Kesi ya inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake itaendelea katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa, ambapo Ushahidi unaendelea kutolewa. Shahidi wa kwanza kwa upande wa Jamhuri ACP Kingai atamalizia Ushahidi wake.
========
Mawakili upande wa utetezi wapo katika chumba cha Mahakama
Watuhumiwa wote wamekwisha wasili katika ukumbi wa mahakama asubuhi hii
Jaji ameingia
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Imetajwa
Wakili wa Serikali: Ikupendeze Mh Jaji Naitwa Robert Kidando nimeongozana na
1. Chriss ........
2. Abdallah Chavula
3. Jenitreza akitali
4. Ester Martin Ignas
5. Mwinuka Tulimanywa Majige
Kibatala: ikukupendeza Mheshimiwa Jaji naitwa Peter Kibatala nipo pamoja na
; 1. Alex Massaba
2. Seleman Matauka
3. Sisty Aloyce
4. Dickson Matata
5. Michael Mwangasa
6. Jonathan Mndeme
7. Hadija Aron
8. Evaresta Kisanga
9. Maria Mushi
10. Idd Msawanga
11. John Malya
JAJI: upande wa Jamhuri
Wakili wa Serikali: Shauri limekuja kwa ajili ya Re examination kwa Shahidi wa Kwanza, Yupo na tupo tayari kuendelea.
Jaji: Upande wa Utetezi..?
Kibatala: Na sisi tupo tayari Mheshimiwa Jaji
Jaji: Umesema kwa niaba ya Wenzio Siyo.?
Kibatala: Ndiyo
Jaji: Mshitakiwa namba 1,2,3, na 4 Wanainuka Kila Mmoja Ishara kwamba wapo Mhakamani
Jaji: Shahidi Jana ulihojiwa Maswali ya Dodoso na Upande wa Utetezi, Leo tukasema utakuja kwa ajili ya Re examination, Nakukumbusha bado upo chini ya kiapo.
Wakili wa Serikali: Jana Mtobesya alikuuliza wakati gani Jalada la Uchunguzi Lilifunguliwa na wakati gani Jalada la Kesi lilifunguliwa
Shahidi: Jalada la Uchunguzi tulikuwa tumefungia Baada ya Kukutana na Luteni Denis Urio katak Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai.
Wakili wa Serikali: Na Jalada la Kesi
Shahidi: Nilifungua baada ya Mimi Kupata Taarifa kuwa Vijana walipokuwa wanatafutwa na Luteni Urio kwa Amri ya Mbowe ndipo tulifungua Jalada.
Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali kuhusiana kama Ulikuwa na Taarifa ya kabla ya Kumchukua Maelezo Mshitakiwa wa Pili, Elezea ni taarifa gani.
Kibatala: OBJECTION swali lilikuwa kwamba Swala la Kumtafuta Moses Lijenje, Je Ulimuhoji Mshitakiwa wa Pili,"
Jaji: Wakili wa Serikali
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa sijauliza alichofanya Cross examination yeye, nipo kwa Mtobesya
JAJI: Uliza tena
Wakili wa Serikali: Uliulizwa kuhusu Kuwa na Taarifa za Moses Lijenje wakati unamuhoji Mshitakiwa wa Pili, Je ulijua Taarifa hizo kabla au Baada?
JAJI: Kibatala Umesikia Swali?
Kibatala: Nimesikia lakini kaniondoa Mimi, Sasa ni Eneo la Mtobesya
Shahidi: Nilipata Taarifa kuwa Freeman Mbowe alikuwa anatafuta Kundi la Waalifu
Kibatala: Wakili Mtobesya Hakufika huko, it's something New alisema alikuwa anatafuta Vijana
JAJI: Ndiyo namimi nimesikia hivyo Jana ulisema Alikuwa anatafuta Vijana siyo Kundi la Wahalifu
Shahidi: Ndiyo nilipata Taarifa kuwa Freeman Mbowe Alikuwa anatafuta Kundi la Vijana walioachishwa kazi Jeshini, Kwa dhumuni la Kudhuru Viongozi wa Serikali na Pia Mpango wa maandamano ya kushinikiza Viongozi ya siyo kuwa na Kikomo na Kwamba Lengo la Kufanya hivyo Nchi ........isitawalike na ionekane imefeli kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Wakili wa Serikali: Uliulizwa hapa Jana Kwamba wakati Mshitakiwa Wa pili Kama Ulikuwa Umempa Onyo, kuhusiana na Ukamataji, wewe Ukasema ulikuwa umeshampa Haki zake. Haki zake zipi?
Shahidi: Haki zake ni Pamoja na Kumfahamisha Kosa alilokuwa anashitakiwa nalo na Kwamba....... halazimishwi Kusema lolote ila Jambo analozungumza linaweza Kutumika kama Ushahidi Dhidi yake Mahakamani.
Wakili wa Serikali: Uliulizwa kwamba Matukio ya Kula Njama Yalifanyika kati ya 01 May 2020 na tarehe 05 August 2020 lakini katika Ushahidi wako ulisema Kula Njama huku kulifanyika tarehe 25 July 2020 hadi tarehe 01 August 2020 huko Aishi Hotel. Unasemeje Juu ya Ushahidi .......wako Kupinga na Hati ya Mashitaka?
Shahidi: Naomba Kuona hiyo Hati ya Mashitaka
Jaji: Utetezi Mapingamizi Juu ya Hilo
MTOBESYA: Hapana apewe tu
Shahidi: Miye naona Hakuna utofauti bado, ipo kati ya (in between) bado
Wakili wa Serikali: Uliulizwa Swali Kuhusiana Maelezo ya mshitakiwa wa Kwanza kwamba yaliandikwa Chang'ombe ukasema ndiyo Ni kweli Na Maelezo Mshitakiwa wa pili na watatu yalichukuliwa Central Dar es Salaam Eleza kwanini uliamuru Maelezo ya Mtuhumiwa wa Kwanza .......yachukuliwe Chang'ombe?
Shahidi: Kwanza Chang'ombe ni Dar es Salaam, Pili uwezi kufananisha na Moshi, Alafu pia na angalia Masaa Manne.
Utetezi: OBJECTION Mheshimiwa Jaji wamuelekeze Shahidi wao Vizuri hatutaki kila Saa Kusimama Simama.
Jaji: Jamhuri
Wakili wa Serikali: Shahidi Eleza sababu tu kwanini uliamuru Maelezo ya Mshitakiwa wa 01 yachukuliwe Chang'ombe?
Shahidi: Baada ya Mshitakiwa kudanganya kuhusu Makazi yake.
Utetezi: OBJECTION Mheshimiwa Jaji hayo ya Kudanganya ni Mapya Sheria ya Ushahidi ipo wazi haupaswi Kuongea Mambo Mapya
Jaji: Nafikiri shida ipo kwenye Neno Kudanganywa hata Mimi sikusikia Neno "Kudanganywa" ondoa hilo Neno uendelee
Wakili wa Serikali: Uliulizwa kwamba Mshitakiwa wa Pili uliomuonya kuhusu Kula Njama ya kutenda Matendo ya ugaidi, kwanini hukumuonya na Makosa mengine
Kibatala: OBJECTION hayo niliuliza Mimi sikumuuliza kwanini Hukumuonya kila Shitaka, Nilikuwa nauliza kwa kila Kosa........Kama Mnataka twende hivyo tutaomba kumuhoji tena.
Jaji: Unasemaje wakili wa Serikali
Wakili wa Serikali: Nitarudia swali Mheshimiwa
Wakili wa Serikali: Uliulizwa Swali kuhusiana na Kuamini na Kutoamini hasa kwenye sababu ya Wakili.
Shahidi: Nilikuwa siamini kwamba Mkuu wa Wilaya anaweza Kushusha Bendera lakini pia ndiyo iwe sababu ya Kumdhuru Kiongozi wa Serikali. Lakini statement niliiamini sababu alitoa yeye.
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kupatiwa Kielelezo P1
Wakili wa Serikali: Shahidi chukua Karatasi hii Nitakuuliza maeneo ambayo ulihojiwa na Mawakili wa Utetezi
Wakili wa Serikali: Tafuta eneo ulikohojiwa kuhusiana Kumfikisha Mheshimiwa Mikocheni, ukipata nitakuuliza swali
Mahakama Bado Ipo Kimya Shahidi anatafuta
Wakili wa Serikali: Baada ya Kufika Dar es Salaam na Kumfikisha Mheshimiwa Mikocheni, hujaona
Jaji: Labda uchukue Kwanza wewe Usome halafu umuonyeshe.
Wakili wa Serikali: Kama hawatokuwa na pingamizi
Kibatala: Hatuna Mheshimiwa Jaji
Wakili wa Serikali: Soma hapa
Shahidi: Baada ya Kufika Dar es Salaam na Kumfikisha Mheshimiwa Mikocheni Mimi na Mohammed tulipewa Laki mbili mbili baada ya Kesho yake kuwa anakuja Lissu na hakumpokea.
Wakili wa Serikali: Uliulizwa kuwa huyo Mheshimiwa ni nani ukasema sasa ieleze Mahakama Huyo Mheshimiwa ni nani?
Mtobesya: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Kifungu cha 61 Cha Sheria ya Ushahidi Inasema Nyaraka Isitafsiriwe Bali Nyaraka ijieleze yenyewe, hapo Shahidi anaulizwa tafsiri.
Wakili wa Serikali: Naona hiyo Objection haina Mashiko sababu tutakuwa hatuna Cha Kufanya.
JAJI: Nafikiri Mtobesya Hoja yako inahusu Thamani ya Nyaraka, Sasa Mahakama itaangalia hicho anachokisema Kipo kwenye Nyaraka.?
MTOBESYA: Sawa Mheshimiwa Jaji
Shahidi: Ni Mheshimiwa Mbowe, Kwa sababu Mheshimiwa aliyetajwa kwenye Statement hii ni Mheshimiwa Mbowe na Mbowe Mwenyewe anaishi Mikocheni
Wakili wa Serikali: Uliulizwa pia kuhusiana na Kupewa Laki mbili na Mohammed, huyu Mohamed med ni nani?
Shahidi: Ni Ling'wenya kwa sababu huko Juu tulikuwa tunazungumzia Mohamed Ling'wenya na statement hii alikuwa anatoa Mwenyewe.
Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali Kama kwenye Statement hiyo, kama alivyoelezea yeye kama Mshitakiwa Wa pili Kama alimfuatilia Sabaya katika Maeneo aliyokuwa akienda Arusha Uliulizwa swali wewe Ukasema Hapana, Sasa nitakupeleka kwenye Statement halafu utafafanua.
Kibatala: OBJECTION samahani Mheshimiwa Jaji labda kwa Maelekezo yako nitakubali Maelekezo ya Mahakama, anachoulizwa Shahidi Alisha Jibu kuwa Hakuwa Arusha anaulizwaje Jambo hilo hilo tena.
JAJI: Nafikiri Ngoja tusubiri swali lake.
Wakili wa Serikali: Kwa Utaratibu wa Mahakama Kibatala anapaswa aongee kwa Ushahidi Kama Kuna kitu kweli Umekiona Kitolee Ushahidi, Siyo kuja na Neno Una suspect, Nani kafanya na Kitu gani Kimefanywa
Jaji: Kibatala ulikusudia Nimuonye, na Tunachukulia una Taarifa za ......kiintelijensia kwamba tumuonye shahidi kwa Intelijensia yako. Kibatala: Mimi nimesema Mahakama imuangalie.
Jaji: Basi kwa sababu Mimi sijaona naomba Upande wa jamhuri waendelee Kuuliza Maswali
Shahidi: Katika Kufuatilia Nyendo za Sabaya tulienda Club Kokoriko lakini hatukumpata Mheshimiwa Sabaya Siku hiyo.
Wakili wa Serikali: Eleza sasa Kwenye Statement hii Kama Mshitakiwa alifika Club Kokoriko.
Shahidi: Alifika
Wakili wa Serikali: Uliulizwa pia swali kuhusiana kama Kuna sehemu yoyote kama Mshitakiwa Wa Pili amechukuliwa finger print katika Statement hii, NI kwanini katika Statement hii hakuna Maelezo ya Kuchukuliwa finger Print
Shahidi: Mimi kama Mchunguzi nilishaona Hakuna haja.....Ya kuchukua Finger prints
Shahidi: Hitaji la Kuchukua Finger Prints lilikuwa baada ya Kumpekua Mshitakiwa Namba Moja na baada kukuta Kijitabu ikabidi sasa Kuchukua Finger Prints. Wakati nachukua Maelekezo Mshitakiwa wa pili ilikuwa tarehe 07 August 2020 kabla ya Kupata Kijitabu hicho.
Wakili wa Serikali: Uliulizwa Kama Ulichukua Sampuli za Finger Prints za Pistol inavyodaiwa kukutwa na Mshitakiwa wa Pili. Sasa wewe Kama Mchunguzi ni kwanini hukuchukua Finger Prints na Sampuli za DNA.
Shahidi: Mimi sikuona haja ya kuchukua Finger Prints kwa sababu.......Mshitakiwa tulikuwa naye, Tunafanya Finger prints kama Mshitakiwa amevunja na hayupo Sisi Hatukuwa na hitaji hilo kama alivyo uliza wakili.
Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali kuwa Kwa kipindi Chote baada ya Kupata nia ya Uhalifu, kama ulimtaarifu Kiongozi aliyelengwa Ole Sabaya, kama ulimpatia taarifa. Ukasema hukumpati na wala Kamati ya Ulinzi ya mkoa wa Kilimanjaro, ni kwanini sasa.
Shahidi: Tulikuwa kuwa na....Uhakika wa Taarifa zetu, hatukuona sababu za kuwaambia Watu wengine kwa kuwa tunge Create Pressure.
Wakili wa Serikali: Uliulizwa Wakati Mtuhumiwa wa kwanza anakamatwa palikuwa na Askari Jeshi na Ukasema Hakukuwa na Askari Jeshi
Shahidi: Hapakuwa na Askari Jeshi kwa sababu Mimi Ndiyo nilikuwa Arresting Officer na Nikisaidiwa na Inspector Mahita pamoja na ASP Mahita
Wakili wa Serikali: Uliulizwa kuhusiana na Maandamano Ukasema ni Sheria Inaruhusu lakini kwa Kufuata taratibu eleza Unamaana gani?
Shahidi: Ni kweli Sheria Inaruhusu Maandamano lakini kuna Sheria zingine pia zinaweka taratibu kuwa kabla ya Kufanya Maandamano awe amepata kibali
Wakili wa Serikali: Kibali gani
Shahidi: Cha Polisi
Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali Kuhusiana na Mtu wa Pili katika Maelezo yake kuwa Mtu Mmoja anaitwa Kakobe, Ukasema ukabaini Kuwa Mtu huyo anayeitwa Kakobe ndiyo Moses Lijenje, eleza ni wakati gani ulibaini
Shahidi: Wakati tunawakamata Watuhumiwa walikuwa wawili......lakini tulikuwa tuna Taarifa wapo watatu, Tukiwauliza Yupo wapi Mwenzetu Wakasema anaitwa Kakobe ambaye ndiyo Lijenje.
Wakili wa Serikali: Uliulizwa Swali kuhusiana na Sheria ya Ushahidi Wakati wa Onyo Kuwa section one na Two hukuweka, Ukasema hiyo ni Curable, Ulikuwa unamaanisha nini.
Shahidi: Haiwezi Kuathiri Maelezo ya Kuonywa
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji tunaomba Tukomee hapa.
Jaji: anaandika Kidogo
JAJI: Upande wa Utetezi
Kibatala: Mheshimiwa Tumekubaliana kuwa hatuna Pingamizi lolote
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji tuna Shahidi Mwingine lakini Kabla ya Kuendelea naye tunaomba ahirisho fupi, Ikiwezekana tuweze Ku resume Saa 5:30.
Jaji: Maombi yanakubaliwa, tutarudi Mahakamani saa Tano na Nusu.
Jaji: Kama tumekukwaza Kwa niaba ya Mahakama naomba Radhi, Naomba Radhi kwa niaba ya Utetezi na Ninakushukuru Kwa Ushahidi wako.
Jaji anatoka Mahakamani
---------
JAJI anaingia
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021
Wakili wa Serikali Kidando: Wapo tayari Kuendelea na Mashahidi
Jaji: Upande wa Utetezi Mpo tayari
Kibatala: Tupo tayari kwa ruhusa yako Mheshimiwa
Jaji: Shahidi wa Pili
Wakili wa Serikali: Shahidi amefuatwa
Mahakama ipo kimya ina subiri shahidi aingie
Shahidi amefika
JAJI: Majina shahidi: JUSTINE ELIYA
Jaji: Umri wako
Shahidi: Umri 31, Kabila Mmeru, Dini Mkrito, Shughuli Mkulima
Shahidi: Naapa Mbele ya Mahakama hii kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa ni kweli, kweli tupu Eenheeeee Mwenye Mungu nisaidie
Wakili wa Serikali: Ataongozwa na Wakili wa Serikali Abdallah Chavula
Jaji: Karibu
Wakili wa Serikali: Nitakuwa nakuhoji Maswali utakuwa unajibu kwa Kuelekea kwa Mheshimiwa Jaji
Wakili wa Serikali: Majina yako yapi:
Shahidi: Justine Eliya Kaaya
Wakili wa Serikali: Bw Kaaya Kwa sasa Shughuli zako ni Zipi?
Shahidi: Kilimo na Biashara
Wakili wa Serikali: Kilimo cha aina gani
Shahidi: Cha Mboga Mboga na Nafaka
Wakili wa Serikali: Unamaanisha nini
Shahidi: Mboga Mboga Nyanya, Vitunguu na Karoti na Nafaka, namaanisha Mahindi na Maharage
Wakili wa Serikali: Shughuli hizi unazifanyia wapi
Shahidi: Arumeru Mkoani Arusha
Wakili wa Serikali: Wateja wako hasa ni wanunuzi wa hayo mazao ni akina nani?
Shahidi: Ni watu tofauti Watanzania na Wageni wanaokuja Mkoa wa Arusha
Wakili wa Serikali: Unazifanyia wapi
Shahidi: Mkoani Arusha, wilaya ya Arumeru, Longido na Wilaya ya Arusha Mjini.
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Mwaka 2017 wewe Maskani yako yaliku a ni wapi?
Shahidi: Nilikuwa naishi Longido
Wakili wa Serikali: Wilaya ya Longido ipo Mkoa gani
Shahidi: Arusha
Wakili wa Serikali: Hapo Wilaya ya Longido ulikuwa unajishughulisha na Shughuli zipi?
Shahidi: Kupiga Picha na Kilimo katika Wilaya ya Arumeru
Wakili wa Serikali: Mwaka 2017 ulikuwa unajishughulisha na Kilimo cha aina gani
Shahidi: Nilikuwa nalima Karoti
Wakili wa Serikali: Wateja wako walikuwa ni akina nani?
Shahidi: Waliotoka Sokoni na baadhi ya watu pale Arusha
Wakili wa Serikali: Tueleze sasa hii Shughuli ya Kupiga Picha nayo, Ni Shughuli gani?
Shahidi: Picha za Mnato kwa kutumia Camera na Simu
Wakili wa Serikali: Ulikuwa ukiwapiga akina nani
Shahidi: Viongozi wa Serikali na Viongozi wa Kisiasa
Wakili wa Serikali: Unaweza ukatuambia ni akina nani hasa
Shahidi: Dr. Steven Kemomo Kiruswa Mbunge wa Longido
Wakili wa Serikali: Mwingine
Shahidi: Mrisho Gambo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Gabriel Daqaro aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Na wengine wengi
Wakili wa Serikali: Hao umewataja wa Ki-serikali, Je wa kisiasa
Shahidi: Lengai Ole Sabaya
Wakili wa Serikali: Huyu Lengai Ole Sabaya ulikutana naye wapi mara ya kwanza?
Shahidi: Mwaka 2017 Uchaguzi Mdogo wa Marudio Jimbo la Longido, Akanitaka nikamsaidie Kupiga Picha katika Shughuli zake zingine Mbalimbali
Wakili wa Serikali: Nini Kilijiri wakati huo baina yako wewe na yeye?
Shahidi: Alikuwa Diwani wa Kata ya Kisambasha, Wilaya ya Arumeru alivutiwa na Upigaji wangu wa picha
Wakili wa Serikali: Alikutaka ukamsaidie Wapi?
Shahidi: Katika kata yake ya kisambasha, Wilayani Arumeru
Wakili wa Serikali: Ulipokea Vipi Ombi hilo
Shahidi: Nilimkubalia kwa kuwa ilikuwa ni fursa kwangu
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama baada kukubali lile Ombi Utaratibu wa Ufanyaji kazi wenu ulikuwaje
Shahidi: Longido ni Mbali, hivyo ilinipasa kuhama Longido na Kuhamia Arusha, Nyumbani Kwa Lengai Ole Sabaya, Sehemu Inaitwa Kibanda Maziwa SAKINA
Wakili wa Serikali: Ulifanya kazi na Ole Sabaya na kuishi kwenye Nyumba yake kwa muda gani?
Shahidi: Mwaka 2017 Mpaka Mwaka 2018 July Alipoteuliwa Kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai
Wakili wa Serikali: Wewe ulienda kuishi wapi baada ya Kuteuliwa?
Shahidi: Nilienda Kuishi naye Hai Mkoani Kilimanjaro katika Makazi ya Mkuu wa Wilaya
Wakili wa Serikali: Kwenye hiyo Nyumba ya Ole Sabaya ulikuwa ukiishi na nani?
Shahidi: Yeye Mwenyewe Sabaya na Mke wake Jesca
Wakili wa Serikali: Ulipokuwa ukiishi naye wewe hasa ulikuwa Ukifanya Shughuli zipi
Shahidi: Kufanya Shughuli zake ndogo Ndogo ikiwemo Kumpelekea Nguo zake Dry Cleaner, Ikiwemo Kumpelekea Chai na Chakula Ofisini Kila Siku.
Wakili wa Serikali: Katika hiyo Nyumba ya Mkuu wa Wilaya Hai, Lengai Ole Sabaya Ulikuwa ukiishi na nani?
Shahidi: Nilikuwa nikiishi naye, yeye Mwenyewe na Mke wake.
Wakili wa Serikali: Umeishi Pale kwa Muda gani?
Shahidi: Kutoka July 2018 Mpaka Mwezi wa 10, 2018
Wakili wa Serikali: Nini kilitokea?
Shahidi: Niliamua Kurudi Longido Kuendelea na Shughuli zangu Nyingine sababu nikiacha Mchumba na Kutaka Kusimamia Shughuli zangu zingine za Kilimo.
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama sasa Mwaka 2018 uliporudi Longido unaweza Kukumbuka watu gani katika Medani za Kisiasa Ulianza Kufanya nao Mawasiliano
Utetezi: OBJECTION, Quite Leading kwa Kutaka Kuuliza ni watu gani wa Kisiasa Ulifanya Mawasiliano nao.
Wakili wa Serikali: Shahidi hebu tuambie Ulifanya Mawasiliano na Watu Gani?
Shahidi: Siku Moja nikiwa nyumbani nilipigiwa simu kwenye simu yangu Airtel 0693006700 kutoka kwenye namba ya Airtel 0784779944 na Mtu aliyejitambulisha Kuwa ni Freeman Mbowe
Wakili wa Serikali: Akakwambia kitu gani?
Shahidi: Nilishtuka sana akaniuliza Ujambo?. Nikamwambia sijambo akasema anashida ya Kuniona
Wakili wa Serikali: Ukafanyeje?
Shahidi: Nikamuuliza Upo wapi, Akajibu yupo Arusha
Wakili wa Serikali: Ukajibu Kitu gani,
Shahidi: Nikamwambia Nipo Longido kwa sasa Siwezi Kuja kwa sababu ya Changamoto ya Usafiri
Wakili wa Serikali: Nini Kikatokea?
Shahidi: Akaniambia Chukua Gari Noah Gharama Nitakuja Kulipa Ukifika Arusha. Kwa sababu ya Ile hofu nikamwambia siwezi Kuja
Wakili wa Serikali: Hofu ya Nini?
Shahidi: Kwanza Nikiongozi Mkubwa lakini Pia sina Ukaribu na Yeye
Wakili wa Serikali: Baada ya Kumueleza hayo nini Kilitokea
Shahidi: Aliniambia Subiri nakupigia, akakata simu.
Shahidi: Baada ya Muda akaniambia nipo Njiani nakufuata Longido.
Wakili wa Serikali: Muitikio wako ulikuwaje?
Shahidi: Kwa kuwa alisema yupo Njiani nakuja nikasema wacha nisubiri nisingeweza Kumzuia
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama nini kilitokea
Shahidi: Baada ya Dakika 40 alinipigia Simu kuwa Njoo hapa Uwanja wa Mpira
Wakili wa Serikali: Uwanja wa Mpira wa wapi?
Shahidi: Ndani ya mji Mdogo wa Longido
Wakili wa Serikali: Baada ya Kumueleza hayo Ulichukua hatua zipi?
Shahidi: Nilichukua Bodaboda na Kwenda
Wakili wa Serikali: Tuambie yaliyojiri
Shahidi: Akunichukua Bodaboda Nikaenda mpaka Uwanjani, na Kukuta Gari inaunguruma
Wakili wa Serikali: Ilikuwa ni Majira ya Muda gani
Shahidi: Saa 3 Usiku
Wakili wa Serikali: Baada ya kukuta gari,
Shahidi: Akaniambia Sogea hapa kwenye Gari Kwa namba ile ile ya 0784779944, Akaniambia ingia Kwenye gari Chief acha Kuogopa
Wakili wa Serikali: Kwenye Gari kulikuwa Kuna watu wangapi?
Shahidi: Nilimkuta yeye na Dereva na Nyuma ya upande wa Dereva palikuwa na Mwanamke
Wakili wa Serikali: Alikwambia Dhumuni lake lilikuwa na Ujumbe gani?
Shahidi: Akaniambia kuwa Lengai anamsumbua Sana
Wakili wa Serikali: Lengai ni nani..?
Shahidi: Mkuu wa Wilaya ya Hai
Wakili wa Serikali: Endelea
Shahidi: Akataka nimpatie Taarifa na Shughuli anazofanya pamoja na Watu anaofanya nao kazi pale Hai
Shahidi: Nikamwambia haitowezekana, kwa sababu mimi Sipo tena kwa Sabaya
Wakili wa Serikali: Ulipomueleza haya, yeye alifanya nini?
Shahidi: Akaniambia yeye Kiongozi Mkuu wa Chama Cha Upinzani Kwenye Nchi hii, Hivyo atafanya Vyovyote vile anavyoweza ili nirudi kwa Sabaya Kuendelea na Kazi
Wakili wa Serikali: Muitikio wako Ulikuwa ni Upi?
Shahidi: Nikamwambia haitowezekana kwa sababu nimechagua Kufanya Shughuli zangu Binafsi
Wakili wa Serikali: Nini Kilitokea?
Shahidi: Akaniambia samahani kwa Usumbufu wa Kunisumbua na akanipa TSh Laki 3
Wakili wa Serikali: Nini kikaendelea?
Shahidi: Akaniambia ni za Usumbufu, Tutawasiliana
Wakili wa Serikali: Nini kiliendelea
Shahidi: Tuliagana na aliondoka
Wakili wa Serikali: Baada ya Yeye Kuondoka wewe Ulielekea wapi
Shahidi: Baada ya kushuka kwenye Gari nilimpigia Ole Sabaya simu lakini hakupokea simu
Wakili wa Serikali: Wewe Ulienda wapi sasa
Shahidi: Nilibakia pale pale kwenye Uwanja na Kumpigia Dr Steven Kiruswa na Kumueleza kilichotokea?
Wakili wa Serikali: Wewe sasa Ulienda wapi?
Shahidi: nilirudi Nyumbani Kwangu
Wakili wa Serikali: Ulirudi Vipi Nyumbani kwako
Shahidi: Niliita Bodaboda nikarudi Nyumbani Kwangu
Wakili wa Serikali: Ni wakati gani tena Ulikuja kuwasiliana na Mtu uliye mtaja kuwa ni Freeman Mbowe pale uwanjani?
Shahidi: Mwaka 2020 Mwanzoni alinipigia Simu kupitia Whatsap
Wakili wa Serikali: Kwa namba ipi?
Shahidi: Kwa namba ile ile ya 0784779944
Wakili wa Serikali: Alikuwa na ujumbe gani
Shahidi: Akasema tumepotezana sana Chief
Wakili wa Serikali: Alikupa ujumbe gani?
Shahidi: Akasema anataka tuonane
Wakili wa Serikali: Wapi?
Shahidi: Moshi, wakati huo nilikuwa Arusha
Wakili wa Serikali: We Ukasemaje?
Shahidi: Ngoja nimalizie Kumwagilizia Shambani huku nikishamaliza nitakuja
Wakili wa Serikali: Nini kilitokea Kutokana na ahadi yenu?
Shahidi: Baada ya Kumalizia Shughuli zangu nilipanda Costa na Kumpigia Simu Kwamba naenda
Wakili wa Serikali: Ulipanda Costa Kuelekea wapi?
Shahidi: Moshi Kilimanjaro
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama ukifika hadi wapi?
Shahidi: Baada ya Kumpa Taarifa kuwa Nipo kwenye gari akasema nishuke Machame road.
Wakili wa Serikali: Kwa namba ipi?
Shahidi: ile ile ya 0784779944
Wakili wa Serikali: Ulipomueleza akakupa Maelekezo yepi?
Shahidi: Akaniambia nishuke Machame Road
Wakili wa Serikali: Ipo wapi?
Shahidi: Ipo Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro
Wakili wa Serikali: Tueleze sasa baada ya Kupewa Maelekezo hayo nini kilitokea?
Shahidi: Nilishuka kwenye Gari nikapiga tena simu
Wakili wa Serikali: Simu ipi?
Shahidi: Namba yake ile ile ya 0784779944
Wakili wa Serikali: Ulipompigia simu nini kilitokea?
Shahidi: Akaniambia ni subiri hapo nakuja
Wakili wa Serikali: Nini kilijiri?
Shahidi: Baada ya Muda akinipigia simu kuniambia, Umefika, umekaa Upande upi, Akaniambia Vuka kaa Upande wa Kulia.
Wakili wa Serikali: We Ulikutana na nini?
Shahidi: Palikuwa na Barabara ya kwenda Machame na Nyingine kwenda Arusha na Nyingine Moshi
Wakili wa Serikali: Nini kikatokea?
Shahidi: Ilikuja Gari aina ya Land cruiser V8 Yenye Mlingoti na Bendera ya Bunge ikiwa na Plate Namba zilizoandikwa KUB
Wakili wa Serikali: Nini kilitokea?
Shahidi: Ilisimama Upande wangu, ikashusha Kioo Upande wa Abiria, nikamuona Mwenyekiti akaniambia Panda
Wakili wa Serikali: Baada ya Kuambiwa Upande nini kili tokea?
Shahidi: Alishuka Mtu kutoka Siti ya Nyuma akaniambia pita nikaingia kwenye Gari
Wakili wa Serikali: Enheeeee
Shahidi: Ile gari ilienda Muelekeo wa Kwenda Machame, Baadae tukaingia sehemu ambayo nilikuja Kugundua Hotel ya Aishi
Wakili wa Serikali: Palikuwa na watu gani kwenye Gari?
Shahidi: Palikuwa na Dereva na huyo Mlinzi wake aliyenipisha nikaingia kwenye Gari
Wakili wa Serikali: Mahusiano yenu ya Dereva na huyo Mlinzi kabla ya Siku hiyo yalikuwaje?
Shahidi: Tulikuwa hatufahamiani
Wakili wa Serikali: Ulijuaje aliyekupisha kuwa ni Mlinzi wake
Shahidi: Baada ya Yeye Kunitambulisha kuwa ni Mlinzi lakini pia ni Diwani wa Kata ya kiboriloni
Wakili wa Serikali: Baada ya Dakika 08 Mlifika wapi Vile?
Shahidi: Hotel ya Aishi Machame Wakili wa Serikali: Wewe ulitambuaje
Shahidi: Sababu ya Kibao Kilichoandikwa Aishi Hotel
Wakili wa Serikali: Tueleze sasa yaliyotokea
Shahidi: Baadae tulishuka kwenye Gari Mimi, yeye na Yule Mlinzi wake
Wakili wa serikali: Mlivyoshuka nini Kiliendelea?
Shahidi: Tulielekea Upande wa Mgahawa
Wakili wa Serikali: Umekuwa ukielezea Yeye na Mlinzi wake. Mlinzi wake na Yeye nani?
Shahidi: Freeman Mbowe
Wakili wa Serikali: Baada ya kushuka kwenye Mgahawa
Shahidi: Akasema tuongee kidogo sababu anamikutano kwenye jimbo lake akaniambia niagize Chakula
Wakili wa Serikali: Muda huo ilikuwa saa ngapi?
Shahidi: Saa Saba Mchana
Wakili wa Serikali: Wakati anakutaka Mkutane Moshi ilikuwa ni Saa Ngapi?
Shahidi: Saa Mbili Asubuhi
Wakili wa Serikali: Wewe Safari yako Kuelekea Moshi ulianza Saa ngapi?
Shahidi: Saa Tano kasoro
Wakili wa Serikali: Ulianzia wapi hiyo saa Tano kasoro
Shahidi: Sehemu inaitwa Kilala Wilaya ya Arumeru
Wakili wa Serikali: Alikwambia nini sasa?
Shahidi: Akauliza Mnampango gani Juu ya Mkutano inayoendelea Jimboni
Wakili wa Serikali: Jambo gani lingine alikwambia
Shahidi: Akaomba nimtajie wale wasaidizi wa Sabaya alipokuwa anatembea nao
Wakili wa Serikali: Wewe ulimwambia nini
Shahidi: Nilimwambia sina Taarifa yoyote ya kumwambia kwa wakati ule
Wakili wa Serikali: Nataka kuhusu hayo Majina
Shahidi: Nikimtajia Majina na Yule Diwani akawa anaandika kwenye Kikaratasi
1.Japhet Rwendela
2.Vedastus sibula
3.Mtoto wa Mkulima
4.Sylvester Nyegu
5.Binti wa kichaga
6.Mwalimu Doreen
7.Watson Malimumgu
JAJI: Mtoto wa Mkulima na Binti wa Kichaga ni Majina?
Shahidi: Ndiyo Majina nilivyokuwa nayafahamu wanayatumia kwenye Mitandao
Wakili wa Serikali: Kipi Kingine alikueleza
Shahidi: Nilitoa hizo namba kwenye simu niliwatajia Wakaziandika
Wakili wa Serikali: Lipi lingine alikueleza
Shahidi: Akasema atashughulika nao tutawasiliana na Wewe na Mimi baadae
Wakili wa Serikali: Nini kilitokea Baina yako wewe na yeye?
Shahidi: Akaniaga kasema atanitumia Chochote jioni
Wakili wa Serikali: Ulisema Chochote umaanisha nini?
Shahidi: Gharama zangu za Nauli
Wakili wa Serikali: Ilikuwaje baada ya hiyo ahadi
Shahidi: Hakutimiza hiyo ahadi na pia hakunitafuta baada ya pale
Wakili wa Serikali: Baada ya Makutano yenu pale Aishi Hotel wewe ukielekea wapi?
Shahidi: Nilirudi Arusha
Wakili wa Serikali: Ni wakati gani Mwingine uliwasiliana na Mbowe?
Shahidi: Mwezi 07 Mwaka 2020
Wakili wa Serikali: Tarehe ngapi?
Shahidi: Sikumbuki tarehe