Yaliyojiri: Mapokezi ya Tundu Lissu Jijini Arusha - Ijumaa 14 Agosti, 2020

Yaliyojiri: Mapokezi ya Tundu Lissu Jijini Arusha - Ijumaa 14 Agosti, 2020

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,358
Ni Ijumaa tulivu.

Kama kawaida jiji la Arusha Kuna ubaridi asubuhi hii.Jiji likiwa katika hekaheka tangu Jana za Maandalizi ya mapokezi ya Mgombea Urais wa Chadema Tundu Lissu.

Kanda ya Kaskazini hususan Jiji la Arusha ni ngome Kuu ya Chadema na akitoa salaam za kunikaribisha jijini humo Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini Godbless Lema alisema mapokezi ya Mgombea wao wa Urais yatazidi Kanda nyingine zote alizokwishatembelea.

Tayari Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe akiongozana na Mwenyekiti wa Kanda ya Kati Lazaro Nyalandu hapo Jana walimlaki Lissu maeneo ya mkoani Manyara tayari kuongozana naye kuingia Arusha leo.

He kweli jiji la Arusha litavunja rekodi leo? Tusubiri tuone.

Molemo Media imekwishawasili jijini Arusha kuwaletea moja kwa moja kitakachojiri katika mapokezi hayo ya kihistoria.

Karibuni...

Taarifa za hivi Punde

Ofisi za Chadema Kanda zachomwa Moto.

Kuna taarifa zilizotujia hivi Punde kwamba ofisi za Chadema Kanda ya Kaskazini zimechomwa Moto usiku wa kuamkia Leo na watu wasiojulikana.Hapa ndipo mgombea wa Urais Tundu Lissu alipaswa kupokelewa kwa ajili ya kudhaminiwa.Tunatarajia kupata taarifa kwa kina zaidi asubuhi hii kutoka kwa viongozi wa chama.

Taarifa ya Awali kutoka Ofisi ya Chama Arusha.

*TAARIFA YA AWALI*

Usiku wa leo, watu ambao hawajatambulika hadi sasa, wamevamia ofisi zetu za Chadema Kanda/Mkoa na Wilaya Arusha, wamechoma moto kwa petrol na kufanya uharibifu mwingine. Tumeshirikiana na jeshi la zimamoto, polisi na wadau wengine hadi sasa.

Taarifa zaidi zitatolewa.

*KATIBU WA MKOA ARUSHA*
*[Ijumaa, 14 Agosti 2020.]*

Saa 3 Asubuhi

Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini Godbless Lema anajitokeza mbele ya wanahabari na kutoa masikitiko yake kuhusu kuchomwa Moto ofisi za chama katika Kesha la ujio wa mgombea Urais Tundu Lissu.

Lema amesema hujuma hizo zinaashiria lengo moja kuvuruga ujio wa mgombea Urais hata hivyo akawatia moyo wananchi wasiyumbishwe na waendelee na mapokezi ya Mgombea Urais Kisha baada ya kuondoka kwake ndiyo chama kitatoa tamko rasmi.

Lissu azungumzia tukio akiwa Karatu.

Akihutubia umati mkubwa wa watu mjini Karatu akiwa njiani kuelekea Arusha Lissu amesikitishwa na vibaka waliotumwa kuchoma Moto ofisi za Kanda ya Kaskazini na akasema mkutano wake wa kusaka wadhamini jijini Arusha utafanyikia hapo hapo ofisi zilipochomwa Moto.

Saa 6.30 Lissu aingia Arusha kwa kishindo kikubwa.

Hoi hoi nderemo na vifijo vinatawala muda huu wakati mgombea Urais Tundu Lissu akikanyaga Ardhi ya Jiji la Arusha huku akiwa ameambatana na Mwamba wa siasa za Tanzania Freeman Aikael Mbowe na Mwenyekiti wa Kanda ya Kati Lazaro Nyalandu.

Pikipiki zisizokuwa na idadi yakiwemo magari na watu kujipanga majiani ndivyo vimetawala mapokezi ya mwana huyu wa Afrika ambaye amepokelewa kwenye viunga vya Kisongo karibu na Uwanja wa ndege
 

Attachments

  • VID-20200814-WA0047.mp4
    2 MB
  • VID-20200814-WA0046.mp4
    1.6 MB
Molemo,

..hapo Arusha anaingia Ijumaa au Jumamosi?

..nimesikia anaanzia Karatu kabla ya kuja Arusha mjini.
 
Back
Top Bottom