambayo tunaenda kuiombea kura.

Kwa kauli moja wajumbe wamefanya uteuzi baada ya kupokea majina kwa watakaokuwa wagombea wa CCM kwa nafasi ya ubunge. Vilikuwepo vingezo na sifa ambazo tumezitumia ikiwemo wanaCCM wanaojitoa kwa chama, tumetafuta yule ambae atatuleta pamoja, wenye mahusiano mazuri na wananchi na wanakubalika na jamii.

Watu ambao wameteuliwa leo wanatakiwa wanatakiwa wafanye maandalizi ya msingi.

Kwenye majimbo wanaCCM ni nidhamu tuendelee kuwa watulivu, wagombea ni wengi hatuwezi kupata wote lakini nawahakikishia kwamba, chama chetu ni kikubwa na fursa zake ni nyingi tuendelee kuwa wanyenyekevu na watulivu, chama kina taarifa zenu.

ARUSHA
Arusha mijini- Mrisho Mashaka Gambo

Arumeru Magharibi- Noah Lebrus Molel

Arumeru Mashariki- John Palangyo

Karatu- Daniel Tlemai

Longido- Stephen Kirusya

Monduli- Fred Lowassa

Ngorongoro- Ole Nasha

DAR
Ubungo- Prof Kitila Kitila

Kibamba- Issa Jumanne Mtemvu

Kinondoni- Abass Tarimba

Kawe- Askofu Josephat Gwajima

Kigamboni- Dr. Faustine Ndugulile

Ilala- Mussa Zungu

Segerea- Bonna Kamoli

Ukonga- Jerry Slaa

Temeke- Doroth Kilave

Mbagala- Abdallah Chaurembo
Bashite lazima atarejea kwa mlango wa uani.... tena anaweza kurejea hapa hapa Dar kama RC. baba mtu hawezi tupa mwanae hata siku moja!

hapa anacheza na akili za Watz tu kuondoa ile dhana ya "kwa nini huyu cheti-less anapendelewa na ofisi kuu" ambayo katika kipindi hiki tunapoelekea October inaweza ikatumiwa vilivyo na mahasimu wa kisiasa wa kambi nyingine.
 
Naona Katibu mkuu akatoa angalizo waandishi wa habari watoke kabla ya kikao rasmi kuanza.

Wabakie waandishi wateule.
 
Back
Top Bottom