Yanayoendelea sasa hivi nchini ni hatari kwa uhai wa chama kilichopo madarakani na baadhi ya viongozi waliopo Serikalini

Yanayoendelea sasa hivi nchini ni hatari kwa uhai wa chama kilichopo madarakani na baadhi ya viongozi waliopo Serikalini

Huwezi kutumia Siasa katika kutoa majibu yanayohitaji ujuzi wa Kitaalamu. Sasa hivi kanywea kama piritoni uwezo huo hana tena. Tusubiri wakati wanajadiri ripoti hiyo halafu tuone mchango wake hapo Bungeni ndio mtajua huyu ni nani hasa.
Aibu kubwa sana
 
Kwa ufisadi mkubwa ulioibuliwa na CAG uliofanyika awamu ya tano, makamu wa Rais wa kipindi hicho anakuwaje msafi ilihali ndiye aliyekuwa mtendaji wa karibu zaidi na Rais?

Tukiacha siasa, ni dhahiri kabisa haya yote yametendeka kutokana na uzembe wa mwendazake na wasaidizi wake akiwemo Rais wa sasa.

Msemakweli ni mpenzi wa Mungu.
Ebooh! Kwani Yeye ndiye alikuwa anaagiza hazina wafanye malipo?

Hahusiki na haya ndio maana aliagiza CAG kwamba asing'ate ulimi.
 
Usiwe kama mtu usielewa huyo alikuwa amebanwa hata kusema hawezi mwendazake aliifanya nchi kama kampuni yake
Kwahyo Samia ambaye alikua makamu, ni msafi kabisa. Ila tu Rais?

Yeye kama makamu wa Rais anakuaje msafi kwa yote hayo? Hivi ni chuki tu kwa Magu au kuna cha zaidi?
 
Ushawahi ona wapi Waafrika wanajiuzulu sababu ya kashfa...?
 
... magufuli kafanya mengi mazuri japo mabaya pia yapo..... nikionacho mimi lile kundi la wanamtandao wa ccm wanataka kurudi ndani ya Chama Kwa gia ya kumchafua magufuli ili jambo watafanikiwa ila Nchi itarudi mikononi mwa kashifa kama za esco Richmond epa na kagoda mambo ya daudi bilali yatajirudia....tutashuhudia twiga akipanda ndege kwenda warabuni nk
Muhimu viroba na kutekana kusiwepo tu
 
Lawama zinaenda kwa nahodha wa chombo kwani ndio huwa na kauli ya mwisho! Halafu kuna kitu kinanishangaza iweje lawama mzikatae wakati sifa alikuwa anapewa peke yake? Ukikubali kushangiliwa ujue pia kuna kuzomewa! Hii kule mkekani tunaita both team score
 
kwenye familia marehemu akifa unafikiri jambo gani hutokea?
 
....ni Kweli katiba ilikanyagwa je Bunge letu lilitimiza wajibu wake wa kuisimamia serikali? Kama Bunge nalo halikutimiza wajibu wake mpaka haya yakatokea spika anatakiwa kuwajibishwa Kwa kushindwa kutumia mamlaka yake mpaka Nchi inapata hasara ya mabilion huku Maisha ya wananchi yakizidi kuwa magumu
Kwa kujua kuwa wanakanusha katiba wajiwekea kinga ya kutoshtakiwa. Kumbuka kama kuna suala nyeti bungeni linalohusu kupiga kura, mfano kura ya kutokuwa na imani na spika, haiwezekani hata siku moja uongozi wa bunge ikakubali ipigwe kura ya siri, itapigwa kura ya wazi. Sasa ni mbunge gani wa CCM ana ubavu wa kusema ndiyo naunga mkono hoja ya kumuondoa spika! Bunge nalo ni maigizo tu. Wanapitisha bajeti isiyokuwa na ununuzi wa ndege wala SGR, Lakini ndege zinaaminika, kinachofuata ni kurap pongezi tuuu! Bila Transparency na Rule of Law hayo mambo ya ufisadi yatadumu milele na milele. Ndiyo maana tunasema kuliko kujenga daraja la surrender Bora angejenga mfumo wa utawala ikiwemo katiba mpya yenye kuzingatia maoni ya wananchi ikiongozwa na rasimu ya tume ya Warioba! Hata Mama Samia ikilikwepa hili, hawezi kufika mbali. Serikali, Bunge, Mahakama na vyombo vya habari viwe independent!
 
Kwahyo Samia ambaye alikua makamu, ni msafi kabisa. Ila tu Rais?

Yeye kama makamu wa Rais anakuaje msafi kwa yote hayo? Hivi ni chuki tu kwa Magu au kuna cha zaidi?
Hakuna Mwenye Shida. Tatizo lipo kwa Wakaguzi. Sheria za ukaguzi wa Mahesabu ya Serikali kwanza ziliandaliwa na Wahasibu kwa kushirikiana na Wagavi. Lengo lao likiwa ni kuhakikisha Wananufaika kulingana na taaluma zao. Sasa baada ya Mfumo kubadilika kuanza kutumia F akaunti wao walikuwa hawana pa kupigia kutokana na utaratibu kubadilika fedha za miradi kusimamiwa moja kwa moja na Wananchi ndiyo maana miradi iko poa.
Mifumo ya kuisimamiwa na wananchi wanafanya manunuzi kwa bei ya Soko siyo ile ya kujiongezea mfano bati la 20000 linanunuliwa 50000 au 60000 na kuingiza hasara Serikali.
Kutokana na Hali hiyo kuna watu hapo walichanganywa na Mfumo huo ambao ni
1. Wazabuni
2. Wakandarasi
3. Wahasibu
4. Wakuu wa Idara
5. Wakurugenzi
6. Wakaguzi
N.k. Kutokana na Hali hiyo wanatumia kila mbinu kuu disaapoint Mfumo wa usimamizi wa Wananchi moja kwa moja.
Na Uzuri wananchi tumeisha jua janja yao. Wakituzingua na cc ni wajumbe tuna Jambo letu. Ukituzingua na cc tutakukanyaga ili tu tusonge mbele.
 
Mama kama Mama
Mwenye madudu alietakiwa kujiuzulu ndo kaenda zake.
Nafasi imechukuliwa na samia
Haina tatizo
salehjembefacts-20210406-0001.jpg


Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Habari zenu ndugu zang watanzania mliopo humu. Ndugu zang nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu sana yanayoendelea nchini, hasa kuhusu tuhuma za ufisadi zinazoelekezwa kwa aliyekuwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati John P Magufuli.

Najua na inajulikana wazi tu kwamba tokea tulipopata uhuru mpaka leo hakuna awamu ambayo haikufanya madudu iwe madogo madogo au makubwa.

Kila serikali iliyoingia madarakani ilifanya mazuri na mabaya pia kwahiyo hili ni jambo la kawaida kwa tawala zote zilizopita kuanzia mwaka 1961 mpk 2020.

Kinachosikitisha ni kuona kila ufisadi au kila jambo baya lililofanyika, au lililofanywa na kiongozi au mtu yoyote aliekuwa katika serikali ya awamu ya tano lawama zote anabebeshwa hayati Magufuli.

Tunafaham kwamb kuna mamb mengi ya kimaendeleo na mazuri lkn watu kadhaa sijui kwa maslahi au faida ya nani wameamua kumchafua.

Na kwa vile mtu akishafariki hawezi kujitetea kwa shutuma zote zinazoelekezwa kwake iwe za kweli au za uongo, sasa sisi tulio hai tutaendelea kumtetea ili kufuta kbs uchafu unaotengenezwa kwa ajili yake.

Najua hata na yeye alikuwa binadamu kwa hiyo kukosea ni jambo la kawaida lkn asibebeshwe makosa na matatizo mengine ambayo hakuyafanya kwa masilahi ya kundi la watu fulani.

Najua kwa sasa wanaomchafua ambao baadhi yao wapo ndani ya CCM na wanaona fahari sana hayati Magufuli kuchafuliwa ili ionekane kwamba yeye na Serikali yake hawajafanya chochote lkn wakumbuke kuwa huyo wanaemsema ameshakwenda zake, sasa kazi kubwa imebaki kwao walio hai.

Mwaka 2025 unakuja wamejipangaje kupangua hoja za wapinzani wa CCM na serikali kwa ujumla kuhusu ufisadi huo unaoongelewa sasa hivi?
Kama na wewe ni great thinker, basi Taifa hili bado lina safari ndefu. Muda huu uliotumia kuandika pumba hizi ni Heri ungelimsaidia mkeo kuchambua mchele.
 
Back
Top Bottom