Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kwenye kampeni za Mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu Mkoani Iringa

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kwenye kampeni za Mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu Mkoani Iringa

Ameandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
_____

1. Kama Tume ya Uchaguzi (NEC) ikifanya makosa, ukaikosoa lakini ukanuniwa na CHADEMA, basi una haki ya kuamini kwamba makosa ya NEC yanaagizwa na CHADEMA. Penye neno CHADEMA, waweza kuweka CCM.

2. Ukivikosoa vyombo vya dola kwa kuipendelea CHADEMA na kuionea CCM, kisha ukaona CHADEMA ndiyo inayojibu tuhuma hizo, ujue vyombo vya dola vinaagizwa na CHADEMA. Penye jina CHADEMA, waweza kuweka CCM.

3. Ukiona wagombea wengi wa CCM wameenguliwa, wakati wagombea wote wa CHADEMA wameteuliwa, una haki ya kuamini kuwa fomu zote za wagombea wa CHADEMA ZILIJAZWA na Tume ya Uchaguzi (NEC). Penye jina CHADEMA waweza kuweka CCM.

4. Ukiona wagombea wengi wa CHADEMA wamepitishwa bila kupingwa na bado wanaendelea na jitihada za kushawishi wagombea wa CCM wajitoe, huku wakiorodhesha na kununua shahada za kupigia kura, una haki ya kuamini kuwa CHADEMA hawana Imani na sanduku la kura. Penye jina CHADEMA waweza kuweka CCM.

5. CHADEMA wanapenda Sana Amani. CCM wanapenda Sana Haki. Siku CHADEMA wakipenda Haki na CCM wakapenda Amani ndipo tutapata Tume HURU ya Uchaguzi. Penye jina CHADEMA waweza kubadili na kuweka CCM bila kupoteza maana ya fungu hili.!
 
Acha taarabu mtoto wa kiume kisa Yesu feki wa Lugola
Wewe kwa sababu unapenda taarabu ndio maana unaona hicho nilichokieleza ni taarabu,ila nimeeleza ukweli kama usingekuwa msimamo usioteteleka wa Magufuli kwenye suala la kuhusu corona basi hata hizi kampeni za kusifia mafuriko/nyomi zisingekuwepo.
 
Mgombea Urais wa Chadema anafanya kampeni kata kwa kata. Usikose kuyasikia madini ya Lissu, leo kata ya Isman.

=====

"Mafurikoo Ya Wananchi Wa Iringa Kwenye Viwanja Vya Mwembe Togwa KatiKati Ya Mji Wa Iringa.


Mheshimiwa Tundu Lissu Akiwa Jukwaa Amenadi Sera Zifuatazo...

1. Itakuwa Jambo La Neema Na Afya Kama Wagombea Wawili Wakubwa Wakikutanishwa Kwenye Mdahalo Utakaorushwa Na Vyombo Vyote Vya Habari, Leo Naomba Nitoe Rai Kwake Kwa Raisi Magufuli Tukutane Kwenye Mdahalo Huo.

2. Uchaguzi Uliopita Tulisema Tutaanzisha Elimu Bora Bure, Lakini Raisi Magufuli Alipoingia Madarakani Akaanzisha Elimu Bure, Kwa Maana Watoto Wetu wanaToka Mashuleni Wakiwa Bure, Yaan Hawana Maarifa. Basi Tunasema Na Kuhusu BIMA Ya Afya Na Wanadandia. Kama walivyokuwa Buree Kwenye Elimu Basi Na Kwenye Afya Napo Itakuwa Bureee.

3. Kuengua Engua, Wagombea 55 Walienguliwa, Na KatiKa Mkoa Wa Morogoro Majimbo 8 Wamewaengua Wagombea 5, Hivyo Ni Wazi Kabisa CCM na Magufuli Hawawezi Hushindani. CCM Imefilisika Kiasi Hicho.. Wenzetu Kwenye Mikutano Yao Lazima Abebe Watu kwenye Mabasi.

Leo Tuongelee Kuhusu Elimu Ya Juu, Mimi Na Wenzangu Pamoja Na Raisi Magufuli Tulisoma Elimu Ya Juu Kwa Kodi Za Wananchi. Lakini Leo Ona Vijana Wetu Wengi Wanakosa Haki Yakusoma Elimu Ya Juu. Vijana Wetu Wanakosa Haki yakupata Mikopo Sababu Wazazi Wao Waliowasomesha Kwenye Shule Binafsi. Ubaguzi Wakutoa Mikopo Unakosesha Vijana Wetu Haki Yakupata Elimu.

Ulipaji Wa Mikopo Umekuwa Tatizo Na Kandamizi Kwa Vijana Wetu, Zamani Ilikuwa Ukipata Kazi Unalipa 3% Lakini Leo Wamebadilisha Sheria Na Wanawakata 15% Ambapo Imekuwa Ni Mzigo Mkubwa Kwao, Serikali Ya Chadema Ikiingia Madarakani Itarudisha Sheria Ya Zamani Ya 3%.

Serikali ya Chadema Ikiingia Madarakani Itaweka Wanachi Wote Wawe Kwenye Mfuko Wa Jamii, Sababu Watu Wote Tunazeeka NA Watu Wote Tunapata Matatizo.

Tanzania Inareserve Kubwa Ya Gesi Kwenye Bahari Ya Hindi, Tanzania Imekuwa Nchi Ya Tatu Afrika Kuwa Nakiasi Kikubwa cha Gesi, Na Ndo Hapo Tutakapotokea Watanzania. Serikali Ya Chadema Inasema Utafiti Na Uendelezwaji Gesi Ulioanzishwa nA Jakaya Kikwete Tutarudisha Mchakato Uendelee, Ambapo Kwa Sasa Umesimama na Wawekezaji Wameenda Nchi Jirani. Kwahyo Sasa Jibu Ni Tutengeneze Uchumi Kwenye Gesi.

Serikali Ya Magufuli Wameifuja Mifuko Ya Jamii, Pesa Za Wafanyakazi Zimetumiaka Kwa mambo Ambayo Hayana Mahusiano Na Wafanyakazi. Walipoona Mambo Magumu Wakaleta Kikokotoo Cha Ajabu. Leo Kuna Wastaafu Hawajalipwa Mpaka Leo. Ufujaji Wa Mifuko Ya Jamii Unamuumiza Kila Mtu, Hivyo Basi Ni Tarehe 28 Piga Kura Ya Ndio Kwann Wagombea WaChadema Tuchukue Nchi Tuondoke Na Hizi Mambo.

Mwisho, Mahusiano Mabaya Na Nchi Jirani Umesababisha Kutokuwa Na Mahusiano Mazuri Kibiashara.
View attachment 1568937View attachment 1568939
View attachment 1568974View attachment 1568941
View attachment 1568946
View attachment 1568969
View attachment 1568950View attachment 1568967
View attachment 1568960View attachment 1568953

Hakuna Chama Chenye Sera Nzuri na za uhakika kama Chadema!! Nasema hili wazi na kukiri waziwazi
 
Kwa Lukuvi hapati kitu anaenda tu kutalii
Mlianza zamani kukomkesa kila kitu lakini bado mnaumia sana kumuona watu wanaimani nae.

Hivi si ulisema akitua tu moja kwa moja mpaka jela au ushasahau?


Basi kujinasibu kwenu kwakujiona kila kitu mnakijua na mipango kibao michafu ya kumfanyia usisahau kuna Mola ambaye nimpangaji kuliko nyinyi.
 
Hivi naachaje kumchagua Lissu wakati ana Sera ya kumsomesha hata mwanangu ambaye nimemsomesha private???

Hivi naachaje kumchagua Lissu ambae anarudisha makato ya mikopo ya bodi ya mikopo kutoka asilimia 15 ya magufuli hadi asilimia 6???

Hivi naachaje kumchagua Lissu ambaye ametoa Sera ya kunijali mimi mlipa kodi na mfanyabiashara kwa kuniwekea mswada wa kunilinda mimi mlipa kodi ili TRA wasininyanyase????

Hivi naachaje kumchagua Tundu Lissu ambaye hataniwekea mipaka kwenye masoko ya kuuza mazao yangu niliyoyalima kwa jasho kubwa????

Hivi naachaje kumchagua Tundu Lissu mwenye Sera ya kurudisha katiba mpya ya warioba itakayoweka misingi ya utawala bora na kuondoa matumizi mabaya ya madaraka?
 
Kipindi cha Dr Slaha ilikuwa heshima sana kushabikia CHADEMA, na ilikuwa aibu kuizungumzia CCM. Sasa hivi ni aibu sana mara 1000 kuishabikia CHADEMA. CHADEMA wamekuwa wanaharakati, sio chama cha siasa. Kipindi kile ilikuwa raha kusikiliza sera zao, lkn leo sera ni matusi, kashifa, kejeri, vurugu, nk. Kimsingi Lissu ameharibu chama. Wapenda amani hawawezi kukipigia kura CHADEMA. Najua mtapinga lakini ndo ukweli na ukweli utabaki kuwa ukweli.
Ni kweli wapenda amani hawatakipigia kura CHADEMA ila wapenda haki ambao ni watanzania wengi watakipigia kura
 
Huu utamaduni ulianzia CUF, baadaye imekuwa kawaida kwa CCM sasa Chadema nao wameingia! Mungu apishie mbali lkn nadhani polisi wawe na ujasiri wa kuzuia hili, inaweza kutokea ajali na badala ya kampeni tukaanza maombolezo.

Vv
Hii picha ni ya 2015, CHADEMA hawatumii lori kubeba wanachama wao tofauti na gari la matangazo tu.
 
Ni kweli wapenda amani hawatakipigia kura CHADEMA ila wapenda haki ambao ni watanzania wengi watakipigia kura

Unasema wapenda haki, Ndani ya CHADEMA kwenyewe hakuna haki. Ni unyanyasaji mtupu. Kila anayetofautiana na Mbowe a akipata cha mtema kuni. Wabunge wazuri, mahiri, wote wametimka sababu ya kutofautiana na Mbowe. Wamebaki wale wa Ndiyo Mzee. CHADEMA wasafishe kwanza uchafu uliomo ndani mwao kabla hawajaona uliopo kwingine.
 
Unasema wapenda haki, Ndani ya CHADEMA kwenyewe hakuna haki. Ni unyanyasaji mtupu. Kila anayetofautiana na Mbowe a akipata cha mtema kuni. Wabunge wazuri, mahiri, wote wametimka sababu ya kutofautiana na Mbowe. Wamebaki wale wa Ndiyo Mzee. CHADEMA wasafishe kwanza uchafu uliomo ndani mwao kabla hawajaona uliopo kwingine.
Ni wabunge wapi mahiri wametimka chadema ?

Nani aliwahi kunyimwa haki yake CHADEMA?

Inamaana wewe unasupport uvunjifu wa haki za msingi kwa wananchi na utawala wa ccm simply CHADEMA nako kuna uozo ?

Hizi akili huwa mnazitoa wapi ?
 
Back
Top Bottom