Uchaguzi 2020 Yaliyojiri: Mapokezi ya Mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu na mkutano mkubwa Shinyanga

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri: Mapokezi ya Mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu na mkutano mkubwa Shinyanga

hiyo picha ni msafara wa Lowasa akiwa sumbawanga mwaka 2015 kwenye kampeni Chadema acheni usanii sio msafara wa leo wa Lisu huo!!

View attachment 1556346
Acha ushamba jaribu kui zoom uone Body guard wa lissu.

Pia hata ndani ya gari ukizoom unamuona lissu akiwa amenyanyua mkono kuweka alama ya vidole viwili ya Chadema.
 
Live broadcasting inawaumbua, picha na clip zinazoletwa hapa zimepitia uhariri zile nzuri kwa chama ndio zinatoka, Mbagala na Kawe walifanya live broadcasting ni aibu mtupu, Kawe mkutano ulikuwa kama kampeni za udiwani.
Si ndio vzirui ili chadema isichaguliwe?? Au vipi
 
Hii staili ya uzinduzi wa chadema lazima imchanganye adui..

Ila sijui kama wataweza kumaliza majimbo yote ya uchaguzi.
 
WanaJF

Karibuni kufuatilia mapokezi makubwa ya Mgombea Urais CHADEMA Tundu Lissu hapa mjini Shinyanga.

Lissu anatarajiwa kuhutubia mkutano Mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Joshoni ikiwa ni uzinduzi wa kampeni kwa Kanda ya Serengeti.

Mgombea huyo wa Urais anaambatana na Mgombea Mwenza Salum Mwalimu na Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe

Sisi wa Molemo Media tumesafiri usiku kucha kutokea Mwanza na tupo hapa Shinyanga kuihabarisha dunia.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu ameingia Kanda ya Serengeti (Mara, Shinyanga & Simiyu) ambapo leo atakuwepo Shinyanga Mjini akiambatana na Mgombea-mwenza, Salum Mwalim pamoja na Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe

Picha zikionesha msafara wa Mgombea Urais wa JMT kwa Tiketi ya Chadema, Mhe. Tundu Lissu tangu alipotua Uwanja wa Ndege wa Kahama leo asubuhi. Kisha kuanza safari ya kuelekea Shinyanga mjini ambapo alilazimika kusimama mara kadhaa sehemu mbalimbali kuwasalimia mamia ya wananchi waliosimama barabarani kuzuia msafara wakiomba awahutubie.
View attachment 1556431


View attachment 1556423

Molemo mnakwama wapi? Yaani mkutano mkubwa kama huu mnaunyima spika? Yaani spika hazitoi sauti ya kutosha!
 
Back
Top Bottom