Lissu karibu sana Tabara kwetu, wanyamwezi ni watu wakarimu mno..... hapa ndipo chimbuko la wapigania haki na demokrasia ya kweli walitokea hapa....
Kijiji cha Ipole Sikonge ndipo alipozaliwa na kuzikwa Mwanamapinduzi nguli... Oscar Kasangatumbo (R.IP) ambaye alikuwa miongoni mwa waasisi wa mageuzi nchini 1992 kwa kuanzisha chama cha UMD na wapigania demokrasia ya kweli tangu enzi za Mwalimu.
Alipata misukosuko mingi sana, kunyanganwa passport, kuibiwa ngombe zake zote na kuwa grounded kwamba asitoke nje ya mji wa Tabora bila idhini ya IKULU baada ya kutuhumiwa kupinga SERA za TANU za ukandamizaji wa uhuru wa kidemodrasia.
Karibu sana, Tabora ndiyo ilipo mizizi wa siasa za Upinzani na watetezi wa haki za binadamu - Tanzania.
Jioni waambie wenyeji hapo wakupatie Ugali na mboga ya nsansa iliyoungwa kwa tui la karanga.... chakua hiki huwa ni speical kwa wageni maalum kama wewe.
Karibu tena Tabora - Rais wetu.