Uchaguzi 2020 Yaliyojiri mkutano wa kampeni za Mgombea wa CCM Dkt. Magufuli akiwa Bukoba, Kagera

CCM hoyeee. Mungu kaibariki Tanzania kutupatia JPM. Hakuna Kama yeye never
Ni kweli,kwani hakuna kama wewe au mimi!Mungu kamuumba kila mtu tofauti na mwenzake!Kwa mantiki hiyo sawa!Ila kama unamaanisha hakuna mtanzania anayefaa kuwa Rais ila yeye,hapo sikubaliani na wew!
 
Dr Bashiru Anasema kuwa,wako WANASIASA wanakuja na Sera za MAJIMBO kuligawa taifa....

Amesema,WANASIASA hao;watakatakata barabara kimajimbo,watakata kimajimbo bomba la mafuta kutoka Chongoleani Tanga Mpaka Hoima...
 
Daah!! Huyu mtu sjiu alikuwaga wapi tu" ama kweli, kila kitu na wakati wake

Sio Siri Mzee, umetufaaa Sana Watanzania, najua, huwezi kuheshimika na kuthaminika Kwa kizazi hiki cha leo, kizazi cha nyoka, kizazi pingapinga, kizazi cha starehe, kizazi kisichopenda kufanya kazi, kizazi cha kula bata bila kufanya kazi

Kizazi kinachotaka Uhuru wa kutukana watu, kizazi kisicho na shukrani,. Kwa vile kila kazi aifanyayo mtu, malipo yake ni Kwa Mungu, Mungu atakulipa Kwa kazi nzuri juu Taifa lako ulilolipenda Kwa Moyo wako wote na kulitumikia Kwa nguvu zako zote!

Nitakuchagua tena
 

Hakika Magufuli ni Jembe,Mitano tena ni haki yake.
 

"Ndugu zangu Wanakagera kabla hatujaongea chochote naomba tusimame kwa Dakika chache kuwaombea watoto wetu walioungua na moto na wale wote majeruhi tuwaombee wapone haraka."
Rais Magufuli Kutoka Bukoba, Kagera.
 
Katika dini ya Kiislam kukariri ni dili imekuwa tofauti kwa Shakh huyu muhaya yeye amesoma sala yote katika karatasi kwa kiswahili sara yenye mvuto na matumaini makubwa.

Askofu wa KKKT Kagera naye alikuja na daftali kubwa na kusoma sala yenye mpangilio na mtiririko ambao unaleta matumaini kama ya Shekh.

Pia na Askofu wa katoriki yeye alikwenda mbali zaidi na kuja na kitini kikubwa sana na kushusha maombi yenye mtililiko mzuri wa kuvutia na kubariki.

Ukifwatilia utaona hawa jamaa walikaa zaidi ya siku si chini ya 7 wakiaandaa sara ya kampeni kweli hawa watu ni wasomi tusiwabeze, wanaelewa maana ya usomi.
 

“Napenda pia nitumie fursa hii kutokana na msiba uliotupata kule Kyerwa kuzihimiza mamlaka zote husika nchini ikiwemo wizara ya TAMISEMI na wizara ya Elimu kuhakikisha shule zote zinazingatia masuala ya Usalama na sheria kabla na hata baada ya kuanzishwa na hasa katika masuala ya ukaguzi ili madhara ya moto na ajali mbalimbali kwa shule zetu yasijirudie tena “.
Rais Magufuli Bukoba mjini
 
“Ninafahamu mkuu wa shule ameshikiliwa na jeshi la polisi, mimi ningeomba jeshi la polisi wakati wakiendelea kufanya uchunguzi huyu mkuu wa shule wamuachie pia, ili wadhibiti na kujua kama ilikuwa ni ajali kweli au palikuwa na sababu za uzembe kwa sababu bado hata akiwa nje ya mahabusu nina uhakika ataendelea kushirikiana na polisi katika kutoa taarifa”
Rais Magufuli Bukoba mjini
 
Tundu Lissu ndio Rais tupa kule huyo mshamba na limbukeni wa ndege
 
Kizazi cha mamarioo hawataki kazi kabisa wao wanapenda kila kitu kiwe mezani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…