Yaliyomfika Rais Ali Hassan Mwinyi katika utawala wake 1985 - 1995

Yaliyomfika Rais Ali Hassan Mwinyi katika utawala wake 1985 - 1995

Shida kubwa mzee wangu kila kitu unakihusisha na uislam naona kuna shida kubwa hapo. Nadhania ndio mjumbe hapo akkatumia neno uchawa.
Choka...
Sijahusisha kila kitu.

Nimeandika kitabu: "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924-1968)the Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism."

Hapa ndiyo mwanzo.

Kitabu kilibadili historia ya TANU na Nyerere.

Historia hii ilionyesha mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Sijahusisha kila kitu.

Ikiwa kwako ni shida kwangu ni jambo la kujivunia.

Kuhusu uchawa.
Wala hilo halinishughulishi.
 
1988 Kwny Halmshauri kuu Hayati Mchungaji Mtikila alitoa waraka wa matusi ya nguoni kabisa kwa Mzee Ally Hassan Mwinyi

tulishangaa kabisa tena alikuwa akiungwa mkono na wahafidhina
Msitake tuwakumbushe yale mapicha ya magono yaliyochapishwa UDSM miaka ile tulikaaa kimyaaa
 
Uko bias sana ndo tatizo hilo mkuu.

Ni kwamba huujui upande wa mazuri kwa wakristo au unapambania uislam hivyo mambo ya ukristo hayakuhusu??

Nadhani majibu mabaya na kukosa heshima ya wadau humu yanatokana na wewe kuegemea upande mmoja tu ambao ni uislam.
 
Kwa nini nijisumbue kiasi hicho?Unachokiongea mbona kiko wazi sana.Kwako viongozi wa Kiislam ndo viongozi wazuri na walioleta maendeleo katika nchi hii na hawakufanya maovu.Wakikosea.unasema.wanasakamwa kwa ajili ya uislam wao.No.wonder ukasema ushindi wa dp world ni ushindi wa ccm na waislam
Nan...
Umenituhumu kuandika historia yenye ubaguzi.

Jibu lako ni wewe kusoma name index ushuhudia wazalendo nilioandika historia zao na hawa si Waislam: Raikes Kusi, Rawson Watts, Cecil Matola, Denis Phombeah, Alexander Tobias kwa kuwataja wachache.

Unasema huwezi kusumbuka.

Ikiwa huwezi kusumbuka gharama yake ni hii kuwa utabaki hujui kitu.

Mimi niliyesumbuka nasomwa ndani ya Cambridge Journal of African History, nasomwa ndani ya Dictionary of African Biography, nasomwa katika vitabu nilivyoandika nk.

Ikiwa hii ndiyo nafasi yangu katika kuijua historia ya Afrika unadhani wewe una uwezo wa kusimama na mimi kujadili chochote?
 
Uko bias sana ndo tatizo hilo mkuu.

Ni kwamba huujui upande wa mazuri kwa wakristo au unapambania uislam hivyo mambo ya ukristo hayakuhusu??

Nadhani majibu mabaya na kukosa heshima ya wadau humu yanatokana na wewe kuegemea upande mmoja tu ambao ni uislam.
Vishu...
Niko bias kwa kurejesha historia iliyofutwa?

Aliyefuta historia ya babu yangu katika kuunda TANU na mie niliyeandika historia ya babu yangu nani aliye bias?

Hii kuwa sina heshima JF wewe umepata wapi?

Mimi Mwandishi Bora Jukwaa la Historia miaka miwili mfululizo 2021 na 2022.
 
Hujaelewa.
Nilimaanisha watu kukukosea heshima kwa majibu yao mabaya, yasiyo na staha.

Na kwa maana hiyo hii ni vita binafsi ya kutaka babu yako atambuliwe mchango wake?
Uislam umeingia vipi ilhali aliepigania uhuru ni babu yako??
Babu yako aliuhusisha vipi uislam na uhuru??
 
Ulizungumza au ulidanganya na watu wakawa wanakutazama tu wapime upeo wa dhamira zako.
Maana toka vurugu za mwembe chai.....dhamira yako uliiweka wazi kuifanya Tanzania kua jamuhuri ya kiislamu na kuweka utamaduni wa kiarabu kwenye utamaduni wetu wabantu....!!
NB: TUNAJUA UMESAFIRI NA SISI TUMESAFIRI PIA.....AU UNATAKA TUTAMBIANE HAPA KILA MMOJA ALIPOSAFIRI..???
Nelson...
Inaelekea huijui Northwestern University na ni watu gani wanaalikwa kuzungumza kwenye chuo hicho.

Si suala la kusafiri hili.

Ni suala unaalikwa kuzungumza chuo kikuu.

Vyuo havialiki ovyo.
Kuna vigezo.

Mwembechai huijui historia yake.
Unahitaji kusoma historia yake.

Serikali imejifunza na haitarudia tena kosa lile.

Nina paper nilizungumza Kenyatta University, Nairobi.
 
Hujaelewa.
Nilimaanisha watu kukukosea heshima kwa majibu yao mabaya, yasiyo na staha.

Na kwa maana hiyo hii ni vita binafsi ya kutaka babu yako atambuliwe mchango wake?
Uislam umeingia vipi ilhali aliepigania uhuru ni babu yako??
Babu yako aliuhusisha vipi uislam na uhuru??
Kujibu bila adabu ni ukosefu wa elimu ya somo.

Ukiwa na elimu ya unachojadili matusi hayapati nafasi.

Uislam umeingia kwa babu zangu kukataa Father Bonnet kuwawakilisha Waafrika wakaunda African Association 1929 na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933.
 
Shida ya mleta mada ni udini, karibu kila kitu anakileta na kukitetea kwa mrengo wa dini ya kiislamu. Hii sio sawa na sio sahihi. Leo anamzungumzia Mwinyi hapa kwa misingi ya kidini, hivyo atampamba kwa lolote kwa sababu Mwinyi ni muislamu.
Hizi mada zenye mlengo wa udini huwa najiuliza sana lengo lake nyuma ya pazia ni lipi.
Kuna baadhi ya Watanzania wana hamu sana ya kuishi kwa kubaguana kwa misingi ya dini.
Siasa na dini haziendani. Mwanasiasa atahamasisha misingi ya udini akiona mambo yanamuelemea ili atetewe lakini yakikaa sawa anasahau kila kitu.
Watanzania tuachane na hii misingi tunayoipandikiza maana mbegu yake itakuja kustawi tungali hatupo.
 
Hii [emoji115] sababu ina mashiko zaidi.
Kweli mkuu
 
Nelson...
Hili kwangu ni jipya.
Unanifananisha mimi na Malcolm X?

Nitampata wapi mimi huyu genius.

Umekosea kuandika jina lake.

Angalia spelling.
Mnafanana utumwa wa akili kwa wakoloni wa kiarab...!!!Ungekua genius usingehamasisha vurugu za mwembe chai mzee wangu
TYPING ERRORS KAWAIDA...AU WEWE HUKOSEI???
 
Nelson...
Inaelekea huijui Northwestern University na ni watu gani wanaalikwa kuzungumza kwenye chuo hicho.

Si suala la kusafiri hili.

Ni suala unaalikwa kuzungumza chuo kikuu.

Vyuo havialiki ovyo.
Kuna vigezo.

Mwembechai huijui historia yake.
Unahitaji kusoma historia yake.

Serikali imejifunza na haitarudia tena kosa lile.

Nina paper nilizungumza Kenyatta University, Nairobi.
Wewe umealikwa na mabepari wa kizungu....basi umevimba kichwa😂🤣🤣🤣 athari za ukoloni wa elimu!!!!
KUHUSU MWEMBECHAI
Wewe ndio ulihamasisha vurugu za mwembe chai......ila unakataa unadai ulikua Saudia.....!!!!
Ukawaponza watanzania wasio na hatia
 
Vishu...
Niko bias kwa kurejesha historia iliyofutwa?

Aliyefuta historia ya babu yangu katika kuunda TANU na mie niliyeandika historia ya babu yangu nani aliye bias?

Hii kuwa sina heshima JF wewe umepata wapi?

Mimi Mwandishi Bora Jukwaa la Historia miaka miwili mfululizo 2021 na 2022.
Babu yako yule mzulu ambae baba yake aliyeletwa na wajerumani???
Mwandishi bora wapi?????
Na historia ipi ya wabantu unaijua wewe mzee wangu zaidi ya udini??
 
Mnafanana utumwa wa akili kwa wakoloni wa kiarab...!!!Ungekua genius usingehamasisha vurugu za mwembe chai mzee wangu
TYPING ERRORS KAWAIDA...AU WEWE HUKOSEI???
Nelson...
Sijahusika na vurugu ya aina yoyote.
Ikiwa una ushahidi ulete hapa peupe uonekane.

Usinivunjie heshima yangu pasi na sababu.

Kesi ya Mwembechai ilikwenda mahakamani na inafahamika.

Typos ni kawaida.
Nimekugutua tu.

Wengi hulikosea.
 
Babu yako yule mzulu ambae baba yake aliyeletwa na wajerumani???
Mwandishi bora wapi?????
Na historia ipi ya wabantu unaijua wewe mzee wangu zaidi ya udini??
Nelson...
Nimemkusudia babu yangu khalis Salum Abdallah Mmanyema na yeye pia baba yake aliingia Tanganyika na Wajerumani akiwa askari akitokea Belgian Congo.

Walikuwa pamoja na Kleist Abdallah Sykes katika Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na katika African Association hadi 1947 babu yangu alipohama Dar-es-Salaam na kwenda Tabora.

Wakiishi jirani nyumba zinatazamana na wote waajiriwa wa Tanganyika Railways katika miaka ya 1920.

Hili la dini nimekujibu kwa ushahidi madhubuti kuwa nimeandika historia ya mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Field of Inquiry.
Corrective History.

Historia hii imepokewa vyema katika vyuo vikuu vinavyosomesha African History.

Haina uhusiano wowote na dini.
Doctronaire.

Historia ya Wabantu.

Nimeandika kitabu cha Maisha ya Rajabu Ibrahim Kirama kutoka Uchaggani.

Kitabu hiki kilizinduliwa Muslim University of Morogoro (MUM).

1709916224350.png
 
Wewe umealikwa na mabepari wa kizungu....basi umevimba kichwa😂🤣🤣🤣 athari za ukoloni wa elimu!!!!
KUHUSU MWEMBECHAI
Wewe ndio ulihamasisha vurugu za mwembe chai......ila unakataa unadai ulikua Saudia.....!!!!
Ukawaponza watanzania wasio na hatia
Nelson...
Naelewa kiwango chako cha kuelewa mambo.

Nimekutambua kwa kutazama unavyoandika.

Unahitaji elimu zaidi.
Mjadala mfano wa huu hutii alama !!!!

Kanuni za uandishi ni dot tatu tu ...
Huchanganyi herufi kubwa na ndogo.

Mimi niko tayari kukusomesha hapa ukapata maarifa.
 
Vishu...
Niko bias kwa kurejesha historia iliyofutwa?

Aliyefuta historia ya babu yangu katika kuunda TANU na mie niliyeandika historia ya babu yangu nani aliye bias?

Hii kuwa sina heshima JF wewe umepata wapi?

Mimi Mwandishi Bora Jukwaa la Historia miaka miwili mfululizo 2021 na 2022.
Basi historia hiyo irekebishwe bila kuhusisha udini. Tunayomengi sana kujifunza kutoka kwako ila sasa kila historia hiyo inapohusisha sana uislam inatutoa kwenye mood ya kufuatilia mafunzo unayoyatoa. Inakuwa kama vile unaugomvi na ukristo. Shida ndiyo inakuwa hapo mzee wangu
 
Back
Top Bottom