Asisahau kumchongea Jiwe, na hapa chini ni sehemu ya Kampeni Chonganishi!!!
Ndugu zangu wa Kusini, sisi tulio kwenye system ndio tunafahamu Rais Magufuli anawachukuliaje!!
Bila kupepesa ndugu zangu, Magufuli anawadharau sana watu wa Kusini na kuwaona ni watu msiojua chochote na ndio maana ndio maana hata kuja huku HAKUTAKA kabisa kuja!!
Magufuli hakutaka kuja kwa sababu anawaona nyie ndugu zetu ni kama watu msiojitambua na msiojua chochote na kwahiyo hata asipokuja mtampigia tu kura!!
Ndo maana Magufuli hakuona taabu kumwambia Majaliwa kwamba atakuja kuwapiga makofi shangazi zake... yaani kwa jinsi Magufuli alivyowadharau, anaona anaweza kuja hapa na kuwatwanga makofi na bado mkampigia tu kura!!!
Ni kutokana na dharau zake kwenu ndo maana wala hakuona taabu kuwapora pesa zenu za korosho ili zisiendeleze Kusini, na badala yake akaziingiza Hazina ili akajengee Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kijijini kwao!!
Lakini kafanya yote hayo kwa sababu amewadharau kwa kuona pamoja na kuwapora jasho bado anaamini mtampigia tu!!!
Ndugu zangu, umbali kutoka Dar es salaam hadi Kigoma ni zaidi ya 1200KM, na umbali kutoka Dar es salaam hadi Kagera ni zaidi ya 1000KM wakati Dar es salaam hadi Lindi ni 460KM tu na Dar es salaam hadi Mtwara, ni 560KM tu!!
Lakini Magufuli kwa kuwadharau watu wa Kusini, kuja huku ameona mbali lakini Kigoma na Kagera ambako ni mbali mara mbili ya huku ameenda!!!
Yaani ameona hawezi kuopoteza muda wake kwa kusafiri kilometa 500 hadi 600 kuja kuwaomba kura zenu kwa sababu anaona hamjitambui na hapa asipokuja, mtampa tu kura!!
Sasa ngoja niwaulize ndugu zangu... Je, niwaulize?
Raia: "NDIYOOOOOOOOOOOO"
Sasa mtu anayewadharau namna hii kweli anastahili kura zenu?!
Raia "HASTAHIIIIILI!"
Tena nimekumbuka... sijui nianzie wapi manake najisikia uchungu sana!!!
Ndugu zangu wa Kusini, pale Lindi kulikuwa na mpango wa kujenga kiwanda cha kuchakata gesi ambacho thamani yake ni karibu shilingi Trillion 70!!!
Hivi mnaijua Shilingi Trillioni 70 Ndugu zangu?! Ukitaka kujua wingi wa Shilingi Trillion 70, chukua biashara zooooooote Tanzania lakini thamani yake haifiki Shilingi Trillion 70!
Uza majengo yooooote yaliyopo Dar es salaam, bila kusahau ile mighorofa, bado huwezi kupata Sh Trilioni 70!!!
Watu wooooote wa Lindi Mtwara hamfiki 3 million. Ukitaka kujua Shilingi Trilioni 70 ni nyingi kiasi gani, watu wooooote wa Lindi na Mtwara, hadi waliokopo vijijini ndani ndani huko, kila mmoja anaweza kupewa Shilingi 20 million na bado chenji ikabaki!!!!
Magufuli kwa kuwadharau watu wa kusini, akaleta mizengwe na matokeo yake kile kiwanda hadi leo hakijajengwa, na katu hakitajengwa endapo ataendelea kubaki madarakani kwa sababu anaona watu wa kusini hamstahili uwekezaji mkubwa namna hiyo!!!
Ngoja niwaulize jambo lingine!
Raia: "ULIZA BABA....."
Hivi mnadhani hii gesi iliyojaa huku Kusini ingekuwa ndo ipo Chato, mnadhani hadi sasa ingekuwa kiwanda hakijajengwa?! Amini amini, hivi sasa ingekuwa kiwanda kimeshajengwa na maghorofa ingekuwa yanajengwa kwa kasi hivi sasa kule Chato lakini kwavile gesi ipo Lindi na Mtwara Magufuli kwa makusudi ameamua kuweka mizengwe kwa sababu hapendi maendeleo yenu, anataka mbaki kuwa maskini maisha yenu yote!!
Je, hiyo ni haki ndugu zangu?!
Raia: 'HAPANAAAAAA"
Sawa sawa, sio haki hata kidogo na ndio maana mimi kwa kuwajali na kuwathamini Watanzania wote nikaapa kwamba ingawaje Tume ya Uchuguzi wamesimamisha kufanya kampeni zangu lakini SITAKUBALI kuwaacha watu wa Kusini na upweke!
Nikaapa kufanya kila niwezalo ili nije kuwajulia hali na kuwaomba kura zenu za urais, wabunge na madiwani ili hatimae mpate serikali inayowajali watu wote kwa usawa!!!
Tena ngoja niwadokeze jambo!!! Si mlimsikia anavyohangaika kuipinga sera yetu ya majimbo kwavile tulisema kila jimbo litakula kutokana na wanachozalisha?!!!
Magufuli anajua tukileta hiyo sera Watu wa Kusini ndio mtanufaika zaidi kwa sababu mna gesi yenye thamani ya mabilioni kwa mabilioni!!!!
Magufuli lazima apinge hiyo sera kwa sababu anafahamu CHADEMA tukiingia madarakani na kuanza kuchimba gesi na watu wa Lindi na Mtwara kuwa ndio wanufaika wa kwanza, basi baada ya miaka michache uchumi wa Kusini utapaa wakati yeye na CCM yake wanataka muendelee kuwa maskini!
Sijui mmemkosea nini huyu baba!!
Niendelee ndugu zangu wa Lindi/Mtwara/Kilwa/Masasi?!