Yaliyojiri Kisutu, Dar: Kesi ya Freeman Mbowe, yaahirishwa hadi 13 Agosti, 2021, Mashtaka yasomwa upya

Yaliyojiri Kisutu, Dar: Kesi ya Freeman Mbowe, yaahirishwa hadi 13 Agosti, 2021, Mashtaka yasomwa upya

Unaona sasa? Hebu tulia, unasema sina msimamo? Usikurupuke kama yule mwendakuzimu, kaa kitako nikupe somo kidogo kijana. Kwa kuanzia nakiri siipendi CCM na wala sijawahi kuipenda.

Sikuipenda CCM wakati wa mfumo wa chama kimoja, niliendelea kutoipenda tulipoingia katika mfumo wa vyama vingi na siku zilivyosogea ndivyo nilivyozidi kutoipenda na hadi sasa siipendi.

Mwaka 1977 siku CCM inaasisiwa na wafanya kazi wote serikalini na kwenye mashirika ya umma kulazimika kuhudhuria vikao vya ufunguzi vya matawi maofisini, nilikataa na kuamua kuacha kazi.

Toka wakati huo hadi leo naamini kwamba adui mkubwa (nambari wani) wa taifa hili ni CCM na hakuna ubishi kwamba chama cha CCM ndicho chanzo cha matatizo yetu kama taifa tangu kuasisiwa kwake.

Ndugu yangu John7371, achana na huyo mpuuzi Stuxnet, eti anadai hana upande mnafiki mkubwa! Anadai pia kwamba eti labda mimi Mag3, naanza kumjua leo!

CCM ni chuo kinachofyatua viongozi wabovu na bahati mbaya kwa Tanzania ni kwamba kila kiongozi tunayesukumiziwa baada ya miaka kumi/mitano ni wa hovyo kuliko wa awali.

CCM wanaamini wana hatimilki ya hatma ya taifa hili lakini toka iasisiwe taifa kila siku linazidi tu kudidimia na nchi iliyojaaliwa maziwa na asali wameitafuna hadi inabaki mifupa mitupu.

Badala ya kutumia ushawishi wa sifa na uwezo kubaki madarakani hivi sasa wanatumia hila, wizi na nguvu kung'ang'ania madaraka kwa kuwatesa, kuwatesa na kuwaua wapinzani wao.

Halafu wanatokea wapuuzi kama Stuxnet ambao kwa njaa ya tumbo wako tayari kuuza utu wao na kuwapa sifa wasizostahili hawa mumiani bila kujua aliyeonja nyama ya mtu haachi.

Adui wa Tanzania ni CCM...nilisema hivyo wakati wa Mwinyi, nikasema wakati wa Mkapa, nikasema wakati wa Kikwete, nikasema wakati wa mwendakuzimu na nasema hivyo sasa.

CCM ilijengwa katika misingi ya dhulma...mali za umma (majengo, magari, viwanja na mashirika ya umma) ndizo nguzo zinazoibeba CCM. Mpaka itakapotolewa madarani taifa litaendelea kuwa kichwa cha mwenda wazimu!

Tanzania bila CCM yawezekana. Mimi naipinga CCM na kila mwenye msimamo wa kweli huyo nitamuunga mkono haijalishi ni wa chama gani...huo ndio uhusiano wangu na Chadema ambao hata ofisi zao sijawahi kukanyaga.
Nchii hii imefika hapa kwa sababu ya utawala wa kishetani wa ibilisi anayeitwa CCM. Wakati wa mwendakuzimu CCM na utawala wake wa kishetani ilifikia hatua mbaya sana. Kwa kuwa Mungu hadhihakiwi, mwendakuzimu alipopora uchaguzi wa 2020, Mungu alimuonesha kuwa hashindwi kujibu mapigo. Sasa ni juu ya chifu Hanga naye kujiangalia ili naye yasije yakamkuta. Mungu hajawahi kuwaacha waja wake waangamizwe na mashetani wa duniani pasipo kuchukua hatua.
 
Back
Top Bottom