Mkuu,naona unajaribu kulinganisha watu tofauti kabisa na mazingira tofauti, yani maji na mafuta.
Kwanza Lowassa alikuwa amekwishatupwa nje ya mfumo kitambo sana, vipi Uhuru alikuwa amemtupa Ruto nje ya mfumo?
UhuRuto walikuwa na mpango wa kupishana Ikulu kama marafiki au washirika, unadhani Wakenya wangekubali huo ujinga? Wangepigana na kuuana.
Unadhani ni kwanini Wakenya wamemkataa Raila? Huoni kwamba Ruto ameshinda kwa kura za hasira kwasababu walikuwa wanamuona Babu Raila ni ProjectUhuru?
Nakurudisha Tanzania, hivi unajua ni kwanini WanaCCM na hata Watanzania walikuwa wanamchukia Membe?😂
Nakurudisha tena Tanzania, unaamini kabisa Magufuli alimshinda Lowassa 2015?😂
Naomba nikuache ujinyonge na kamba uliyojinunulia.