Yaliyojiri Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam: Maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara

Yaliyojiri Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam: Maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara

Tunasherehekea siku ya Uhuru, je ni kipi cha kujivunia toka waingereza waondoke mpaka leo
 
Yule jamaa ni sikio la kufa. Inaonekana haamini kama ni yeye ndo mkuu wa mkoa. Unajua mtu ukitokea mtaani tu ukapewa nafasi ya kukaa kiti cha mbele lazima utaonesha hali ya kuchanganyikiwa kwa sababu hukutegemea kuwepo hapo. Ni sawa na mtu aliyeokota bilioni moja bila kutoa jasho, lazima achanganyikiwe tofauti na aliyezipata kwa kupigika.

Mkuu safi sana na umemaliza kila kitu hadi sina tena cha kuongezea hapo. Message sent and delivered!
 
Wimbo wa taifa sasa.!

Hizi sherehe mwaka huu zimepoa sana aisee.!
 
Nani aliona alichofanya JPM wakati anarudi kwenye jukwaa kuu baada ya kumaliza kukagua gwaride, alikuwa analeta utani huku akitanua mikono kuiga mwendo wa kijeshi wa haraka
Ahahaha,kumbe na wewe umemuona!mwangalie MOTOCHINI,Ameiweka Hapo Juu!
 
Huyu dogo ataishia pabaya.!

Mkuu tusimwombee hayo mabaya labda yamtomkee bali tujitahidi tu kumsaidia kumwelekeza ili basi aweze kubadilika na naamini kama atayasikia au kuyaona haya tunayomwambia atabadilika tu. Kamwe tusiombeane mabaya kwani na yeye anatafuta kama sisi tunavyotafuta isipokuwa tu ana mapungufu madogo sana ambayo ni ya Kiushamba zaidi ambayo kwa Wataalam wa Psychology kama sisi ni rahisi kumwelekeza na kumbadilisha kwani yanarekebishika. Ni Kijana mzuri na Tanzania ya sasa inamuhitaji ila tu ni hayo mapungufu.
 
Mama salma kikwete yupo?

Jecha nae amekuja na nini kutoka Zanzibar?
 
Gwaride limekamilika. Linajiweka tayari kuondoka uwanjani kupisha ratiba nyingine kuendelea. Yatafuata maonyesho ya makomandoo na kikosi cha wanamaji wakiwa na kilo 65 migongoni mwao.
 
Umenikumbusha katibu tarafa mmoja pale Iringa aliitwa MBIGILI alikuwa na kiherehere sana.Mwaka 1987 alikuja Rais mzee Mwinyi pale kiwanda cha Tancut basi mzee Mbigili akataka kuwahi kumfungulia mlango wa gari Rais,kwa kasi ya umeme hatukuona kilichotokea ila tulimshuhudia Mbigili amelazwa chali pembeni ya barabara akiwa hajitambui/amezimia

Makonda siku atajichanganya, kiusalama hakuna anaeaminiwa. Taasisi ya rais haina partner. Inataratibu zake
 
Back
Top Bottom