Nimekupata mkuu, ila Kwa Zama hizi siku ya Tano hii Leo uhakiki tu, vituo 46000 tu, we huon kama matokeo yanatolewa upya hiv
Kila kituo kina kura za vyeo sita vinahezabiwa, i.e Gavana, Mbunge, seneta, rais, mwakilishi wa wadi, mwakilishi wa wanawake... hio tayari huchukua masaa 24 baada ya kituo kufungwa... Zikiisha PO wa kituo anazisafirisha mabox na fomu hadi HQ ya eneo bunge lake na kuzipatia mkubwa wa IEBC wa bunge aneitwa RO, PO akifika kwa RO anapata laini kubwa ya kila PO anaregesha mabox sita na form zake hio laini itaisha baada ya masaa 12 angalau, ikitoka hapo RO anahezabu matokeo ya kila cheo, na kujumlisha, yani kama ni mbunge anahesabu matokeo ya form zote kwahivyo kama form za eneo bunge ni 300, basi kila fomu lazima aipitie na kuandika hayo majibu kwa kila cheo kwahivyo hizo ni form 300 * 6 = 1,800 forms, hii nayo ni kama siku mbili angalau ndo atakua amemaliza hesabu yote kisha atangaze mshindi wa eneo bunge na wawakilishi wa wadi...
Kwahivyo hapo kuna siku tatu tayari zishapita, kutoka hapa sasa ndo kila RO anapanda ndege kusafirisha original forms zake za Rais hadi nairobi ndo zianze kuhesabiwa moja moja hesabu rasmi sasa, Kwahivyo siku ya tatu au siku ya nne baada ya uchaguzi ndo RO's huanza kuwasili nairobi na original forms zake ndo sasa angojee kwa line kukabidhi form zake zote
Nimeweka mmoja wepo wa form original iliopigwa picha, nimeipata kwa hio tovuti nilioweka hapo awali, sasa hizi ndo from 34A ambazo ni mpaka zote 46,229 zifike Nairobi