Yaliyotokea kwa ACT Wazalendo kwenye chaguzi Ujiji kwa Polisi kuilinda CCM kuiba kura, 2024/25 yanawasubiri CHADEMA, mtafanya nini yakitokea?

Kwa upande mwingine naona kama CCM wanajua nini watakachofanya, ujue haya mambo ya uchaguzi wakati mwingine ni kucheza na akili za wapiga kura tu, na bahati mbaya CCM tayari wanazifahamu akili zetu.

Nachoona kitachoenda kutokea kwenye chaguzi mbili kubwa zijazo, haitakuwa CCM watapora complete kama ilivyokuwa 2020, No!, watachofanya this time ....

Huko majimboni, watahakikisha wanagawana majimbo yale yenye ushawishi na upinzani, hasa Chadema.

Mfano, kama Chadema itashinda Arusha Mjini, basi sitashangaa CCM kulazimisha washinde Moshi Mjini, kama Chadema itashinda Iringa Mjini, basi sitashangaa CCM kulazimisha washinde Mbeya Mjini hata kama kura zao hazitoshi.

Ile maana ya nusu mkate ambayo alikuwa anaipinga Lissu huku baadhi ya wapinzani wengine wakiifurahia ndio itakwenda kutokea hapa, unapewa hapa, unanyimwa pale hata kama ulistahili, then unakosa mandate ya kudai umeibiwa, ukilalamika watakujibu mbona pale mmeshinda kwa tume hii!, mchezo unaishia hapo.

Na wala sio ile nusu mkate wapinzani wanadhani watapewa tu majimbo yote wanayokubalika ilimradi CCM irudi ikulu, No, hii nusu mkate itagawanywa kote hata hadi majimboni, Samia ataambiwa na CCM wenzake mama wewe tulia pale utazame mchezo..

Huu mchezo utachezwa ili kuepusha kelele nyingi za tumeibiwa kama ilivyokuwa 2020. This time itakuwa mnapewa nusu, mnatuachia nusu mpende au msipende.

So, at the end of the day itakuwa aliyepata amepata, na aliyekosa amekosa, maisha yanaendelea...
 
Naunga mkono wizi wa kura.
 
Tena ilitakiwa wawatandike marungu, unalalamika kuibiwa wakati mwizi unamjua.
 
Dawa ni vyama vya upinzani kujitoa kwenye uchaguzi na kuunda rebel movement. Tuingie msituni tu.
 
Bwashee ile kitu Chadema walifanyia Julius Mtatiro 2015 jimboni Segerea ndio itawakuta na wao

CCM majimboni hawakubali kabisa habari za Nusu mkate na hakuna wa kuwalazimisha

Ndio sababu Sugu atagombea Makete πŸ˜‚πŸ”₯
 
demokrasia ni mambo ya kuhuni na ulaghai.
wananchi tunasisitizwa kupiga kura na kurudi nyumbani kusubiri matoke.
 
Shida kubwa ya bwana kabwe( licha ya kuondoka Kwa mchongo) ni msalti wenzake wanaongoza mapambano ya kuhakikisha mambo yanawekwa sawa yeye na watu wake wanakwamisha..
Note: kwenye siasa hakuna urafiki zito na viongozi wake walijue hili..
CCM huwa hawana fadhila !
Tenda wema uende zako !!
 
Bwashee ile kitu Chadema walifanyia Julius Mtatiro 2015 jimboni Segerea ndio itawakuta na wao

CCM majimboni hawakubali kabisa habari za Nusu mkate na hakuna wa kuwalazimisha

Ndio sababu Sugu atagombea Makete πŸ˜‚πŸ”₯
No way Nusu mkate ni lazima watapewa wale ambao wanaogopewa kwa influence zao kwa wapiga kura !!

Kwani majimbo ndiyo yanayotangaza matokeo au ni just mukubwa mmoja aliyepewa mamlaka hayo ?!
Na sioni anawezaje kukaidi agizo πŸ˜…πŸ™πŸ™
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…