Yanayoendelea ndani ya uongozi wa CCM na serikali yanatafakarisha



Si mkajadiliane huko haya mambo yenu ya familia?
 
Ukiona hivyo ujue bado hujaelewa dhima ya mchora katuni.
Dhima ya mchora katuni imeishia kwenye Ccm/Chadema na mgao wa sahani za ubwabwa kwa wapiga kura.
Lakini nyumba na ghorofa za nyasi tupu hata wewe ulikuwa haujazitafakari.
 
Wewe ndiye mdau Jf unayeielewa vizuri hali halisi ya Tz na raia wake ilivyo.

Kama ulivyokwisha kusema 'kupendwa' huonekana kwa mwitikio wa raia, hizo zingine ni ngonjera, chuki zao, kununuliwa au kampeni chafu.

Kiuhalisia Makonda ni kiongozi mzuri na mwenye uwezo wa kutatua changamoto na ni mtu anayekubalika sana, hilo wakubali ama wakatae lakini ukweli unabaki pale pale.
 
Kikwete ni tatizo linawazidi uwezo wa kulitatua kwa sasa, ni tatizo linalochanganyika na suluhisho la matatizo ya kiuongozi ya juu kabisa.

Anategemewa na anajua kuwa anategemewa hivyo anayo nguvu ya kufanya kazi nyingi nyuma ya Rais Samia, kwa ufupi ushawishi wake haukwepeki, tunaishi kwa kutegemea fadhila zake na hilo kwa muda mrefu ujao ni suala baya kwa mustakabali mzima wa Tanzania.
 
Ni vizuri sana anavyofanya Nchimbi kumpinga Makonda kwani huyu bwana akili zake ni mbovu kabisa na wote wananwona anafaa akili zao pia ni mbovu kabisa.
Anajirekodi akisikiliza taarabu ya kumpamba Samia, huwezi kumuona mkuu wa mkoa yoyote akifanya ujinga wa namna hiyo.

Ni masuala ya kitoto na inaonekana anamjua boss wake vizuri na anafanya hivyo akijua muitikio wake utakuwa vipi kuhusu hiyo video.
 
Kuongea kwa niaba ya wananchi sio hulka ya CCM hii yenye ushawishi wa JK, hata kidogo hawana sifa ya aina hiyo.

JPM alipendwa na kuaminiwa kwa sababu alijua kujiweka karibu na mwananchi wa kawaida kwa vitendo, hakuonyesha kutawaliwa na kuitukuza mali ya dunia hii ambayo anakufa na kuiacha. Aliifahamu hekima ya kiuongozi na akajitahidi kuiishi japo ubinadamu ulimzidi nguvu.

JK na Samia wana hulka ya kuiabudu dunia na anasa zake ambayo ina msingi wa tamaduni za kwao za asili yaani wamelelewa hivyo tangu utotoni. Hawana uwezo wa kuzitumikia mali na wakati huo huo wakamtumikia Mungu {kwa maana ya kuwa mtumishi wa watu}.
 
Kabisa mkuu, ni kama ilivyokuwa 2015, bila Dkt Magufuli CCM tulikuwa tumepoteza uchaguzi tena bila chenga maana kila mpiga kura aliamini ni Dkt Magufuli pekee anaweza kuivusha CCM. Same kwa Makonda tangu alipoteuliwa uenezi alionesha matumaini kwa wapiga kura tena kwa mwitikio ambao hata Dkt Samia Mwenyekiti wetu hawezi kumfikia, ilikuwa salama ya CCM kuhakikisha Makonda wanamtumia kukihuisha Chama. Ila kwa sasa nakuhakikishia CCM bila watu kama akina Makonda haibebeki, maana wapiga kura kule vijijini wanaamini CCM hao hao baadhi ya viongozi wa juu walimuua Dkt Magufuli ili waibe, na kuuza rasilimali za nchi. Na moto wa akina Mbowe na kampeni zao siyo za kudharau wananchi wanaelewa kabisa. Sijui kama CCM itapata mwenye akili ya kujua kesho yake 2025. Na kibaya zaidi tena kibaya zaidi ni kundi kubwa la Dkt Magufuli kupitia wabunge aliowaweka bungeni kwa mkono wake na lile kundi alilolikata Dkt Magufuli kwa mkono wake wa chuma, hayo ni makundi nayaita Dynamics “ukilizingua kundi mojawapo” linahamia chadema na kila kundi lina ajenda ya udhaifu wa serikali ya Dkt Samia na dhihaka dhidi ya mpendwa wao Dkt Magufuli, kwa hiyo 2025 tutegemee chochote kutokea. Mtu pekee anayeweza kuivusha CCM ni Paul Makonda tena akiwa kama Katibu Mkuu wa CCM chama kinaweza kuvuka kwa sababu Dkt Nchimbi hana ushawishi kwa wapiga kura, yes anaweza kuwa na ushawishi ndani ya CCM na mfumo ila hana ushawishi kwa masikini. Na akitaka kujilinganisha na Dkt Kikwete atakosea, kikwete 2005 na alikuwa na popularity ya ajabu yaani watu walimpenda bila hata kuongea, ila baada ya Kikwete kushidwa kuzuia wizi alichukiwa mpaka leo na wapiga kura wa leo wanataka kiongozi anayekemea wizi, anawajibisha na analinda maslahi wa walio wengi kwa kuhakikisha wachache pia maslahi yao yanakuwa second priority.
 
Mkiwa na Rais mwanamke wa nchi kama ya Tanganyika yenye taasisi kama Bunge, mahakama, TISS, PCCB, AG nk dhaifu katika kusimamia utendaji wa serikali mnategemea nini?

Ni lazima mambo yawe hovyo tu kwa sababu pembeni mwa mwanamke huyu lazima atakuwepo mshauri au kundi la washauri wanaume waovu kadhaa kumshauri na kumwelekeza kusimamia mambo vile watakavyo wao kwa manufaa yao na sio ya nchi...

Lakini inakuwa ni hatari zaidi mambo hayo anayoshauriwa yanapokuwa yanaihusu nchi na ustawi wa wananchi...

Kwa hiyo shida hapa ni "Rais Mwanamke" na sio kitu kingine chochote..

Hao kina Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli hawakuwategemea wala ku - rely kwenye ushauri wa watangulizi wao ktk kufanya maamuzi kuhusu nchi kwa sababu walikuwa ni wanaume - free & independent men...

Bila shaka mmenielewa japo kuna baadhi wanaweza kudhani siwapendi wanawake au nadharau uwezo wao. Ukweli ni kuwa Nawapenda sana wanawake, siwadharau wanawake lakini ukweli ni kuwa hakuna mwanamke wa kuweza kubeba jukumu la uongozi mkuu wa nchi hususani ya kwetu Tanganyika.!!
 
Uliyoongea ni madini matupu umetema.

Ninaona Samia anayumbishwa na kakikundi ama mtu fulani, hatawali kufuata falsafa zake na utashi wake.
.
Kila nikiigeuza geuza orodha ya ninaowajua walioko juu huko, ninashindwa kumhisi mchawi kwa kuona kila sura hapo Samia anaimudu kwa kuifanya lolote apendavyo.

Ukija na uchawa wao, kila mtu kuanzia Pm ni kusifia na kuabudu, ndiyo hapo ninavurugwa napotezwa.

Kwa utata na mkoroganyo huu, ndiyo maana watu wanamhisi Jk kuendelea kututawala kwa remote control.

Haiwezekani mtu kakiheshimisha chama kwa muda mfupi na matokeo ya raia kukikubali chama halafu aondolewe ghafla!

Hako kakikundi ama ni mtu basi ana nguvu sana kuliko Samia mwenyewe kwenye maamuzi nchi hii.
 
Huyo mwanamke angekuwa mpaka leo hii ni makamu iwapo Magufuli angekuwa anaishi mpaka dakika hii, tukumbuke ni mpango wa Mungu. Kwa matakwa yetu ya kibinadamu Magufuli angeachia madaraka mwaka 2025.

Hivyo tusiegemee kwenye hoja ya uanamke wa Samia, waliopendekeza jina lake ni binadamu kama mimi na wewe na hawakuona kwa namna yoyote ile kuwa mwisho wa JPM ungekuwa ni March 17 2021.

Huyo huyo mwanamke amekuwa na bahati mbaya ya kuletwa huku bara na kupewa cheo na JK, kwake JK ni sawa na kiongozi anayeendelea kuwa hai miaka na miaka, hawezi kuusahau mchango wa JK katika uongozi wake hata akija kustaafu.

Tatizo ni mipango ya Mungu namna inavyofanya kazi, alitaka mpaka muda huu wastaafu wote isipokuwa JK wawe wameshatangulia mbele ya haki, tatizo lipo kwa hiyo JK namna asivyoonekana kujali wala kuguswa na vilio vya watu huku mtaani.

Ana unafiki kwa kumuangalia tu akiwa anaongea majukwaani. Hajali na haonyeshi kabisa kujali n mtu yupo kwa ajili ya tabaka fulani la juu.
 
Makonda anauweza uongozi kwa maana ya ufuatlliaji wa maagizo ya kiserikali lakini hana kabisa busara wala hekima.

Alimsingizia Lowassa kwamba ana mtoto wa nje, ili amchafue tu. Akaenda msibani kule Arusha akisahau kuwa anayemzika ni yule yule aliyemtungia uongo.

JPM alianzisha siasa za kibabe na za ajabu sana hivyo Sabaya, Makonda na Hapi wakawa wanaingia moja kwa moja kwenye siasa hizo chafu.

Kuamini kwamba Makonda eti anaweza kuivusha CCM ni sawa na kufilisika kabisa kimtazamo.

Hana hoja za kwake mwenyewe za maana. Ni mtu anayetumika kuanzisha 'michezo' ya kisiasa ya kuhamisha akili za jamii wakati serikali ikiwa inataka kufunika suala fulani lenye kuhojiwa kwa kina na jamii.
 
Upo sawa ila ukiangalia kwa jicho la pembeni utagundua kizazi kilichopo kinahitaji mtu wa aina gani ili wampigie kura. Ndiyo maana nchi kama Ukraine wanachagua rais eti muigizaji matokeo yake wapo vitani mpaka leo. Kwa ufupi mfumo unatakiwa ufanye kazi kuhakikisha nchi inapata viongozi sahihi. Na ndiyo maana cde Dkt Nchimbi naona kabisa hana agenda ktk nafasi ya KM ila kwingine anaweza faa sana hasa nafasi ya Makamu wa rais etc ila kwenye CCM inahitaji mikikimikiki ambayo kwa upole wake na hekima naona kabisa ni ngumu sana CCM kutoboa
 
Makonda na Nchimbi ni wanasiasa wa marika mawili tofauti na wana misingi tofauti ya ukuaji wao.

Nchimbi ana hoja kwa watu wa rika lake na makuzi aliyopitia pia Makonda ana hoja kwa watu wa rika lake.

Rais SSH katizama mvuto wa Makonda kwa watu wanaomuelewa anapozungumza. Mzee Kikwete bado ana nguvu na ushawishi kwenye siasa za Tanzania na anao uwezo wa kuzima kabisa ndoto za Rais Samia. Mtandao wake kautengeneza kwa miaka mingi, japo kiuhalisia simuoni akikubali kuonekana mbaya wakati historia ya nchi hii itakapokuwa ikiandikwa.
 
Uchomoe kama unakuwasha kwani lazina ubebe mimba husiyopenda baba yake?
 
Mkuu andiko lako kimsingi linamuhusu JK, tunakuomba uthibitishe jinsi JK anavyoingilia maamuzi ya Raisi aliyepo sasa hivi. Punguza chuki mkuu.
Jk inajulikana na kiongozi mroho hajawai tokea kwenye ili bara la Afrika....keshajimilikisha kila kitu ila hatosheki...kaona haifai sasa anatumia vijana wake mkumtusi mama...Na sisi tukiwa bega kwa bega na Makonda wala hatuwezi kubali.
 
Ni hakika umegonga penyewe, na ndiyo maana vyama vikongwe hushindwa uchaguzi. Ktk mambo ya uongozi wa biashara huwa tunasema biashara huzaliwa na kukua kupitia wateja kupenda product na inafika wakati unahitaji kubadili mbinu ili kuweza kuendana na matakwa ya wateja, Dkt Nchimbi na Dkt Kikwete hawaoni kabisa ila Dkt Magufuli aliona mapema ndiyo maana akawa adui yao. Ila nakuhakikishia kama wakiendelea hivi kuelekea uchaguzi, aisee hali itakuwa ngumu sana tena itakuwa zaidi ya 2010 na 2015, maana wapiga kura wa sasa ni kile kizazi kinachoelewa CCM ni chama cha kulinda mafisadi etc, yaani ukikiambia eti Amani hakijui maana mauaji ya Rwanda na Burundi haviyajui. Dkt Samia namshauri bora aahirishe uchaguzi, katiba mpya ipatikane na asigombee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…