Ameandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
_____
1. Kama Tume ya Uchaguzi (NEC) ikifanya makosa, ukaikosoa lakini ukanuniwa na CHADEMA, basi una haki ya kuamini kwamba makosa ya NEC yanaagizwa na CHADEMA. Penye neno CHADEMA, waweza kuweka CCM.
2. Ukivikosoa vyombo vya dola kwa kuipendelea CHADEMA na kuionea CCM, kisha ukaona CHADEMA ndiyo inayojibu tuhuma hizo, ujue vyombo vya dola vinaagizwa na CHADEMA. Penye jina CHADEMA, waweza kuweka CCM.
3. Ukiona wagombea wengi wa CCM wameenguliwa, wakati wagombea wote wa CHADEMA wameteuliwa, una haki ya kuamini kuwa fomu zote za wagombea wa CHADEMA ZILIJAZWA na Tume ya Uchaguzi (NEC). Penye jina CHADEMA waweza kuweka CCM.
4. Ukiona wagombea wengi wa CHADEMA wamepitishwa bila kupingwa na bado wanaendelea na jitihada za kushawishi wagombea wa CCM wajitoe, huku wakiorodhesha na kununua shahada za kupigia kura, una haki ya kuamini kuwa CHADEMA hawana Imani na sanduku la kura. Penye jina CHADEMA waweza kuweka CCM.
5. CHADEMA wanapenda Sana Amani. CCM wanapenda Sana Haki. Siku CHADEMA wakipenda Haki na CCM wakapenda Amani ndipo tutapata Tume HURU ya Uchaguzi. Penye jina CHADEMA waweza kubadili na kuweka CCM bila kupoteza maana ya fungu hili.!