Yamenifika shingoni sijui la kufanya mimi

Hili huwa naliona ndo bora lakin kwa ninavomjua ndo atanipa makwazo makubwa ,,,,kinachoniuma ni kuona aman na baba yangu haipo
Kaka kuna wewe na kuna yeye mzee.
Mzee wako ni mtu mzima anatambua nini anachofanya,sio kwamba haoni anachofanya na hajui anachofanya.
Sasa unaumiaje juu ya mtu ambaye anatambua anachofanya!??
Wewe jipange ukishajipanga chomoka nenda unapopajua utaanzisha maisha yako kwa utaratibu sahihi.
Ila ukiondoka usiwatusi wala usiwavunjie adabu,ondoka kiadabu tu.
 
sherehe sio kitu cha kulalamikia am 30's sijui sherehe yoyote ile mpaka saiv sio basidei mahafari au ndugu yake na hayo
 
Mdau kumbe wenye degree ndio mko hivi?

Pole lakini kwa matatizo.
Ulivyohitimu Darasa la Saba ungeendelea na mambo mengine, ungekuwa mbali sana.
 
Pole mkuu kwa unayopitia, shirikisha ndugu wa baba ako kama mashangazi, kaka zake baba ako na babu yako ili mmalize hizo tofauti zenu.
 
Habari,
Pole kwa sintofahamu unayopitia.

1: Kuna mambo yanakuwa magumu kuyasemea kinagaubaga, kwani maelezo yako yameanzia katikati ya mwenendo mzima wa maisha yako na mzazi. Na umejikita kwenye upande hasi zaidi wa maisha yenu.

2: Suala jingine ni kusikiliza/kupata maelezo ya upande mmoja. Ili mtu aweze kuwatibu/kuwapatia mwafaka ni vyema kuwasikiliza wote watatu: baba, mama, mtoto na lia wakati mwingine kuhusisha jirani vs walimu wako.

3: Ni vyema kujua kwa watoto wengine kama wapo, je wao wanamahusiano yapi na wazazi?

Ushauri wa jumla:
1: Pata ndugu, jirani, kiongozi wa dini au mtu yeyote anaeheshimika miongoni mwenu na anaewafahamu ili aweze kuwasikilizeni na kuwasaidia kupata mwafaka kati yenu.

2: Kwako, kwa makosa yoyote mliyowahi kukoseana basi uwe tayari kuanza upya na kwa wema na wazazi wako.

3: Fahamu, kwa umri ulionao wewe utakuwa nani kwenye maisha ni wajibu wako kwa sasa kwa elimu na umri uliofikia.

4: Pamoja na yote, baba bado kuna aliyofanya yawe hasi au chanya kwa njia moja au nyingine amechangia mpaka hapo ulipo hivyo tambua hata yale machache aliyoweza kutimiza.

Hii inatokana na jinsi ulivyoandika mwanzo mwisho ni mambo hasi tu. Mfano: baba hakukupatia pesa kwa kadri ipasavyo, ila ulipataje hela ya ku-save wakati uko shule?
Ni mambo ya kawaida wazazi kutofikia matamanio ya watoto.

Kwa ujumla, kuna pengo kwa kila sehemu hivyo mnahesabiana nakosa likely kwako na wazazi.

Turudishe nyoyo zetu nyuma kwani hata kama ukianza maisha binafsi, ugumu wowote kwenye maisha unaweza kukuletra taharuki ya kuwa inahusiana na sintofahamu toka kwa wazazi.
 
Kwenye maisha jaribu kubalance shobo lia na anayelia na wewe,nenda na anayeenda na wewe,akikukataa na wewe mkatae.
Yani iweje mambo madogo hivi yakuletee msongo wa mawazo.Ukijifunza kubalance shobo maisha yatakuwa simple sana
 
Ahsante sana mkuu kwa kunitia moyo ubarikiwe
 
Ahsante sana mkuu kwa kunitia moyo uba
😁😁😁 nimekuelewa mkuu
 
Kwenye maisha jaribu kubalance shobo lia na anayelia na wewe,nenda na anayeenda na wewe,akikukataa na wewe mkatae.
Yani iweje mambo madogo hivi yakuletee msongo wa mawazo.Ukijifunza kubalance shobo maisha yatakuwa simple sana
Sawa nimekuelewa mkuu wangu
 
Better live your life , usitafutie maisha nyumbani
Go far away and expect nothing from no one

Disappointment comes for those who trust must😭😭😭
Well,,, i understand what you say
 
Kwenu mko wangapi mmezaliwa na huyo baba yako!? Je kama una ndg zako je hao nao Baba yako ana wa treat vp!? Tafakuru!!
Tupo wawili huyo mwingine wa kike ashaolewa mimi ndo first born
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…