Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kwenye kampeni za Mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu Mkoani Iringa

Ameandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
_____

1. Kama Tume ya Uchaguzi (NEC) ikifanya makosa, ukaikosoa lakini ukanuniwa na CHADEMA, basi una haki ya kuamini kwamba makosa ya NEC yanaagizwa na CHADEMA. Penye neno CHADEMA, waweza kuweka CCM.

2. Ukivikosoa vyombo vya dola kwa kuipendelea CHADEMA na kuionea CCM, kisha ukaona CHADEMA ndiyo inayojibu tuhuma hizo, ujue vyombo vya dola vinaagizwa na CHADEMA. Penye jina CHADEMA, waweza kuweka CCM.

3. Ukiona wagombea wengi wa CCM wameenguliwa, wakati wagombea wote wa CHADEMA wameteuliwa, una haki ya kuamini kuwa fomu zote za wagombea wa CHADEMA ZILIJAZWA na Tume ya Uchaguzi (NEC). Penye jina CHADEMA waweza kuweka CCM.

4. Ukiona wagombea wengi wa CHADEMA wamepitishwa bila kupingwa na bado wanaendelea na jitihada za kushawishi wagombea wa CCM wajitoe, huku wakiorodhesha na kununua shahada za kupigia kura, una haki ya kuamini kuwa CHADEMA hawana Imani na sanduku la kura. Penye jina CHADEMA waweza kuweka CCM.

5. CHADEMA wanapenda Sana Amani. CCM wanapenda Sana Haki. Siku CHADEMA wakipenda Haki na CCM wakapenda Amani ndipo tutapata Tume HURU ya Uchaguzi. Penye jina CHADEMA waweza kubadili na kuweka CCM bila kupoteza maana ya fungu hili.!
 
Acha taarabu mtoto wa kiume kisa Yesu feki wa Lugola
Wewe kwa sababu unapenda taarabu ndio maana unaona hicho nilichokieleza ni taarabu,ila nimeeleza ukweli kama usingekuwa msimamo usioteteleka wa Magufuli kwenye suala la kuhusu corona basi hata hizi kampeni za kusifia mafuriko/nyomi zisingekuwepo.
 
Hakuna Chama Chenye Sera Nzuri na za uhakika kama Chadema!! Nasema hili wazi na kukiri waziwazi
 
Kwa Lukuvi hapati kitu anaenda tu kutalii
Mlianza zamani kukomkesa kila kitu lakini bado mnaumia sana kumuona watu wanaimani nae.

Hivi si ulisema akitua tu moja kwa moja mpaka jela au ushasahau?


Basi kujinasibu kwenu kwakujiona kila kitu mnakijua na mipango kibao michafu ya kumfanyia usisahau kuna Mola ambaye nimpangaji kuliko nyinyi.
 
Hivi naachaje kumchagua Lissu wakati ana Sera ya kumsomesha hata mwanangu ambaye nimemsomesha private???

Hivi naachaje kumchagua Lissu ambae anarudisha makato ya mikopo ya bodi ya mikopo kutoka asilimia 15 ya magufuli hadi asilimia 6???

Hivi naachaje kumchagua Lissu ambaye ametoa Sera ya kunijali mimi mlipa kodi na mfanyabiashara kwa kuniwekea mswada wa kunilinda mimi mlipa kodi ili TRA wasininyanyase????

Hivi naachaje kumchagua Tundu Lissu ambaye hataniwekea mipaka kwenye masoko ya kuuza mazao yangu niliyoyalima kwa jasho kubwa????

Hivi naachaje kumchagua Tundu Lissu mwenye Sera ya kurudisha katiba mpya ya warioba itakayoweka misingi ya utawala bora na kuondoa matumizi mabaya ya madaraka?
 
Ni kweli wapenda amani hawatakipigia kura CHADEMA ila wapenda haki ambao ni watanzania wengi watakipigia kura
 
Huu utamaduni ulianzia CUF, baadaye imekuwa kawaida kwa CCM sasa Chadema nao wameingia! Mungu apishie mbali lkn nadhani polisi wawe na ujasiri wa kuzuia hili, inaweza kutokea ajali na badala ya kampeni tukaanza maombolezo.

Vv
Hii picha ni ya 2015, CHADEMA hawatumii lori kubeba wanachama wao tofauti na gari la matangazo tu.
 
Ni kweli wapenda amani hawatakipigia kura CHADEMA ila wapenda haki ambao ni watanzania wengi watakipigia kura

Unasema wapenda haki, Ndani ya CHADEMA kwenyewe hakuna haki. Ni unyanyasaji mtupu. Kila anayetofautiana na Mbowe a akipata cha mtema kuni. Wabunge wazuri, mahiri, wote wametimka sababu ya kutofautiana na Mbowe. Wamebaki wale wa Ndiyo Mzee. CHADEMA wasafishe kwanza uchafu uliomo ndani mwao kabla hawajaona uliopo kwingine.
 
Ni wabunge wapi mahiri wametimka chadema ?

Nani aliwahi kunyimwa haki yake CHADEMA?

Inamaana wewe unasupport uvunjifu wa haki za msingi kwa wananchi na utawala wa ccm simply CHADEMA nako kuna uozo ?

Hizi akili huwa mnazitoa wapi ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…