Uchaguzi 2020 Yaliyojiri mkutano wa kampeni za Mgombea wa CCM Dkt. Magufuli akiwa Bukoba, Kagera

BUKOBA MMEWAVUA NGUO CHADEMA OOOH TETEMEKO LEO WAMEAMUA KUWATETEMESHA
1600275825461.png
 
MGOMBEA Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt John Pombe Magufuli, leo Septemba 16, 2020 ameendelea kupiga kampeni, ambapo baada ya kumaliza wilayani Chato, mkoani Geita, Muleba leo yupo Bukoba Mjini mkoani Kagera Uwanja wa Gymkana.

MGOMBEA Ubunge jimbo la Bukoba Mjini Stephen Byabato amewaomba wananchi wa jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu kuhakikisha wanajenga mnara wa mawasiliano kati yao na Rais Dk.John Magufuli kwa kuchagua Rais, Mbunge , madiwani kutoka Chama Cha Mapinduzi( CCM).

Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Kagera waliohudhuria mkutano wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Magufuli kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu, Byabato amesema katika uchaguzi hakuna sababu ya hao kufanya makosa kama yaliyofanyika uchaguzi wa mwaka 2015 kwa kuchagua mbunge na madiwani wa upinzani.

"Bukoba Mjini tulikosea mwaka 2015 kwa kuchagua upinzani , na hivyo kukata mawasiliano kati yetu na Rais Magufuli.Huu ni mwaka wa kujenga mnara wa mawasiliano,naomba wote tumchague Dk.Magufuli kwa nafasi ya urais,mnichague mimi kwenye ubunge jimbo la Bukoba Mjini pamoja na wabunge wote wa CCM,"amesema Byabato.

Amefafanua kuwa ni kweli maendeleo hayana Chama na ndio maana Rais Magufuli amefanya maendeleo makubwa bila kuombwa na mtu yoyote lakini kwa upendo wake mkubwa kwa wananchi wa Bukoba Mjini na Kagera Mjini ameleta maendeleo.

Ameongeza katika miaka mitano iliyopita chini ya uongozi wa Rais Magufuli wananchi wa Bukoba Mjini kunamaendeleo makubwa yamefanyika na kwamba Sh.bilioni 158 zimetumika kwa maendeeleo."Tunatambua kwamba yote hatukuomba lakini tumezipata fedha hizo kwa upendo mkubwa alionao kwa ajili yetu."

Amesisitiza Bukoba Mjini kuna taa za barabarani wamepata kilometa 13 za lami, wamepata mradi mkubwa wa maji wenye kuzalisha lita milioni 18 wakati mahitaji ni lita milioni 15 kwa siku na hivyo kubaki na ziada ya lita milioni tatu na kwamba yote hayo yamefanyika sio kwasababu waliomba bali yametokana na Rais Magufuli na mapenzi yake kwa wananchi.

Pia Sh.milioni 500 zimetolewa na Rais Magufuli kwa ajili ya vituo vya afya na leo, miundombinu katika sekta ya afya imeboreshwa na kuimarika sana."Hayo yote hatukuomba katika miaka mitano lakini tumepewa.Nawaombeni wana Bokoba, tusifanye makosa tena.Tumchague Dk.Magufuli kwanza jina lake ni kubwa hata ukilitaja unasikia raha.

"Tujenge mnara wa mawasiliano ambao utakuwa rasmi kwa ajili ya kupeleka mawasiliano kati ya wananchi na Rais wetu.Tunataka tukipiga simu kwa Rais tunaambiwa mawasiliano yapo na tunayoomba yanafanyiwa kazi, Bukoba iwe na mawasiliano mazuri na sio ukipiga unaambiwa Not reachable,"amesema Byabato.

----
Sehemu ya Wanachama na Wananchi wa Mkoa wa Kagera waliohudhuria mkutano wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Magufuli kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.

WhatsApp%2BImage%2B2020-09-16%2Bat%2B8.54.24%2BAM.jpeg

WhatsApp%2BImage%2B2020-09-16%2Bat%2B8.54.25%2BAM%2B%25281%2529.jpeg

Kagera pambe sana
 
Attachments

  • a701581f-6182-4acd-8872-dcea7dd48bd8.JPG
    a701581f-6182-4acd-8872-dcea7dd48bd8.JPG
    121.9 KB · Views: 1
Wanakagera hatujasahu ujue ewe john.

Ulituambia twafa Tetemeko halikuletwa na sirikali yako
Ee bhana na leo Wana Kagera wamedhihirisha wazi kabisa wanampenda Magufuli na wanaipenda CCM na hata Kama mnafanya propaganda za kuwafanya wamchukie kwa sababu ya tetemeko wamewapuuuza

Check huo umati

Hakika Bukoba mmetisha sana
IMG-20200916-WA0148.jpg
 
Vitendo vinaongea, Mladi wa maji, Vituo vya Afya, Barabara, Elimu bure, vivuko na meri kwa nini wasijae endeleeni na hoja yenu ya Tetemeko ila Kagera kwa CCM wanachukuwa wanaweka Uwaaaaaaaaaa
1600276642176.png
1600276642176.png
 
Asante Bukoba, asante Kagera kwa kuionyenyesha dunia kuwa mnamuelewa JPM na serikali yake!
 
Hapo Tundu Lissu alikuwa bado hajapita je angekuwa tayari ameshawalisha upupu si ingekuwa balaaaaa.Lissu atakuja kuweka mambo sawa
Ila kimsingi ukiachana na tetemeko na meli hakuna cha maana serikali ya CCM imefanya bukoba.
 
MGOMBEA Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt John Pombe Magufuli, leo Septemba 16, 2020 ameendelea kupiga kampeni, ambapo baada ya kumaliza wilayani Chato, mkoani Geita, Muleba leo yupo Bukoba Mjini mkoani Kagera Uwanja wa Gymkana.

MGOMBEA Ubunge jimbo la Bukoba Mjini Stephen Byabato amewaomba wananchi wa jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu kuhakikisha wanajenga mnara wa mawasiliano kati yao na Rais Dk.John Magufuli kwa kuchagua Rais, Mbunge , madiwani kutoka Chama Cha Mapinduzi( CCM).

Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Kagera waliohudhuria mkutano wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Magufuli kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu, Byabato amesema katika uchaguzi hakuna sababu ya hao kufanya makosa kama yaliyofanyika uchaguzi wa mwaka 2015 kwa kuchagua mbunge na madiwani wa upinzani.

"Bukoba Mjini tulikosea mwaka 2015 kwa kuchagua upinzani , na hivyo kukata mawasiliano kati yetu na Rais Magufuli.Huu ni mwaka wa kujenga mnara wa mawasiliano,naomba wote tumchague Dk.Magufuli kwa nafasi ya urais,mnichague mimi kwenye ubunge jimbo la Bukoba Mjini pamoja na wabunge wote wa CCM,"amesema Byabato.

Amefafanua kuwa ni kweli maendeleo hayana Chama na ndio maana Rais Magufuli amefanya maendeleo makubwa bila kuombwa na mtu yoyote lakini kwa upendo wake mkubwa kwa wananchi wa Bukoba Mjini na Kagera Mjini ameleta maendeleo.

Ameongeza katika miaka mitano iliyopita chini ya uongozi wa Rais Magufuli wananchi wa Bukoba Mjini kunamaendeleo makubwa yamefanyika na kwamba Sh.bilioni 158 zimetumika kwa maendeeleo."Tunatambua kwamba yote hatukuomba lakini tumezipata fedha hizo kwa upendo mkubwa alionao kwa ajili yetu."

Amesisitiza Bukoba Mjini kuna taa za barabarani wamepata kilometa 13 za lami, wamepata mradi mkubwa wa maji wenye kuzalisha lita milioni 18 wakati mahitaji ni lita milioni 15 kwa siku na hivyo kubaki na ziada ya lita milioni tatu na kwamba yote hayo yamefanyika sio kwasababu waliomba bali yametokana na Rais Magufuli na mapenzi yake kwa wananchi.

Pia Sh.milioni 500 zimetolewa na Rais Magufuli kwa ajili ya vituo vya afya na leo, miundombinu katika sekta ya afya imeboreshwa na kuimarika sana."Hayo yote hatukuomba katika miaka mitano lakini tumepewa.Nawaombeni wana Bokoba, tusifanye makosa tena.Tumchague Dk.Magufuli kwanza jina lake ni kubwa hata ukilitaja unasikia raha.

"Tujenge mnara wa mawasiliano ambao utakuwa rasmi kwa ajili ya kupeleka mawasiliano kati ya wananchi na Rais wetu.Tunataka tukipiga simu kwa Rais tunaambiwa mawasiliano yapo na tunayoomba yanafanyiwa kazi, Bukoba iwe na mawasiliano mazuri na sio ukipiga unaambiwa Not reachable,"amesema Byabato.

----
Sehemu ya Wanachama na Wananchi wa Mkoa wa Kagera waliohudhuria mkutano wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Magufuli kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.

WhatsApp%2BImage%2B2020-09-16%2Bat%2B8.54.24%2BAM.jpeg

WhatsApp%2BImage%2B2020-09-16%2Bat%2B8.54.25%2BAM%2B%25281%2529.jpeg

#JPM2020 #CCM #mitanotena #mitanotenayajpm #achakaziiendelee #achakaziiendeleenajpm
kg1 (3).JPG
kg1 (12).JPG
 
Ila kimsingi ukiachana na tetemeko na meli hakuna cha maana serikali ya CCM imefanya bukoba.

Baadhii tu ni kama yafuatayo:
1. Kugeuza mapori yaliyotumika kwa uhalifu na ujambazi kuwa hifadhi ya taifa ( Burigi; Chato; Ibanda na Lumanyika)
2. Kulipa madeni ya kahawa kwenye vyama vya ushirika.
3. Kukarabati shule za sekondari za Kagemu, Bukoba, Rugambwa na Kahororo.
4. Kujenga shuke mpya za sekondari mbili; Nyakato na Ihogo kwa gharama ya shilingi bilioni 14.
 
Tunamsubiria mzee was kusakafia.anajinasibu eti maendeleo hayana vyama,lakini huwa uhalisia wake unajionyesha kwrnye kampeni.mngese thaaaaana mshua wa kinje
 
Baadhii tu ni kama yafuatayo:
1. Kugeuza mapori yaliyotumika kwa uhalifu na ujambazi kuwa hifadhi ya taifa ( Burigi; Chato; Ibanda na Lumanyika)
2. Kulipa madeni ya kahawa kwenye vyama vya ushirika.
3. Kukarabati shule za sekondari za Kagemu, Bukoba, Rugambwa na Kahororo.
4. Kujenga shuke mpya za sekondari mbili; Nyakato na Ihogo kwa gharama ya shilingi bilioni 14.
Bado hujaiongelea Bukoba hapo juu.

Acha kuchanganya bukoba na kagera
 
Mataa ya barabarani kwa nini yanachukuliwa ni maendeleo?
 
Back
Top Bottom