Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake. Shahidi Justine Eliya Kaaya, amtaja Ole Sabaya. Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 28, 2021

mwenzako kashapigwa miaka 30, kumbe na wewe ulijua matendo yake siyo ila ukayaficha kwa sababu unazozijua wewe, bac sawa Shahidi ila mbele ya safari utatuonyesha GOLGOTA palikuwa ni wapi, na kina nani waliingia humo.
 

.tena level ya Komando ambaye ambao bado vijana wenye nguvu.................................... .....(kuna mengi hayawezi kusemwa kwenye kesi)
 
Hii kesi inaitia aibu serikali. Mi nilikuwa nadhani commando ni asset, kumbe takataka kabisa, wanafukuzwa kiholelaholela, hata Mimi naweza kumuajifi awe mlinzi wa ?getini nyumbani kwangu.

Hivi Hawa wamefundishwa kwa gharama kubwa, si wanaweza chukuliwa na nchi jirani?
 
Ficha ujinga wako usije kudharaulika mbele ya jamii
"Shahidi: Siku Moja nikiwa nyumbani nilipigiwa simu kwenye simu yangu Airtel 0693006700 kutoka kwenye namba ya Airtel 0784779944 na Mtu aliyejitambulisha Kuwa ni Freeman Mbowe"- Tuendelee kula mtori nyama tutaikuta chini
 
Wakili wa Serikali: We Ulikutana na nini?

Shahidi: Palikuwa na Barabara ya kwenda Machame na Nyingine kwenda Arusha na Nyingine Moshi

Wakili wa Serikali: Nini kikatokea?

Shahidi: Ilikuja Gari aina ya Land cruiser V8 Yenye Mlingoti na Bendera ya Bunge ikiwa na Plate Namba zilizoandikwa KUB

Wakili wa Serikali: Nini kilitokea?


Shahidi: Ilisimama Upande wangu, ikashusha Kioo Upande wa Abiria, nikamuona Mwenyekiti akaniambia Panda

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuambiwa Upande nini kili tokea?

Shahidi: Alishuka Mtu kutoka Siti ya Nyuma akaniambia pita nikaingia kwenye Gari
 
Hii dunia ngumu sana yaani mwenye mamlaka anaweza akaamua "huyu gaidi" weka ndani.

Rais Samia nakuomba ukumbuke uislamu unapinga dhulma kwa yeyote yule hata mnyama (sembuse binadamu).

Hii kesi ya Mbowe naona ni ya kubambika na tayari kuna athari ya kauli yako katika kesi hii wakati ulipohojiwa na BBC hivyo ni ngumu sana Mbowe kuchomoka (hata akiwa hana hatia) kwa sababu mahakama iko CHINI YAKO na ni ngumu mno kwa mahakama kuamua kinyume na mtazamo wako.

Kama ishu ni makongamano ya kikatiba ilikuwa bora ungemuita Mbowe privately then mkayajenga wenyewe huko ila siyo hali hii.

Makosa ya kuwaweka akina Mselemu ndani mama etu unayajua hasa na ndo maana ulipopata uongozi kesi yao imefutwa naamini JK anajuta kwa hili hivyo nakuomba nawe mama usirejee kosa kama hilo ni DHAMBI.

Mama Samia binafsi nakupenda sana na natamani ufanikiwe katika uongozi wako katika nyanja Mbalimbali lakini kwa kesi hii nakuhurumia sana (unajijengea chuki kwa Watanzania).

You better Change mama isije kuwa shida kwenye uongozi wako na kukumbukwa kwa mabaya.

Wakuu kama nimemkwaza yeyote kumradhi lengo ni kujenga.
 
Kweli kabisa ndiyo maana yule mwasisi wa chuki hizi za kisiasa yupo motoni sasa hivi anaokwa kama ndafu.
Hapana ndugu, adhabu ya moto kwa waovu bado haijatekelezwa.

Kwa mujibu wa 'Maandiko ya Biblia' wafu wote wanasubiri siku ya ufufuo wa pili na baada ya ufufuo wa pili ndipo itafuatia hukumu.

Kutakuwa na aina mbili za 'ufufuo wa wafu'. Ufufuo wa kwanza ni ufufuo wa watakatifu siku ile KRISTO atakaporudi. Hao watakaofufuliwa siku ya kurudi BWANA YESU ni watakatifu na hakutakuwa na hukumu siku hiyo bali wataenda kula raha na kustarehe kwenye UFALME WA MUNGU kwa muda wa miaka 1000.

Na baada ya hiyo miaka elfu moja kupita, wale wafu wote ambao hawakufufuliwa siku ile aliporudi BWANA ndiyo watafufuliwa na kuletwa hukumuni. Na kila atakayeonekana ana hatia atatupwa kwenye 'Jehanamu' ya moto.

Hivyo basi hata kama Magufuli ana hatia bado hajahukumiwa. Sasa hivi amelala na atalala mpaka hapo atakapofufuliwa na kuletwa hukumuni.
 
Kiruswa naye aitwe kama shahidi aulizwe kama alipigiwa hizo simu na huyo dada shahidi na kuelezwa hayo maneno....kampuni husika ya simu itoe records za hizo namba hizo tarehe kama kweli kulikuwa na mawasiliano ya dada shahidi - Mbowe na huyo Mbunge Kiruswa...

Lakini pia bado naumiza Kichwa....Mbowe anawezaje kuwa jasiri kutumia simu yake kufanya mawasialiano na watu anaotaka kufanya nao issue mbaya, inawezekana Mbowe aende mwenyewe front na sio kutuma watu? BADO NATAFAKARI....tuendelee mstari kwa mstari then tujadili..
 
Mwendazake alichukua vijana wa TISS na KUWAGAWIA ujaji ili wakaivuruge Mahakama, na kwa kweli wamefanikiwa sana. Bila ya Katiba Mpya itatuchukua miaka mingi sana KUIREJESHA Mahakama kwenye hadhi yake ya kutoa hukumu za haki.
 
Kwa ushahidi tu wa jana na leo, kesi imekaa vibaya sana kwa Mbowe. Yaanii kifungo kinaanza kumnyemelea. IGP Sirro alikuwa sahihi aliposema Mbowe siyo malaika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…