JENERALI
Kila kilichoko chini ya ardhi na katika nchi (rasilimali ni za nani) ni za serikali au ni za wananchi? nani awe na kauli kali juu ya usimamizi wa rasimilali hizi ni nani? jamii zinazosihi karibu na rasilimali hizi zina haki gani na wajibu gani katika rasilimali hizi?
anatoa mfano wa loliondo ambako wananchi wanaonekana kuwa ndio kero kwenye rasilimali walizonazo
Vyombo vya serikali ikiwemo bunge wanapaswa kujua juu ya mikataba inayoingiwa katika nchi hii. Nasema hivi kushadidia transparency as oposed to opaque. Mfumo wa kumuachia mtu mmoja kufanya mambo mengi ni utata.
Ingekuwa vizuri kama wananchi katika maeneo yao wangechagua watawala wao, katika nafasi za kisiasa kama mkuu wa weilaya, waytu wengi hawaoni umuhimu wa nafasi kama hizi. Nafasi za polisi na nyinge waachiwe wa magogoni wateue, ila kwa swala la mtu wa kilimo n NAFASI muhimu wananchi waachiwe wachague wenyewe.
Hakuna umuhimu wa wakuu wa wilaya ila kama itaonekana na wananchi wanafaa basi wachaguliwe na wananchi na wawajaribu ili nmiaka mitano wapimwe na kama hawafai watimuliwe
Hawa nao wamelewa kama wakubwa, hawa wadogo wamelewa vijiweni na wakubwa banquet kubwa, wwanasimama mbele ya wananchi wanawaatukana na kuwaambaia hawana la kuwafanya na kama vipi wakaseme juu.
Je tunahitaji wabungfe zaidi ya 200, wakati India wanawananchi zaidi ya bilioni kadhaa, wanawabunge 500 sisi watu 40M lakini tunawabunge kibao. Sasa hivi tunamfumo koko ambao hujui ni mfume wa kiraisi au kibunge
Mwalimu aliulizwa kwa nini kateulia waziri mkuu ambae hajatajwa kwenye katiba, Mwalimu akasema haijaandikwa kwenye katiba kwamba kutakuwa n awaziri mkuu lakini pia haijasema hakutakuwa na waziri mkuu
Mijadala ya civil society izungumze juu ya utawala bora na madalaka ya umma na ni mgawanyo gani uwepo kati ya serikali kuu na serikali za mitaa
Tumesikia mara nyingi wakuu wa serikali wakionya halmahsauri msipofanya moja mbili tatu tutafuta sisi hizi halmashauri. Kwa hisyo uwepo wa halmahsauri hizi ni kwa hisani ya srikali kuu. Bila hisani hizo halmshauri hizo hazipo. Hii inatalkiwa isiwepo kwa sababu wananchi wameamua kuwa na serilkali zao za mitaa na vyombo hivyo vitakuwepo bial kujali serikali kuu ipende au ispende
Je kuna haja ya kuwa na wakuu wa wilaya na mikoa wanaoteuliwa dsm? huu ni mpangilio wa kikoloni. Gvana wa kikoloni alikuwa akikaa dsm na kuteua watu wa kwenda kusimamia na kutekeleza ukoloni wao.
Tunajua uwezo waliokuwa nao magavana ulikuwa ni katika kuwateua watu waliokuwa mahiri na wenye uwezo mkubwa sana wa kuchota mali za watanganyika na kuzipeleka nje. India na Malaysia walikuwa wakilimisha bangi, na kuuzwa china na nchi nyingine ili fedha zikipatikana waendeshe imaya zao huko india. Umahiri wao ni kuchota rasilimali zetu na hatujui wanapeleka wapi.
Sijui hawa wakuu wa wilaya wanateuliwa kwa vigezo viupi. Mana nimeona kuna alieteuliwa darasa la 7 na mwingine phd na mwingine koplo mwingine brigedia jenerali, wote wakuu wa wilaya.
Imefika mahali, ahsakum, mpaka wananchi wanajua huyu kaletwa hapa kwa kuwa ni shemeji yake fulani huko juu (ApplauseS). Zamani Mwl na Kawawa, mara nyingi walikuwa wakipeleka watu kwa kuwa ni dereva mzuri wa tanu alipewa pensheni na sio ukuu wa wilaya. Ila inapofika hata wachumba zenu ni wakuu wa wilaya sasa hapo pengine (Big applauseS)