Kukaa sana kwa amani tunalewa sio polisi, uhamiaji, JW au wapi tuko vizuri. Tatizo ni kukaa na imani kwamba jeshi ni kwa ajili ya vita tu, zana (sio silaha) za kijeshi zina dual use ukiwa nazo zitatumika sana kwa civilians kuliko mara moja kwa miaka kadhaa usubiri vita.
Jana nimeona mabasi ya JWTZ yamejaza wanajeshi wakashuka mikono mitupu, sanasana walichosaidia ni kusogeza watu pembeni ili magari ya wagonjwa na viongozi wapite. Jambo ambalo mgambo anaweza.
Nchi zenye majeshi yenye bajeti, zilizokaa chonjo unakuta military ina search and rescue helicopters kadhaa za nchi kavu na majini, ikitokea mafuriko au meli kuzama wanajeshi wanawahi. Kule Bukoba ajari ya ndege tungeona Navy wanatumia ujuzi wao kama wangekuwa na small base Bukoba au Mwanza, badala yake wavaa yeboyebo kina Majaliwa ndio walionekana.
Hizohizo helicopters zinatumika kuzima moto mkubwa ukiwaka mjini, au milimani kama Kilimanjaro kule moto huwaka mara nyingi.
Hapa kwenye hili jengo tungeona Engineering Brigade ambayo imefundishwa vitu kama kutengeneza airstrip ya haraka wakati wa vita, kurekebisha barabara na madaraja kama Bailey bridge, kuwa na floating piers kusafirisha mizigo ya dharura kwenye mito, kujenga base kwa haraka, kufanya demolition au kuokoa kama strategic factories, buildings zimeharibiwa na adui.
Ingekuwa hivyo tungeona jeshi wanafika na zana zao wanafanya kazi kwa haraka na kwa ufanisi zaidi maana discipline ya kuwa haraka wanakuwa nayo, mafunzo ya gharama kubwa wanayo, vifaa vya uwezo zaidi wanavyo.
Sasa bongo bajeti kama hiyo haitengwi.