Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake. Shahidi wa 12 Luteni Urio kuendelea kutoa ushahidi Januari 31, 2022

Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake. Shahidi wa 12 Luteni Urio kuendelea kutoa ushahidi Januari 31, 2022

Mjue shahidi ni komandoo na wala si mtu mjinga mjinga
angalia Comedian Mh. Matata anavyojiingiza mdomoni mwa komandoo Urio

Matata: kwenye huo Umuhimu hukuona Kuna Umuhimu Wa Vinasa Sauti na Meseji ambao Vitasema Exactly Kuwa anataka Kulipua
Masoko

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Mbowe alikuwa alishaniambia Kwa Meneno, asingerudia

Matata: Narudia Swali langu, kwenye huo Umuhimu hukuona Kuna Umuhimu Wa Vinasa Sauti na Meseji ambao Vita, sema Exactly Kuwa anataka Kulipua Masoko

Shahidi: Sikuwa na Vifaa Vya kunasa Sauti
Hapa wakili ndiye aliyemtega shahidi kama alishaongea mara moja na kwamaneno ya asingerudia maana ake hakukua na mijadala tena ya mipango baina yake na mharifu, hivyo dhana ya vikao vya mipango anaikanusha shaidi havikuwepo, ndomana vikao vyote walivyokaa anakiri kuongoza yeye na sio mbowe nakatika hili ndo mana wakili akamhoji kuwa mipango ya uharifu aliongoza yeye? Hoja ameikamirisha shaidi baada yakukiri alipewa kazi ya kutafuta walinzi nasivinginevyo''tusipotoshe''
 
Mbowe sio kiazi kiasi hicho, yaani akurupuke aende kuongea na luteni wa jeshi kuhusu kuleta taharuki?
Hivi kwa cheo Mbowe alichonacho, namna anaijua serikali kuliko hata mimi ambae nisingekubali, inakuwaje aongee na luteni wa jeshi jambo classified kama hilo eti kisa ni homeboy?
Urio alimtafutia mbowe walinzi binafsi ambao ni Asikari wasitaafu kwa nia njema pasipo shaka lakini DC Sabaya alipopata taarifa kuwa mbowe anaenda kuwa na ulinzi imara ambao utamfanya ashindwe kumhujumu mbowe ndipo akabuni mbinu ya kutengeneza kesi ya mchongo ili kumdhoofisha mbowe hata huyo Lt Urio alikuwa mtuhumiwa ambapo aliteswa na kupigwa sana, cha ajabu sasa amekuwa shahidi wa kulinda uonevu wa watesi akina kingai mahita na wetesi wenzao
 
Kuna uncle angu standard 7 alimlaza na viatu askari upande wa serikali....kweny kesi mahakamani.....

Uncle Alipewa mzizi na babu aweke mdomon akat anahojiwa mahakamani....

Wakati wa hukumu uncle akaulizwa na jaji una la kujitetea....

Aka muuliza askar shahd upande wa serikal ni Mara yake ya ngap kusimama katika mahakama tukufu kutoa ushaid wa uongo ambao ni batili......

Askar; akajib Mara 3

Wakili wa serikali; akauliza Mara ngap akajibu Mara 3,

Jaji ;akauliza Mara ngap.....askar akajib Mara 3


Hukumu ikatoka jamaa yupo huru...

Jaji akati anasoma hukumu alimuhukumu askari kifungo au faini.....Askari ilibid alipe faini kuepuka kifungo....kwa kutoka ushaid wa uongo mahakamani......


#Mbowe sio Gaidi
#free freeman
 
Story gani ya Willy Gamba imerejewa? Unasoma lakini huelewi “context”. Pole yako.
Alikuwa areje nyakati tu,hakuna story ya Willy Gamba iliyorejelewa.Kwenye cross examination Kuna mambo na techniques nyingi.Kuna kitu kinaitwa demeanor.
 
  • Thanks
Reactions: T11
Vita ya waaminifu wa uongo na waaminifu wa ukweli,giza na nuru,uongo haujawahi kuushinda ukweli wala giza kuishinda nuru bado kitambo kidogo mwenye haki atashangilia
 
Kwamba dunia inamfuatilia Mbowe kwa lipi? Na kwamba inaweza kuizuia Tanzania kumfunga?! Ndiyo kinga yenu? Muulize X mass aliiilia wapi na leo analala wapi? Hii kesi mpaka 2026
Kwa hiyo unahakika Kuna kesi ya kujibu mpaka hapo? Hakuna hata jinai moja hapo yenye ushahidi concreat.Ninachokiona ni fabrication tu.Hakuna hata mesej moja au voice note inayoonesha jinai ama kusudio la kutenda jinai.Mtu hafungwi tuNd,anafungwa kwa kesi ya kujibu ambayo upande wa mashtaka utaleta ushahidi usioacha hata punje tu ya shaka.Shahidi aliyekuwa anasafiri bila ticket,anaingia office za serikali bila kusign vitabu vya wageni ndo aje asababishe mtu afungwe.Siyo rahisi.
 
Urio yupo kwenye jela za jwtz yupo chini ya Ulinzi hayupo huru hata ushahidi anaoutoa ni wa maelekezo ya kuwalinda akina kingai mahita na watesi wenzao ni vyema Serikali wangefuta hiyo kesi kuepuka fedheha zaidi
Sasa kwann Jwtz wamuweke kizuizini?
 
Matata: Ukiulizwa, Ukiachana Na Sabaya ni Viongozi gani wengine Walipanga Kuwashambulia

Shahidi: Sikutaja Jina la Kiongozi Yoyote, Hakuniambia Kiongozi Yupi



Sasa Kingai yeye alijuaje kuwa kiongozi aliyetakiwa kudhuliwa ni Sabaya wakati mwenye first hand infomation bwana Urio anasema Mbowe hakumwambia ni Kiongozi yupi ..... Ah ha ......!!
Mbowe hakusema lakini Bwire alimwambia
 
Luteni ama Afisa wa JWTZ anaona uhalifu unataka kutendeka, option anayochukua ni kumtafuta DCI ambaye yupo mbali badala ya kwanza kuriport kambi iliyo karibu kabisa na eneo ambalo walifanya mkutano na Mbowe ili kuzima tukio nzima kwa uharaka.

Sasa tukisema huyu Luteni ni BOYA kabisa tutakuwa tumesema urongo ndugu zangu ?
Nilivyoelewa ulikuwa mchongo Mbowe ajae

Napenda kusema heri tusikilize tu itakuwaje maana urio sio mwehu
 
Nilivyoelewa ulikuwa mchongo Mbowe ajae

Napenda kusema heri tusikilize tu itakuwaje maana urio sio mwehu
Lt Urio sasa hatoi ushahidi kwa mjibu wa ukweli halisi bali anatoa ushahidi wa maelekezo tokea kwa kingai na watesi wenzake nadhani umeshuhudia anavyo jikanyaga kanyaga kujibu maswali
 
Kesi ilifunguliwa yarehe 18, August, yeye kaanza kutafuta watu yarehe 20, August. Mh mnisamehe ndugu zangu wa upande wa pili[emoji103][emoji103]
Hili limenishangaza pia
 
Na ukumbuke awali Lt Urio alikamatwa kama mtuhumiwa akateswa sana na hao hao akina kingai cha kushangaza leo kawa shahidi baada ya kununuliwa na akina kingai
Urio inavyoonesha angali mateka wa kina Kingai si kwamba kanunuliwa (rejea maswali ya kiufundi toka kwa mh. Kibatala - kamuuliza katokea wapi kuja mahakamani - hotelini au nyumbani!? Alisali lini kanisani kwake...)

Huyu inaonesha yaliyomkuta ROMA ndio yanaendelea kwake hajatokea kwake bali katoka kizuizi fulani!!
Giza linaendelea kufunikwa na mwanga hatimae kutapambazuka na nuru itaangaza huku madhalimu wakiangamia mmoja baada ya mwingine.
 
Nilivyoelewa ulikuwa mchongo Mbowe ajae

Napenda kusema heri tusikilize tu itakuwaje maana urio sio mwehu
Wewe mwenyewe umethibisha ilikuwa ni mchongo. Nasi kwamba Mbowe alikuwa na nia mbaya . Sasa kesi za mchongo za nini kama si za uonevu ?!
 
Back
Top Bottom