Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake. Shahidi wa 12 Luteni Urio kuendelea kutoa ushahidi Januari 31, 2022

Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake. Shahidi wa 12 Luteni Urio kuendelea kutoa ushahidi Januari 31, 2022

Jeshi la Polisi wamefanya jambo wasilolijua. Hii kesi itaacha aibu kubwa sana kwenye jeshi la Polisi Tanzania, lkn na Nchi kwa ujumla. Kinachonisikitisha ni IGP kuiaminisha Dunia kwamba wanao ushahidi madhubuti kwamba Mbowe ni Gaidi.
Tangazo lake likachukuliwa pia na Mheshimiwa Rais nae bila kuelewa kwa undani akaiambia Dunia kweli Mbowe ni Gaidi na wenzake walishakutwa na hatia na kufungwa.

Sijui kwa nini hawataki kuwasikiliza watu wanaoshauri kesi hii ifutwe. Waathiriwa walipwe fidia na kusamehe.
Waliohusika kuwabambikia Raia wema kesi hii wawajibishwe kwa kufutwa kazi na kuisababishia Serikali hasara kubwa ya pesa na hasara ya uaminifu wa Serikali kwa Umma na Jumuiya ya Kimataifa.
Kadri siku zinavyokwenda, Taifa linajianika na kujionyesha namna jeshi letu la Polisi walivyo na mzaha juu ya usalama wa Nchi.
 
Dahh! Luteni Urio leo kanifunza kitu..hivi kumbe Koplo ni cheo cha afisa jeshii...sasa mbona huwa hawaruhusiwi kuingia "officer's mess" kumbe huwa wanawaonea tu! mimi nilifikiria ngazi ya ofisa jeshini inaanzia Luteni Usu!
Mtu yoyote anayefanya kazi katika taasisi fulani ni afisa wa taasisi hiyo ila idara husika huwa ina madaraja ya maafisa wake.

Hivyo koplo ni afisa wa jeshi(mtumishi wa jeshi) ila tukija kwenye upande wa madaraja koplo atatambulika kama askari wa cheo cha chini(R&F).
 
Urio inasemekana kuna sehemu kafungiwa na serikali. kifupi huyu sio shahidi huru. Yupo remoted. Vyombo vya habari za kiintelijensia vilitakiwa viumbue hapa
Aliposema amefikia hotelini, na jaji kuzuia kuulizwa ataje hoteli aliyofikia, Kibatala alitakiwa ambane kwa kusema uongo chini ya kiapo. Kwamba kafikia hotelini kumbe kawekwa sehemu tofauti.
 
Kesi ya ugaidi ilishafunguliwa kabla hata ya magaidi wenyewe kupatikana ama kufahamika! Duh![emoji2365] Ndo mambo ya mchongo haya!

Kibatala: Ni sahihi Kwamba Umeanza Kuwakusanya hawa baada ya Tarehe 20 July 2020

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Na wewe ndiyo Ulikuwa Unawafahamu hawa wala Siyo Mbowe

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Unaweza Kutuisaidia Kuwa Kwanini Inspector Swila alifungua Faili la Kula Njama Tarehe 18 July 2020 Wakati Wakati Umekutana hawa Vijana Tarehe 20 Mpaka 24

Shahidi: Sijui sasa
Huyu jamaa kaamua kuharibu hii kesi makusudi kabisa.
 
Ni mwehu kama hakuelewa swali aneomba ufafanuzi...kwa jibu lake amedhibitisha udhaifu wake...na ametia mashaka uelewa wake..si ajabu angeulizwa "je mlipokutana na Mbowe alikufahamisha nia yake ya ku create chaos nchi nzima' angejibu " hapana mimi aliniambia tu anataka kusababisha taharuki nchi nzima na sio mambo ya ku create chaos"....na bado ungefikiri shahidi sio mburura!
Wengi wanaojadili hapa wamesahau ishu nzima ilivyo

Wamebeba ushabiki mpaka hawaoni ujinga wa upande wa kina kibatala

Mtu anarejea stori za willy gamba halafu anajiita msomi
 
Aliposema amefikia hotelini, na jaji kuzuia kuulizwa ataje hoteli aliyofikia, Kibatala alitakiwa ambane kwa kusema uongo chini ya kiapo. Kwamba kafikia hotelini kumbe kawekwa sehemu tofauti.
Jaji naye fala tu,shahidi kaonekana ni mwongo lakini hatari watu wamuumbue uwongo zaidi na zaidi
 
Jeshi la Polisi wamefanya jambo wasilolijua. Hii kesi itaacha aibu kubwa sana kwenye jeshi la Polisi Tanzania, lkn na Nchi kwa ujumla. Kinachonisikitisha ni IGP kuiaminisha Dunia kwamba wanao ushahidi madhubuti kwamba Mbowe ni Gaidi.
Tangazo lake likachukuliwa pia na Mheshimiwa Rais nae bila kuelewa kwa undani akaiambia Dunia kweli Mbowe ni Gaidi na wenzake walishakutwa na hatia na kufungwa.

Sijui kwa nini hawataki kuwasikiliza watu wanaoshauri kesi hii ifutwe. Waathiriwa walipwe fidia na kusamehe.
Waliohusika kuwabambikia Raia wema kesi hii wawajibishwe kwa kufutwa kazi na kuisababishia Serikali hasara kubwa ya pesa na hasara ya uaminifu wa Serikali kwa Umma na Jumuiya ya Kimataifa.
Kadri siku zinavyokwenda, Taifa linajianika na kujionyesha namna jeshi letu la Polisi walivyo na mzaha juu ya usalama wa Nchi.
Sasa unawatisha polisi na aibu- hivi aibu ya polisi wewe inakuhusu nini- si yao. Wewe badala ya kuhangaika kupinga ushahidi wa polisi wewe unawaibisha polisi. Hivi leo yule mnaemuita balozi wa Ujerumani kaja mahakamani?
 
This nigga is going down...😬😬

Kibatala: Kwa hiyo wewe ulimruhusu Bwire Waendelee na Mipango yao, Mipango ipi

Shahidi: Waendelee na Mipango yao ya Kumdhuru Sabaya, Kama Wakiweza

Kibatala: kwa hiyo Baada ya Kumdhuru Sabaya Walitakiwa Kuriport Kwako tena

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kwa hiyo Wewe Luteni Wa Jeshi la Wananchi Tanzania, uliwaruhusu Kwamba wakatekeleze Mpango wa Kumdhuru Sabaya Kwa sababu wapo Ground?

Shahidi: Ningefanyaje sasa na Watu wapo Ground

Kibatala: Kwani Wakati huo walikuwa weshamdhuru au Bado

Shahidi: Walikuwa Bado, Ndiyo Wapo Kwenye Mpango

Kibatala: Je Baada ya Bwire Ku Confess Kwako, Ulimwambia Afande Kingai

Shahidi: Sikumwambia
 
Aliposema amefikia hotelini, na jaji kuzuia kuulizwa ataje hoteli aliyofikia, Kibatala alitakiwa ambane kwa kusema uongo chini ya kiapo. Kwamba kafikia hotelini kumbe kawekwa sehemu tofauti.
Halafu kesi ingefutwa? Ndo ujue Mh. Kibatala ni Comedian zaidi ya Masanja
 
Aliposema amefikia hotelini, na jaji kuzuia kuulizwa ataje hoteli aliyofikia, Kibatala alitakiwa ambane kwa kusema uongo chini ya kiapo. Kwamba kafikia hotelini kumbe kawekwa sehemu tofauti.
Nadhani kuna sehemu shahidi huyu atatakiwa kuthibitisha hotel aliyofikia
 
Hatuna askari wenye weledi /wao kwao ni msuli basi ndo haya yanayotokea
Huwa tunaaminishwa tuna jeshi na askari bora kwa ukanda wetu wa east Africa,dah!! nimemsikiliza Luteni wetu anavyojichanganya kujibu maswali..namashaka sana na vikosi vyetu.
 
Back
Top Bottom