Ni zamu ya Musoma leo.
Rais Mtarajiwa Tundu Lissu atatikisa viunga vya Musoma kwenye Mkutano wa Kampeni leo.
Ni Kama Musoma imesimama kwa ujio wa Shujaa huyu aliye gumzo Afrika na duniani kwa Sasa.
Lissu anayeungwa mkono na Makundi yote hususan wafanyabiashara na Wafanyakazi kote nchini ameapa kufuta Mara moja sheria Haramu iliyowekwa ya kupunguza Mafao ya wastaafu na kurudisha Mara moja Fao la Kujitoa.Serikali ya CCM ilipitishwa Sheria ya kikandamizaji kwamba mtu akiacha kazi ya kuajiriwa hata Kama ana miaka 30 sharti asubiri afikishe miaka 60 ndiyo apate haki yake ya Mafao.Shetia hiyo imelaaniwa na kila mpenda haki lakini serikali ya CCM imeweka Pamba masikioni.
Kwa tathmini iliyo wazi mpaka Sasa Lissu ana uwezekano wa kushinda kwa zaidi ya asilimia 60% Ngome pekee ya Mgombea wa CCM aliyokuwa anatamba nayo ilikuwa mkoa wa Geita hata hivyo Lissu ameiteka ngome hiyo wiki hii kwa kupata mapokezi yanayobaki historia vizazi na vizazi
Tutawaletea yatakayojiri