Yaliyojiri Yanga Vs FC Platinum

Yaliyojiri Yanga Vs FC Platinum

Heti tuwe wazalendo.Kwa uzalendo upi waliowahi kutufanyia?.Nikikumbuka ya TP MAZEMBE Machozi yananitoka.Nanyie azam mnaitakia yanga ushindi kwa lip?Mmesahau walivyowafanyia kwa al marek pale chamanzi?.Mimi siwezi kuwa mnafiki kutoka moyoni nawatakia ushindi mnono tena wa goli nyingi platnum fc.
 
Kufungwa kubaya jamani we acha tu toka tumefungwa na mtani nilipotea kwenye jukwaa hili kama nipo kifungoni.

Ila YANGA naombea leo msituangushe maana naweza likimbia jukwaa hili kwa muda mrefu.

Tupige moyo konde ndugu yangu.
 
Japo sipendi Yanga washinde lakini kwa hiki kikosi naona kwa mbali kuna ushindi. Mabeki wa kati wajitahidi tu kutoa back up inapotokea mabeki wa pembeni wamepanda hasa beki mbili huwa anapenda sana kupanda ingawa yeye huwa anajitahidi kurudi mapema wakati timu inashambuliwa, beki wa kushoto huwa ni mzito kidogo na kwa sababu hiyo kama atakuwa akipanda sana itabidi Kelvin na Twite wafanye kazi ya ziada kumpa cover up la sivyo kufikia saa 12 tutakuwa tunaongea mengine.

Ikitokea Makapu kazidiwa itabidi kocha aue winga moja na kubakia winga ya wizi wizi ili Niyonzima awe anacheza muda mwingi kati na Telela kuja kumlinda Makapu ili kuimarisha kiungo wakati timu inashambuliwa.

Pamoja na hayo bado sisi watu wa kwa Mugabe tunawatakia ushindi Platinum.

Kama we ni kijana ukiwa mtu mzima utakuwa mchawi..game la leo sio mtani jembe support kitaifa bwana
 
Back
Top Bottom