Kenya 2022 Yaliyojiri Uchaguzi Mkuu wa Kenya: William Ruto ashinda kiti cha Urais, apata 50.49% ya kura

Kenya 2022 Yaliyojiri Uchaguzi Mkuu wa Kenya: William Ruto ashinda kiti cha Urais, apata 50.49% ya kura

Kenya 2022 General Election
Siasa za Kenya ni ngumu tangu zamani. Nakubali process zao za kupiga kura na kuhesabu kwa sasa ni nzuri na ziko open kuliko sisi lakini ukiingia kwa undani kuna makandokando mengi sana. Kuna mgombea mmoja wa ubunge ameua mtu kwa risasi na mpaka sasa hajulikani aliko. Ni mgombea wa ushirika wa Ruto na watu wanasema anasubiri Ruto ashinde ili ajitokeze akitegemea atalindwa na mamlaka. Yaani mtu hata urais hajaupata lakini tayari wameanza kuonyesha uongozi wa hovyo.
Kenya kuna mijitu katitili sana zaidi ya Magu
 
Hili swali hawezi jibu,tangu mchana yeye ana matokeo yake.Hata ukienda kwa Social Media za Wakenya hukuti hizi figure zake
Nimeshangaa sana ujue[emoji23]
Maana nachojua NTV ndiyo wako mbele zaidi, na mpaka sasa Ruto ana 3.6M votes, Odinga ana 3.4M votes...
Sasa hii ya jamaa ya 5.2M votes sijui kazitoa wapi..
 
Ruto anaongoza kwa asilimia 52 na Odinga 46 kwa mujibu wa mahesabu ya Daily Nation. Hali imekuwa tofauti kwani zile zilizotegemewa kuwa zitakuwa ngome za Odinga haikuwa hivyo na amepata ushindani mkubwa sana kutoka kwa Ruto.
Aloo mbona niliona humu walisema odinga kafanya come back ya nguvu...imekuaje tena
 
Huyu hajawahi soma story ya Robert Ouko ,Tom Mboya,JM Kariuki n.k
Mauaji ya Kenya yalianza rasmi 1963/4 baada ya kuuwawa kwa Pio Gama Pinto na inner circle ya Jomo Kenyata by then.Gama alikuwa mshauri mkuu wa Jaramogi Oginga Odinga hawa walikuwa wana mrengo wa kijamaa. Badae 1966 or 1968 akaja kuuwawa yule wakili aliyemuwakikisha Jomo Kenyatta kwenye ile kesi ya The Kapenguria six Argwing Ghodhek then Tom Mboya then Josia Mwangi Kariuki.......etc
 
Mkenya mmoja alinisimulia kuwa OgingaOdinga baba yake na Raila waligombana na Jomo Kenyatta baba yake Uhuru.

Ikumbukwe wawili hawa walikuwa viongozi na marafiki wakubwa.

Baada ya ugomvi wao walilaaniana.

Oginga alimlaani Kenyata kuwa

1. Hatakaa Ikulu na kweli alikuwa hakai ikulu.
2. Haruhusiwi kuvaa viatu vya dukani. Hapo sijui kama ilitmia
3. Hatapanda ndege. Inasemekana mpaka anakufa hakupandaga ndege. Kifupi hakuwahi kwenda ng'ambo baada ya laana hiyo.

Kenyata alimlaani Oginga laana moja tu kuwa
" Watoto wa Odinga watakuwa maarufu sana ila hawatakuja kuwa ma(rais)".

Tafadhali mawe sihitaji ni maoni tu.
Kiufupi Mzee Oginga ndiyo alitakiwa kuwa Rais wa kwanza wa Kenya and by that time alikiwa maarufu kuliko mwanasiasa yoyote yule.Huruma yake dhidi ya Kenyatta ndio iliyomponza.
 
Ndo kina nani hao?
Mboya na Kariuki walikuwa mawaziri enzi za Jomo Kenyata. Walikufa vifo vya kutatanisha. Tom Mboya labda angekuwa Rais baada ya Kenyata. Huyu alikuwa very intelligent naona Kenyata aliogopa popularity ya Mboya. Ouko yeye alikufa kipindi cha Moi. Huyu nae mwili wake ulikutwa umechomwa moto kabisa.
 
Back
Top Bottom