Yaliyonikuta Ziwa Rukwa sitokaa niyasahau

Yaliyonikuta Ziwa Rukwa sitokaa niyasahau

Nimesahau chajaa
IMG-20220905-WA0013.jpg
 
Safari ya kuelekea ziwani ikaanza tukapita vijiji kadhaa ,.baada ya Saa nzima tukaingia nankanga Kijiji Cha mwisho kabla hujalifikia ziwa. Hiyo ilikuwa yapata Saa mbili hivi ,tulikatiza kwenye mapori yaliyoshona kweli kweli Kila muda nikawa nahisi tunakaribia kufika na jamaa ananipa Imani (mdogo wangu tunakaribia kufika .) Ilifika Saa Saba mchana jua limekuwa Kali
Mshushe mshushe we mse...e. Nikagundua wale jamaa wako siliasi wanatuuua!! Hapo sauti ikaniambia nijiteteee ! Nikaanza kupiga kelele jamani nisaidieni Mimi sio mwizi ni mwanafunzi nimepewa lifti tu na huyu jamaa hata mm cmjui .lile jamaa lenye roho mbaya likasema hayo maneno utaenda kumwambia yesu kwamba wewe ulikuwa mwanafunzi da!! jamaa yangu Fred kavuliwa nguo zote wakamfunga na nyavu nikasikia wanashauriana hawa tukamtupe kwenye fonka pale Kuna mamba wengi ndio niligundua hapa duniani Kuna watu wanaroho mbaya uusiombe ukutane nao!

Jamaa wanamtoa vidole kimoja kimoja wanamhoji maswali kujibu hawezi kapigwa sana .Mimi wamenipa kisogo kwanza ila ndo nimepasuliwa sana huwezi kunitazama mara mbili na nguo zote wamechukuwa nimebaki uchi wa mnyama! Mwingine anakuja anashika korodani anavuta anavyotaka .kiujumla nilijua hata nikipona wakiniachia sitaweza kuwa mwanaume Tena! Walitupeleka mpaka hapo wanapaita fonka! Yaani ni sehemu ambayo mto unaingilia Kuna kuwa na mamba wengi sana maeneo hayo huwezi kutembea hatua mbili usimuone mamba !! nikajua utani nikaona wanajiandaa kumnyanyua jamaa wamtupe!!

Oyaaaa mfunge mikono tukimtupa asiogelee! Kuna jamaa alikuwa anaitwa mesha mwamba alikuwa na mateso ya kuogofya anamchoma choma visu makalioni .nikimwangalia natamani kama kungekuwa bastora nijipige risasi maana nilijua wakimalizana na huyo jamaa lazima watahamia kwangu !sikuwahi kwenda kanisani nilijikuta ndani ya moyo naomba maombi mazito ambayo sio Kwa uwezo wangu na nyimbo za tenzi zikinijia kichwani Huku nakumbuka wadogo zangu ambao nimekuja kuwapigania inamaana sitawaona Tena na hata kaburi langu hawatakuja walione popote !

Wakamaliza kumfunga kamba jamaa kama utani wengine wakamshika miguu wengine mikono wakaanza kuhesabu Moja..mbili.,...tatuuuu pwaaaaa! Lahaula! Nikasahau maumivu nikakodoa Kwa hofu kuangalia kama jamaa ataibuka ! Lo kimya zikapita kama dakika kumi wote wamekaa kimya Huku jamaa anaeitwa mesha anaandaa kamba za kunifunga Mimi ..ghafla nikasikia kupwaaaa!! Yule jamaa kaibuliwa juu kuangalia vizuri anagombaniwa na mamba zaidi ya watatu !! Nikalia sanaaaa kupita kiasi nikamkumbuka mamaangu kwamba angekuwepo huenda hayo yasingenikuta !!

Nakufa kifo kubaya sana ,ni Bora ningeendelea kulala njaa nyumbani kuliko kufa kifo Cha aina hii !! Yule jamaa mamba walimchana chana nikiwa naona Kwa macho ,,Kuna wakati slomotion ya lile tukio Huwa inajirudia kichwani mwangu!!? Oyaaaa mfunge kamba tuondoke Hawa mamba Leo wamefurahi kinoma noma !! Wale jamaa Sasa wote wakanigeukia Mimi Kila mtu anapiga anapotaka Huku nafungwa kamba miguuni na mikononi ! Wakaanza kunilisha vikambale vibichi vilivyooza vinanuka mabaki ya kwenye mitumbwi Yao !! Oyaa unajifanya unaomba sana Sasa hapa tunataka uombe Hawa mamba wasikutafune ila wakubebe wakutupe nje!!! We si mlokole mwiziii!!

Jamani jamani naombeni basi mnisikilize..nikajitetea lakini wapi ! Kuna jamaa kaniuliza wewe kwenu wapi ? Nikamjibu Kwa tabu sana maporomoko tunduma! Ni kama Kuna mtu kahamaki ! We ni mtoto wa nani ? Nikamjibu haraka Mimi ni mtoto wa Mzee kayuni ! Aaaah ! Mzee kayuni yule muuza mitumba yule shot! Nikamjibu ndio huyo huyo!! Nikasikia oyaa mfungueni huyu sio mwizi ni mdogo wangu kabisa huyu !! Haaaaaa!! Nikashusha pumzi nikamshukuru mungu sana !

Japo walianza kulaumiana ooh kasema ni mwanafunzi we si unamuona bado mdogo huyu !! Twende nae kempu !!! Mmechelewa kusema hii itakuwa kesi ikitokea amekata moto itakuwaje ? huyu amekwisha kabisa tumtupeni hii kesi hii !!! oyaa dogo unanisikia ? Nikamjibu Kwa tabu sana ...nikaona mtumbwi anaenda Kasi kuelekea ufukweni ndani ya moyo nikiendelea kumshukuru mungu sana!! Itaendeleaaa
 
Back
Top Bottom