Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Mbowe na Wenzake: Shahidi Afred Kapala wa tiGO atoa Ushahidi, Kesi kuendelea, Nov 03, 2021

Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Mbowe na Wenzake: Shahidi Afred Kapala wa tiGO atoa Ushahidi, Kesi kuendelea, Nov 03, 2021

Wakili wa Serikali: Unakumbuka Ilikuwa ni wakati gani?

Shahidi: (Tigo) walitaka Taarifa za mihamala ya Fedha kutoka 01 June ya 2020 Mpaka 31 June ya 2020 Nikaingia Kwenye Computer Nikaziona

Bla bla bla bla bla bla bla bla .....

Wakili wa Serikali:Shahidi tufafanulie Maneno Ya Juu kama Sender Maana yake nini

Shahidi (Tigo): Send My Op namba 0719933386 Receiver 0787555200 Miamala wa Tarehe 20 Kiasi 500,0000 Tarehe 20 July 2020 Saa 2 na Dakika 21na Balance Ilikuwa 2.3M
Hivi kuna 31 ya June kweli? au mie ndie sielewi?
 
Hivi mbona mnataka kulaumu kila mtu? Mlitaka huyu Legal Officer akatae kweli kutoa taarifa alizoombwa? Kuna sehemu amesema uongo mpaka sasa? Ungekuwa wewe ndiyo mwajiriwa wa Tigo kwa nafasi hiyo na umetakiwa kwenda kutoa ushahidi ungekataa? Hebu tuacheni kusukuma lawama kwa kila mtu.
Ana ukweli gani njaa tupu inamsumbua.
 
Shahidi wa leo naye ni mwanasheria, sasa kama alikua anaona wenzake waliomtangulia wanakosea kwasababu hawajasomea sheria ngoja asubiri zamu yake, kibatala anamlia karanga
Tena kheri asingesema ni mwanasheria..Leo ni leo ..naona muda huu na mkewe anamsikiliza mume wake eskariot akiwa mahakamani ili hela wazigawane vzr
 
Unataka kuwalaumu bure MIC,ulitaka wafanyeje kama wameombwa watoe hizo taarifa tena kwa barua rasmi kutoka Taasisi inayoruhusiwa kisheria kupewa hizo taarifa? Mbona Makampuni karibu yote yanafanya hivyo,pindi yanapotakiwa kutoa taarifa kwa Taasisi zinazoruhusiwa kisheria.Hakuna Kampuni yoyote hapa Nchini itakataa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi,Mahakama na TRA.
Jamii forum tu ndiyo wanauwezo huo wa kumtetea member wao kutoka kwenye uonevu
 
Hivi mbona mnataka kulaumu kila mtu? Mlitaka huyu Legal Officer akatae kweli kutoa taarifa alizoombwa? Kuna sehemu amesema uongo mpaka sasa? Ungekuwa wewe ndiyo mwajiriwa wa Tigo kwa nafasi hiyo na umetakiwa kwenda kutoa ushahidi ungekataa? Hebu tuacheni kusukuma lawama kwa kila mtu.
Kampuni lakini wategemee kupungua kwa wateja
 
Kwenye nchi zetu sie mazwazwa na misukule ya CCM ndipo hizi Sheria zinafanya kazi.

Kwa wanaojielewa huu u$3ng3 haupo..

Kampuni kama apple FBI waliomba taarifa hawakupewa, just imagine FBI hawakupewa taarifa...

Mtandao kama twitter unamfungia raisi DTrump account...

Haipaswi kampuni yeyote Kutoa taarifa za mteja bila idhini yake...

Na hii michezo hata ukifahamiana tu na hao IT wa hizi kampuni, ukiomba tu taarifa za mtu fulani hata mkeo Wana print zoooteee...

Watu wanashindwa kuelewa kwanini tunamlaani mwendazake...

Enzi za utawala wake aliwanyanyasa sana wapinzani pamoja na wananchi waliokuwa wakishirikiana nao katika mambo mbalimbali ya kijamii....

Kwa mhe. Mbowe hali ilikuwa mbaya sana...
Akinunua hata shati dukani kwako akaonekana na wambea wa ccm, TRA watakutwanga kodi mpaka ufilisike!
Akila chakula kwenye mgahawa wako (akaonekana na wambea wa ccm), TRA watakumaliza!
Yani ilikuwa shida tupu, kwenye vikao vya ccm mkoa na wilaya unamsikia mwenyekiti anasema 'flani si anajifanya mbishi, umeona kitu tumemfanyia?" Hii iliwaumiza sana hata baadhi ya wanaccm wenye ubin-adam waliokua vikaoni.
Ewe Lucifer, umgeuzegeuze huyo karagosi aive kotekote kama mshikaki wa fillet!!!
 
Ikiwa leo ni tarehe 2 November 2021 , kesi hii inayobeba sehemu kubwa ya habari za Tanzania inaendelea tena Mahakamani hapo .

Baada ya ushahidi wa Muuza Mbege wa Rau Kukamilika , Leo upande wa Jamhuri utaleta shahidi wa Tano miongoni mwa wale 24 waliopangwa kutoa ushahidi huo .

Kama kawaida JF itakuletea moja kwa moja kesi hii kutoka Mahakamani , usiondoke .

===========

Jaji ameingia Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe Imeshatajwa

Wakili wa Serikali Robert Kidando Anatambulisha

1.Pius Hilla
2.Nassoro Katuga
3,Abdallah Chavula
4.Ester Martin
5.Jenitreza Kitali
6.Tulimanywa Majige

Kibatala anatambulisha Jopo lake

1. Michael Mwangasa
2.Seleman Matauka
3.Nashon Nkungu
4.Alex Massaba
5.Michael Lugina
6.Maria Mushi
7.Hadija Aron
8.Dickson Matata
9.Jonathan Mndeme
10.Fredrick Kihwelo
11. John Malya

Jaji Mashtakiwa 1,2,3 na 4 Wananyanyuka kuashiria uwepo wao

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Tunashahidi Mmoja Kwa Leo Lakini Kabla ya Kuendelea Leo tuna ombi, Na Maombi yetu yatamuhusu Shahidi Wa Leo Mheshimiwa

Jaji: Wakati wa Kufile Mashahidi tuliorodhesha Majina Kama Frank Kapala

Jaji: Ndiyo

Wakili wa Serikali: na Kule Kwenye Comito Proceedings Katika Ukusara wa 32 wa zile proceeding za Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu zilitaja Kama Frank Kapala Lakin kama tulivyo leta information Barua ya 11 August 2021 Ndiyo alitaja kama Frank Kapala Mheshimiwa Jaji Kwa Usahihi ....Shahidi huyu anaitwa Frank kapara.

Wakili wa serikali: Kwa hiyo tunaomba Kumbukumbu sahihi za Mahakama zi-note kama Frank Kapara Kwa kifungu 264 Sura ya 20 cha CPA Rev Ya 2009 Na Kwa sababu Ushahidi wa Shahidi huyu ulisomwa wakati wa Comito Proceedings tunaomba turuhusiwe Kuendelea na Shahidi huyu.

Jaji: Kifungu gani?

Wakili wa Serikali: 264 Sura ya 20 kama Ilivyofanyiwa marekebisho Mwaka 2009

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Maombi yetu ni hayo tu

Mtobesya: Tumesikia Maombi ya Upande wa Mashitaka na Kwa sababu Wanasema Substance ndiyo Iliyo contain Ushahidi Wake tangu Maelezo yake Polisi. Kwa Upande wetu hatuoni Kama inaathiri Haki za Mteja wetu, Hatupingi hilo Ombi Kwa niaba ya Mshitakiwa Wa Kwanza, Asante.

Wakili John Mallya: Kwa niaba ya Mshitakiwa wa Pili hatuna Pingamizi.

Wakili Fredrick Kihwelo: hatuna Pingamizi Kwa Niaba ya Mshitakiwa wa tatu.

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi Kwakuwa wameleta Maombi Rasmi.

Jaji: Samahani Kidogo, Unachotaka Kirekebishwe Unaweza Ku-Spell

Wakili wa Serikali: FREDY KAPALA

Jaji: Basi maombi ambayo yameletwa Kurekebisha Kumbukumbu za Mahakama Kuwa Shahidi alikuwa Frank Kampala na Sasa atafahamika kuwa ni FREDY Kapala Na hiyo ndiyo Itakuwa kumbukumbu Mpya ya Mahakama, NATOA AMRI. Mawakili wote Wananyuka na Kukubaliana na Jaji.

JAJI: Shahidi aletwe sasa

Wakili wa Serikali: Ameenda Kuitwa

Jaji: Anakuwa Shahidi Wa Ngapi huyo

Wakili wa Serikali: Shahidi 05

Jaji: Utetezi Ndiyo..?

Kibatala: Ndiyo

Jaji: Majina yako

Shahidi: Naitwa Afredy Kapala

Jaji: Umri

Shahidi: 38yr

Jaji: kabila

Shahidi: Mpare

Jaji: Shughuli yako

Shahidi: Nimeajiriwa na kampuni ya Tigo

Jaji: Dini yako

Shahidi: Mkristo

Shahidi: Naapa Mbele ya Mahakama hii kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa ni Kweli, kweli tupu Eenheeeee Mwenyezi Mungu nisaidie.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Wakili Nasorro Katuga atamuongoza

Wakili wa Serikali Nasorro: Nitakuuliza Maswali

Wakili wa Serikali: Umesema Unashughulika na nini?

Shahidi: Nimeajiriwa na kampuni ya kibiashara inaitwa TIGO

Wakili wa Serikali: Kwanini Unasema Kampuni ya kibiashara

Shahidi: Kwa sababu kampuni iliyosainiwa Brela ni MIC Tanzania

Wakili wa Serikali: Jina la Kibiashara ndiyo

Shahidi: Tigo

Wakili wa Serikali: Kampuni ya MIC Tanzania Ltd Inafanya Shughuli gani?

Shahidi: Mawasiliano ya Simu pamoja na Mihamala ya Kifedha

Wakili wa Serikali: Mwambie Mheshimiwa Jaji Umeajiriwa lini

Shahidi: March Mwaka 2012

Wakili wa Serikali: Umeajiriwa kama nani?

Shahidi: Kama Mwanasheria wa Tigo

Wakili wa Serikali: Katika Kitengo Kipi

Shahidi: Kitengo cha Sheria

Wakili wa Serikali: Umesema Kampuni yako inajishughulisha Kutoa Mawasiliano ya Simu na Mihamala ya kifedha Iambie Mahakama kwa nani?

Shahidi: Kwa Wateja Ambao wanamiliki line za Mitandao ya Simu

Wakili wa Serikali: Hawa wateja Wa Tigo Wanapatikana Vipi?

Shahidi: Wanapatikana Kwa Kununua line za Tigo na Wakaitumia basi Wanakuwa Wateja wetu. Na ili ifanye kazi lazima ifanyiwe Usajili.

Wakili wa Serikali: Kwenye Kusajili mnasajili Kitu gani?

Shahidi: Kwa mtu ambaye ana kitambukisho cha NIDA tunatumia NATIONAL IDENTIFICATION NUMBER. Mtu anaye sajili ataingiza Namba ya Kitambulisho Cha Taifa Itasoma Taarifa.

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama process za Manunuzi ya Line kama zipo?

Shahidi: Mtu yoyote anaweza Kufika kwenye Duka au sehemu ambayo kuna Wakala anauza hizo line za Tigo akiwa na Kitambulisho Cha Taifa, Lakini pia Kuna Wageni ambao wanatakiwa kutumia passport....

Wakili wa Serikali: Mtu anaye jua atafanya nini?

Shahidi: Ataweke Kidole Kigumba, Zitasoma Taarifa zote ambazo zipo Kwenye NIDA, Kama Jina Na tarehe ya kuzaliwa Kwa hiyo Taarifa hiyo itachukuliwa Na kuhifadhiwa Kwenye Mfumo wa Tigo kama Taarifa za Owner au Mtumiaji wa hiyo line.

Wakili wa Serikali: Mtu asiyejua NIDA, unaposema Zinaenda Kutally na Taarifa za NIDA unamaanisha Nini?

Shahidi: NIDA nimfumo wa Usajili wa Vitambulisho Vya Taifa ambao unatunzwa na Authority

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama unaposema Taarifa zile zitachukukiwa na Kuhifadhiwa Tigo, Nani atazichukua

Shahidi: Tunasema Ki Electronic kuna Mfumo wetu ikizipata na Ikatally inatunza Kwetu, Kwa hiyo Mifumo inawasiliana

Wakili wa Serikali: Jinsi ya Kusajili line Taratibu ziko Vipi

Shahidi: Ukishanunua Laini na Kwamba wewe sasa Unawasiliana, Tuna kutumia Meseji Kuwa kama Unataka Kutumia huduma ya Mihamala ya Fedha, Ukisema Okey tunakupa Vigezo na Masharti.

Wakili wa Serikali: Hiko Kitendo Mnakiitaje?

Shahidi: Umejiregister Kwenye Huduma ya Tigopesa

Wakili wa Serikali: Nikurudiahe kwako sasa wewe Mwenyewe, Tigo Umeajiriwa kama Mwanasheria Je Majukumu yako ni Yapi

Shahidi: Kushauri Viongozi Maswala Yanayohusu Sheria, Kutengeneza Kusoma, kupitia na Kusaini Mikataba Kufuatilia, Kusimamia Kesi zote zinazohusiana na Tigo ...Kumsaidia VYOMBO Vya Ulinzi na Usalama Katika Kupata Taarifa Mbalimbali Kutoka kwa Wateja zinapohitajika.

Wakili wa Serikali: Jingine, Baada ya kutoa hizo Taarifa

Shahidi: Kama Kuna Jinsi Yoyote Kusaidia Chombo chochote Katika Kutafuta Taarifa, Naweza Kusaidia Siyo VYOMBO Vya Ulinzi na Usalama tu Bali hata Mtu Binafsi anaweza kupata Msaada wangu.

Wakili wa Serikali: Ni Vipi Mtu Binafsi, Mtu X anaweza kupata Taarifa za Mtu Y

Shahidi: Mtu Mmoja Kupata Taarifa za mtu Mwingine HAIWEZEKANI

Wakili wa Serikali: Kwa mujukumu hayo uliyoyataja, Unamajukumu gani au Ujuzi gani inayo Kusaidia katika Kutekeleza Majukumu yako

Shahidi: Kama Mwanasheria wa kampuni Nina Digrii ya Sheria, Nimesomea India JSS law college. Under MYSORI University, Ambayo niliipata 2009 Nilisoma Pia Advanced Computer Course, MYSORI University India 2007. Nilisoma Pia Advanced Diploma in Practice Nilimaliza Mwaka 2012 Baada ya hapo Kuna Training mbalimbali ambazo Nimezipata Nikiwa kazini 2012 nilipoanza Kazi

Wakili wa Serikali: Zitaje Training gani

Shahidi: Nilipopata kazi ilikuwa ni Majukumu yangu Nilikuwa nimeingia Kampuni ya Telecom Nilipata Training Ya Mwezi na nusu

Wakili wa Serikali: Ulisomea nini ktk hiyo Training

Shahidi: Mifumo ya Kujifunza Kutumia, ilikupata Taarifa Wa kwanza ni oracle Wa Kusaidia Kupata Taarifa mbalimbali zilizopo Sehemu za Kazi.

Shahidi: Kuna system Nyingine ambayo CONVIVER iliyokuwa Inasaidia Kupata Mihamala Yote ni soft ware BILL QUERY Iilikuwq Inasaidia Kujua matumizi Mbalimbali ya Mteja Upande wa Vocha Na SMAP ni Mfumo Sawa QUERY Kwa hiyo nilikuwa nasaidia VYOMBO Vya Ulinzi Na Usalama Kupata ...Information

Wakili wa Serikali: Unaweza Kukumbuka Ulikuwa unafanyiwa na nani

Shahidi: Ofisini na Mtu anaitwa Mr.....

Wakili wa Serikali: Ofisi za Tigo ziko wapi

Shahidi: Ofisi za Tigo Zipo Makumbusho DERM COMPLEX

Wakili wa Serikali: Unakumbuka Training Nyingine

Shahidi: 2015 palikuwa na Training Nyingine Baada ya Mifumo Kubadilika Baada ya oracle ikaja SQL Server CONVIVER ikaja Kubadirishwa Ikaja TELVIVER IKAJA ENVIVER ambayo sasa Ikaja Information Mbayo Ukiingia Unaona Matumizi ...na Kila Kitu. Wanakufundisha Kule Unakoenda Kuchukua zile Information Siyo Kila amtu anaruhusiwa Kwenda Kuchukua Unafundishwa Jinsi gani ya Kuzilinda.

Wakili wa Serikali: Baada ya Mifumo Kubadilika sasa

Shahidi: Ikabidi tupate Training, Jinsi zinavyofanya kazi na Tabia zake

Wakili wa Serikali: Katika Training zako ulipata Lolote Kuhusiana na Information ambazo unaenda kufanyia Kazi

Shahidi: Wanakufundisha General Overview

Wakili wa Serikali: Umetaja Training za 2012 na 2015 Je una Training Nyingine

Shahidi: Zipo Nyingine hizo ni Major Kila Siku Dunia Ikileta System Mpya tutaambiwa tu Kuna Training za Kila Siku Katika Majukumu ya kazi

Wakili wa Serikali: Nikurudishe Nyuma Wakati Unataja Majukumu Yako Unasema Unasaidia VYOMBO Vya Ulinzi na Usalama. Je Ni VYOMBO gani

Shahidi: VYOMBO Vyote Vya Usalama Ukijumlisha Polisi, Jeshi, Kama ni Anga kama ni Ardhi na VYOMBO Vyote Vinavyofanya Uchunguzi wa Kisayansi. 2.Taarifa za Mihamala ya Fedha, Kutuma na Kupokea fedha 3. Kuna Recharge ya Vocha na Kutumia pamoja na Matumizi yake 4. Taarifa za Usajili 5. Taarifa Nyingine zote zinazoambatana Kama NIDA, LOCATIONS, BILL MBALIMBALI ANAZOLIPA

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama sasa Unawasaidia Kuwapa Taarifa, Je ni Taarifa zipi Mnawapa, ulikuwa unatumia Neno zinazoruhusiwa Kisheria

Shahidi: Zozote ambazo zitakuwa zinahitajika sisi tunazo 1.Kuna Kupiga na Kupokea Simu, Za wateja wetu zinaitwa Call Details ...

Wakili wa Serikali: Shahidi Iambie Mahakama Hizo Taarifa wewe unazitoa wapi

Shahidi: (Tigo) Taarifa zote za kampuni pamoja na Wateja wake Zinakuwa Stored Kwenye Server

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Nani anaitoa Taarifa kwenye Server

Shahidi: (Tigo) Taarifa zote Zinakuwa Served Automatically Mtu anapo piga Simu Mnara Unasima na Taarifa zinashuka na Zina switch kwenda Automatically Kwenda Kwenye Server Kuwa stored. Lakini pia Kuna watu ambao ni Observers wa kungalia na Ku Audit kazi Nzima ya Server

Wakili wa Serikali: hizo Taarifa unazozitoa Unasema Zinakuwa self Generated, Je kiuadilifu kuwa hizi ni zile zilizojitengeneza, Uadilifu wake kwenye Server?

Shahidi: (Tigo) Kama kampuni ina Mifumo ya tofauti ilitengenezwa Mahususi Kulinda hizi Server na The Whole System

Wakili wa Serikali: Unaweza kuwa unaijua hiyo Mifumo

Shahidi: (Tigo) Yeah Naweza kukujibu Kuna Mfumo Obeservit, Server au Kutoka Kwenye Switch yanyewe inakuwa na Catalist Na Kuna HUAWEI pia

Wakili wa Serikali: Unajishughulisha na nini na unafanyaje kazi?

Shahidi: (Tigo) ni software ambayo kazi yake ni Kucheki Kama Kuna Mtu au kitu kili Intend Kuingia. Kuna Firewall ni Mfumo wa kuulinzi Pale kwetu wanatumia SISQO Kuchuja kinachoingia Na Kutoka Kwenda kwenye ....

Shahidi: (Tigo) Kuna Kitu Kinaitwa AUDIT Kuangalia nani na nani Kachukua nini na Kapita wapi Kingine kuna VAPT Volumeability Acess And Penetration Test Hizi Test zinafanywa na Watu ambao ni Very Profesional lakini ni Independent Office ambapo Mnawapa Kazi Ya Kuingia .... Kwenye Mifumo yenu So It's the test Ukitaka Unamleta Unamwambia Vunja Mifumo yako Akijaribu anakwambia Wapi pana Udhaifu na wapi Mtu anaweza Kupita Inabidi Kufanya Test Mara kwa mara ili Ujue.

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Ili Usitujaze sana, Wewe Umeyajuaje

Shahidi: (Tigo) Training niliyopata, Kazi nilizofanya, uzoefu niliyopata, na Matatizo ya kila Siku (Challenge).

Wakili wa Serikali: Unaiambia Mahakama ndiyo yaliyokupa Ujuzi

SHAHIDI: (Tigo) Training, Experience ya 9yrs na Matatizo Computer nitakayopewa, nitapewa Acess kwa kuombewa Access Kwamba Mtu tuliyemuajiri anahitaji Kupata Access ili utendaji wake wa Kazi uwe Rahisi

Wakili Wa Serikali: Iambie Mahakama wewe Kwakuisaidia VYOMBO Pelelezi au VYOMBO Vya Ulinzi wewe Unafanyeje

Shahidi: (Tigo) Ukipata Kazi tuh, Kwa Maana ya kuajiriwa Kuna Vitendea Kazi kama Computer na simu ya Kwanza, Ni Vitu Vinavyo Configure Namaanisha Simu nitakayopewa na ..

Wakili wa Serikali: Unapoombewa Acess Unapewa Vitu gani?

Shahidi: (Tigo) wakati Unapewa Access Kuna SERVICE NOW system ambayo inampa Ruhusa Boss wako Ruhusa ya kuthibitisha kwamba unakuja Kufanya Kazi Fulani Kuna watu ambao ni IT security wanatakiwa kuangalia. Naingia Mara ya Kwanza Kwa Laptop lakini Kuna System Nyingine itaniambia Kama tunataka Password Yako Kuverify Either Inipigie Simu au Itumie sms, itatuma Alafu itatuma sasa Code ili niweze Kufungua Sasa Kwenye System.

Wakili wa Serikali: Sasa Umeshakuwa Approved Kwamba Huyu Mtu anafaa, Iambie Mahakama sasa Vitu gani Unakabidhiwa

Shahidi: (Tigo) Laptop Ukishapewa na Simu Kuna Vitu Vinakuwa vinawekwa ndani ya Laptop ambapo Kuna System Nyingine itaniruhusu Mimi Kuingia Mimi kwenye hiyo Computer.

Wakili wa Serikali: Code Unapewa Mara Moja unapo ajiriwa.?

Shahidi: (Tigo) Kila Ninapotaka Kuingia

Wakili wa Serikali: Nini Kitafuata

Shahidi: (Tigo) ndiyo nitakuwa na Uwezo wa Ku Access Emails, Kufungua Systems yoyote ile

Wakili wa Serikali: Nataka Kujua Sasa Jinsi ya Kuingia Kwenye Server

Shahidi: (Tigo) Kuna Mifumo sasa Nilitaja Mfumo wa SQL Itanisaidia ku-Commicate Kupata Taarifa mbalimbali

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Unaweza Je Kujua hapa umezipata na Utafanya nini

Shahidi: (Tigo) nikishaingia na kama nimezipata Kuna Button ya ku-Execute itazileta Kwenye Screen ya Laptop Yangu Kwamba naziona lakini siwezi ku-editi (READ ONLY) Kwamba naweza Kuziona tu ..nikitaka itaniruhusu Kuzi Print

Wakili wa Serikali: Ishu ya kuvisaidia VYOMBO Vya Ulinzi na Usalama Utaratibu Ukoje

Shahidi: (Tigo) Kila Chombo Cha Ulinzi Kinahitaji Kuwa na Hizo Document iwe Amri au Ombi lazima iwe In Writing

Wakili wa Serikali: In Writing Unamaanisha nini?

Shahidi: (Tigo) iwe na Proper heading, naIwe na Nini wanataka

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo ni Barua, lazima iwe hivyo

Shahidi: (Tigo) NI Barua au Order ya Mahakama

Wakili wa Serikali: Kwa kumbukumbu zako Mnamo tarehe 02 Mwezi 07 2021 ulikuwa wapi

Shahidi: (Tigo) nilipata Barua Mbalimbali za Maombi, Katika Barua hizo Kuna Barua ilitoka Kwa Kamishina wa Upelelezi wa Kisayansi Ikihitaji Taarifa za Namba ya mteja.

Wakili wa Serikali: Ulisema kuna aina Mbili Za Maombi kuwa kuna Maombi na Amri. Je hiyo ilikuwa nini?

Shahidi: (Tigo) Ilikuwa ni Requeast

Wakili wa Serikali: Unaweza Kukumbuka Ilikuja kwa Maombi Ya Kuomba Taarifa fulani za Namba fulani, Je unaweza Kukumbuka.? Hiyo namba uliyoombewa Kwenye Hiyo barua

Shahidi: (Tigo) Baada ya Kuifikiria Sana anaitaja 0719933386

Wakili wa Serikali: hilo Ombi lilikuwa ni Maombi Mangapi

Shahidi: (Tigo) yalikuwa Maombi ya Mihamala ya Fedha na KYC

Wakili wa Serikali: KYC unamaanisha nini

Shahidi: (Tigo) Usajili.

Wakili wa Serikali: baada ya Kupokea Sasa, Nini Ulifanya Kuhusiana na Ombi hilo

Shahidi: (Tigo) nilipopokea ombi Kutoka kwa kamishina, Niliingia Kwenye Computer yangu Nikaweka Credentials Zangu Nikafunga Screen Server Nikaingiza namba ya Simu kwenye Procedure Ambayo...Inaniruhusu Kupata Tigo Pesa.

Wakili wa Serikali: Unakumbuka Ilikuwa ni wakati gani?

Shahidi: (Tigo) walitaka Taarifa za mihamala ya Fedha kutoka 01 June ya 2020 Mpaka 31 June ya 2020 Nikaingia Kwenye Computer Nikaziona

Wakili wa Serikali: Baada Ya Kuziona

Shahidi: (Tigo): Nikaziprint

Wakili wa Serikali: Kabla ya kuziprint

Shahidi (Tigo): nili-execute Kuona Ni Yenyewe Nikaingiza Namba sehemu ambayo itanipa Usajili. Server yenyewe ilitoa Majibu Ambapo Taarifa Inapokaa iliweza Kutoa hiyo Taarifa ambayo niliweza Kuiomba.

Wakili wa Serikali: Na huko Unatumia Mfumo gani?

Shahidi(Tigo): SQL server

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Utendaji kazi wa Siku hiyo Ulikuwaje

Shahidi (Tigo): Laptop yangu ilikuwa Kwenye condition Nzuri Inafanya kazi Kawaida SQL sever ilikuwa Inafanya kazi Vizuri ....

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama hicho ulichokifanya, watu wapi wa Kitengo gani wanaweza Kuwa na Access ya Server kama wapo?

Shahidi: (Tigo) kila Mtu anapata Access Kutokana na Kazi anayoifanya ambapo Kuna watu wanaangalia ile server Kama Inapata Moto Kila wakati ili iweze Kufanya kazi yake

Wakili wa Serikali: Kama watu gani?

Shahidi (Tigo): Kama Legal Department Ambapo tulipaswa Kuwa na Access Ya Kuingia Kutokana na Order za Mahakama ni watu tunaoweza Kufanyia Kazi Haraka Kuna watu Wanaitwa Order Audit, Watu wa IT security Kuna watu pia wa Data warehouse ...

Wakili wa Serikali: Nyinyi Legal Department Mnapewa Access ya Kufanyaje

Shahidi (Tigo): Kusaidia VYOMBO Vya Ulinzi na Usalama na lazima Muhuri wa MIC Tanzania Ltd

Wakili wa Serikali: Turudi Kwenye namba uliyotaja, Baada ya kuprint Ukafanya nini?

Shahidi (Tigo): Niliandika Barua kumjibu Kamishina wa Makosa ya kisayansi alichokuwa anakitafuta, nikamrudishia Katika Barua nilisha Print lazima Nigonge Muhuri na Signature yangu ....

Wakili wa Serikali: Ukiambatanisha na nini hiyo Barua?

Shahidi (Tigo): Cover later, Barua ya kamishina, Mihamala ya kifedha na KYC

Wakili wa Serikali: Ukafanya nini?

Shahidi (Tigo): Nikazipeleka Ofisi ya Cyber

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Leo hii Ukionyeshwa hiyo Barua na Hizo Print Out kama utaweza Kuzikumbuka.

Shahidi (Tigo): naweza Kuzimbuka kwa Barua yangu ambapo Cover later ipo kwenye headed Paper. Cover later Ya Tigo Nimesaini Nimegonga na Muhuri

Wakili wa Serikali: Barua Ukiona Utakumbuka

Shahidi (Tigo): Nitakumbuka kwa namba Niliyofanyia Kazi

Wakili wa Serikali: Namba ngapi

Shahidi (Tigo): Nimesahau

Wakili wa Serikali: Tarehe?

Shahidi (Tigo): Nimesahau ila ni 2020

Wakili wa Serikali: ambapo ulisema hiyo namba ni ngapi

Shahidi (Tigo): 0719933386

Wakili wa Serikali: Kingine

Shahidi (Tigo): Mihamala ya Fedha pia ninaweza kutambua Kwa sababu niligonga Muhuri wa MIC Tanzania Ltd

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Kwa ridhaa ya Mahakama naomba nimuonyeshe Shahidi Documents fulani Kama anaweza Kuzitambua.

Wakili wa Serikali: Anamkabidhi Makaratasi

Wakili wa Serikali: Nakupa hii Nyaraka Ishike iangalie Moja badala ya Nyingine

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Kama umeweza Kuitambua

Shahidi (Tigo): nimetambua Barua ya juu ambayo ni Cover later ambapo ina later Head ya Tigo

Wakili wa Serikali: Kingine

Shahidi (Tigo): Nimeona Muhuri Niliogonga na namba ambavyo Nililetewa kwenye Barua ya kamishina

Wakili wa Serikali: na KYC

Shahidi (Tigo): Same same Ina namba na pia nimegonga Muhuri za Usajili wa namba hiyo, Ziwe Kielelezo katika Kesi hii

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Sasa Unaiomba nini Mahakama

Shahidi (Tigo): Naomba Mahakama hii Ipokee Barua niliyoandika kwa kamishina Uchunguzi wa Kisayansi, Barua iliyokuwa inahitaji Taarifa alizokuwa akihitaji Mihamala ya Fedha ya namba iliyokuwa anaiombea na Taarifa ...

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshitakiwa wa kwanza hatuna Pingamizi

Malya: kwa niaba ya Mshitakiwa wa Pili hatuna Pingamizi

Fredrick Kihwelo: hatuna Pingamizi Kwa Niaba ya Mshitakiwa wa tatu

Peter Kibatala: na sisi pia kwa niaba ya Mshitakiwa wa Nne hatuna Pingamizi

Jaji: tunaweza Kukiita Kielelezo namba ngapi

Wakili wa Serikali: Namba 05 Mheshimiwa jaji

Mahakama ipo Kimya kwa Dakika 10 Sasa

Jaji:
Mahakama Imepokea Barua ilivyoandikwa Kutaka Taarifa ya Uchunguzi wa Kisayansi kama Kielelezo namba 06 Napokea Barua ya Tigo, Majibu yao Kama Kielelezo namba 07 Napokea Print Out Kama Kielelezo namba 08 Na Mwisho Nyaraka ya KYC kama Kielelezo Namba 09.

Jaji: Sasa Naomba Shahidi utusomee Kila Kielelezo

Shahidi (Tigo): anasoma Barua ya Ombi la Kupatiwa Uchunguzi wa Kisayansi

Shahidi (Tigo): anasoma Barua ya majibu yao Kwa Kamishina wa Upelelezi wa Kisayansi Kwa niaba ya MIC Tanzania Ltd Ni matumaini Yangu Taarifa tuliyowapatia Itawasaidia

Shahidi (Tigo): anasoma Taarifa ya Mihamala ya Kifedha.

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji nafikiri Shahidi (Tigo) hawezi Kusoma hiyo Nyaraka yote tutakesha hapa Wao Wamuongoze na Kisha Tukubaliane kuwa Nyaraka ilisomwa.

Jaji: upande wa serikali

Wakili wa Serikali: Sawa Mheshimiwa Jaji

Wakili wa Serikali:Shahidi tufafanulie Maneno Ya Juu kama Sender Maana yake nini

Shahidi (Tigo): Send My Op namba 0719933386 Receiver 0787555200 Miamala wa Tarehe 20 Kiasi 500,0000 Tarehe 20 July 2020 Saa 2 na Dakika 21na Balance Ilikuwa 2.3M

Wakili wa Serikali: Twende kwenye hii KYC Kielelezo namba 09

Shahidi (Tigo): Imeanza na namba pale Juu Jina la Kwanza Jina la Katika, Taifa, Jenda na Vitu Vinginevyo Mstari unaofuata 0719933386 Jina Freeman Last name Mbowe Nationality Tanzanian From Kilimanjaro

Shahidi (Tigo): Kuna namba ya Tigo ya O719933386 imetuma kiasi cha fedha Tsh 500,000 kwenda kwa namba ya Airtel namba 0787555200

Wakili wa Serikali: IOP Maana Yake nini?

Shahidi (Tigo): Kitu Kimetumwa kutoka Namba hiyo

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa hayo ndiyo maeneo ambayo tulikuwa tunaomba Shahidi ayasome

Wakili wa Serikali:Kielelezo namba 7 iambie Mahakama ni nini?

Shahidi (Tigo): Barua iliyotoka kwa Kamishina Ikiwa inataka taarifa za mteja

Wakili wa Serikali: Tarehe 20.7.2020 inaonekana nini.

Wakili wa Serikali: Sender City maana yake nini?

Shahidi: Mnara wa mtu aliyetuma Pesa alikuwa wapi?

Wakili wa Serikali: Fafanua Sender One Mikocheni

Shahidi: aliyetuma fedha alikuwa Mikocheni na alikuwa Kinondoni

Wakili wa Serikali: Fafanua hapo Kwamba Mikocheni ipo Kinondoni

Shahidi (Tigo): hapana, MIKOCHENI ni KITONGOJI

Wakili wa Serikali: Kielelezo namba 9 Kuna Kitu Umesema First name na Middle name Na ulianzana namba

Shahidi: 0719933386 ni namba ya Tigo

Shahidi: First name Freeman, Middle name Aikael, Last name Mbowe

Wakili wa Serikali: Maana yake

Shahidi (Tigo): namba inamilikiwa na Mtu anaitwa Freeman Aikael Mbowe

Wakili wa Serikali: chini ni nini

Shahidi (Tigo): Tarehe ya kuzaliwa

Wakili wa Serikali: ID proof Maana yake nini?

Shahidi (Tigo): Kitambulisho kilichotumika Kusajilia namba

WS: Mwenye namba hii alisajili kwa alama za Vidole tarehe ngapi?

Shahidi (Tigo): 16.9.2019

Wakili wa Serikali: hizi Null Null Null fafanua kidogo

Shahidi (Tigo): System haipati Taarifa za Usajili wa wakati Ule wa zamani
Asante kwa update mkuu, kazi nzuri sana, hawa mashahidi wanatia kinyaa
 
Back
Top Bottom