Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake. Shahidi wa 12 Luteni Urio kuendelea kutoa ushahidi Januari 31, 2022

Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake. Shahidi wa 12 Luteni Urio kuendelea kutoa ushahidi Januari 31, 2022

Hakuna nchi yenye viongozi wa hovyo kama hii, yaani wameacha kabisa kesi ya kubumba kama hii eti iendelee ili iweje sasa. Very stupid.
 
LT Urio ni ndugu yake mbowe kiukoo na mbowe alimuomba amsaidie walinzi makomandoo wasitaafu kwa nia njema pasipo shaka akiwa na nia ya kujilinda dhidi ya hujuma tokea kwa Dc Sabaya ambaye baada ya kubaini hilo ndipo akatengeneza kesi ya mchongo ili kumdhoofisha mbowe lakini hao siyo magaidi na hakukuwa na ugaidi wowote ule
Urio kasema Bwire, Adamoo na Doyi ni watu wazuri sana! Na aliwaambia wataenda kufanya kazi ya VIP protection. Na hakuwahi kuwaambia kuhusu ugaidi wala matukio ya kuleta taharuki.
Ndio huu wa Urio. Hapa ndio serikali imeweka roho yake.
Mkuu huyu nadhani asingetekwa na kupangiwa ya kusema nadhani angenyoosha ukweli wote wa kina Kingai, Sabaya na kundi lao la wasiojulikana.
Mimi bado najipa moyo kuwa mashahidi watakaokuja baada ya Lt. Urio ni hatari zaidi.

NB: Ushahidi wa Urio hauna muunganiko... Kuna vitu anataka kusema lakini anaogopa!
 
Halafu imekuaje Ghafla Huyu URIO amemchukia Sana Mboweee? Kiasi kwamba anamuona kama nini sijui
Mbowe kategua mtego ndiyo maana Urio kachanganyikiwa na nilazima ashitakiwe kwa kuwaingiza nduguze matatani na hii lazima iende mahakama ya kijeshi nakule jakuna ujinga ujinga
 
Halafu imekuaje Ghafla Huyu URIO amemchukia Sana Mboweee? Kiasi kwamba anamuona kama nini sijui
UkiSoma between the lines; wala Lt. Urio hajamchukia Mbowe.
Tatizo ni waliochukua simu zake na anakotokea kuja kutoa ushahidi wake.
 
HII KESI INASHABIHIANA SANA NA KESI NYINGINE YA MCHONGO ILIYOMO KWENYE BIBLIA.....

1 Wafalme 21:

4 Basi Ahabu akaenda nyumbani kwake, ana moyo mzito, tena amekasirika, kwa sababu ya neno lile aliloambiwa na Nabothi Myezreeli, akisema, Sitakupa urithi wa baba zangu. Akajilaza kitandani pake, akageuza uso wake, akakataa kula.

5 Lakini Yezebeli mkewe akamwendea, akamwambia, Kwa nini roho yako ina huzuni hata usile chakula?

6 Akamwambia, Kwa sababu nimesema na Nabothi Myezreeli, nikamwambia, Unipe shamba lako la mizabibu kwa fedha, au, ukipenda, nitakupa shamba la mizabibu lingine badala yake. Akajibu, Sitakupa shamba langu la mizabibu.

7 Yezebeli mkewe akamwambia, Je! Sasa wewe unaumiliki ufalme wa Israeli? Ondoka, ule chakula, moyo wako ufurahi; mimi nitakupa shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli.

8 Basi, akaandika nyaraka kwa jina la Ahabu, akazitia muhuri yake, akazipeleka zile nyaraka kwa wazee, na kwa watu wenye nguvu waliokuwa katika mji wake, waliokaa pamoja na Nabothi.

9 Akaandika katika zile nyaraka, akasema, Pigeni mbiu ya watu kufunga, mkamweke Nabothi juu mbele ya watu,

10 mkainue watu wawili, watu wasiofaa, ili wamshitaki, na kumshuhudia, kunena, Umemtukana Mungu na mfalme. Kisha mchukueni nje, mkampige kwa mawe, ili afe.

11 Wale wazee wa mji wake, na walio wenye nguvu waliokaa mjini mwake, wakafanya kama Yezebeli alivyowaagiza, kama ilivyoandikwa katika nyaraka alizowapelekea.

12 Wakapiga mbiu ya watu kufunga, wakamweka Nabothi juu mbele ya watu.

13 Na hao watu wawili, watu wasiofaa, wakaingia, wakaketi mbele yake; wale watu wasiofaa wakamshuhudia Nabothi mbele ya watu, wakasema, Nabothi amemtukana Mungu na mfalme. Ndipo wakamchukua nje ya mji, wakampiga kwa mawe hata akafa.
 
Kuna maelekezo mengine hugomewa na mungu ndiyo maana Lt Urio amejikanyaga kajichanganya changanya mahakamani na endapo Jaji atatoa hukumu feki ajua mungu yupo anaona kila baya linaloendelea
Cha kushangaza Kingai alifunguaje faili CD/IR/2097/2020 tarehe 18/7/2020 kabla ya informer Luteni Urio kupeleka taarifa za ugaidi tarehe 24/7/2020? Je, Kingai alioteshwa kwamba kutatokea taarifa za ugaidi afungue faili?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
aisee balaa hili!!
kumbe ndio maana wafuasi wa Mbowe walikuwa wakishinikiza mahakama imfutie Kesi!! sasa uovu wote huu alikuwa anauratibu huyu mbowe tungeujuaje?!!
afadhali sasa tunajua matendo yake ya kimafia aliyo kuwa anayafanya dhidi ya serikli.
huyu mhalifu alikuwa anawatumia watu mbalimbali amabo sio waaminifu na waadilifu kukidhi mhitaji yake.........ndio maana alikuwa anatumia neno "atakinukisha" maana yake atachafua amani ya nchi.
Charge sheet inasema mnamo May 2020 watuhumiwa walikula njama za kutenda uhalifu nchi isitawalike, lakini ushahidi uliotolewa na informer Luteni Urio walianza kukutana 24/7/2020. Hapa Kuna tatizo Kati ya Polisi walioandaa mashitaka na informer Luteni Urio! Inakuwaje mashitaka yaseme njama zilifanyika May 2020, lakini mkutano wa kwanza wa njama uwe 24/7/2020? Mungu ni fundi wa kuumbua.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Dahh! Luteni Urio leo kanifunza kitu..hivi kumbe Koplo ni cheo cha afisa jeshii...sasa mbona huwa hawaruhusiwi kuingia "officer's mess" kumbe huwa wanawaonea tu! mimi nilifikiria ngazi ya ofisa jeshini inaanzia Luteni Usu!
Keshavurugwa huyo, hata gari lake amepark at owner's risk huko kambini jeshini!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hivi hawa akina Mh. Kibatala unaweza ukatoa hela yako ukawalipa kwamba wanakutetea kweli??
Ila UNAWEZA kuwalipa kina Kingai na Swilwa waliofungua kesi tarehe 18/7/2020 kabla ya kupelekewa taarifa za ugaidi na Luteni Urio tarehe 24/7/2020? Hao ndo UNAWEZA kuwalipa wanafungua kesi ya ugaidi mapema kabla ya informer Luteni Urio kupeleka taarifa!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Urio hana analojua kuhusu Sheria ushahidi wake lazima utupwe kampuni. Shahidi gani huyo anajikanyaga hivyo?
 
Hakika uongo haudumu. Nyerere aliwahi kusema ukiwa Muongo usiwe msahulifu.
Freeman Mbowe hana kesi ya kujibu hapo
 
Ila UNAWEZA kuwalipa kina Kingai na Swilwa waliofungua kesi tarehe 18/7/2020 kabla ya kupelekewa taarifa za ugaidi na Luteni Urio tarehe 24/7/2020? Hao ndo UNAWEZA kuwalipa wanafungua kesi ya ugaidi mapema kabla ya informer Luteni Urio kupeleka taarifa!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Huijui serikali
 
Back
Top Bottom